Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,075
Hili linaweza lisiwahusu wote bali waishio kwa imani.
Kristo alitukanwa, alikashifiwa, alidhalilishwa (fikiria mpaka kuvuliwa nguo), alitemewa mate, na mwishowe aliuawa. Yesu, akiwa katika mateso makali katika safari yake kuelekea kuuawa, akijua kabisa hawa wanaomtesa, mwishowe watamwua, alisema, "Baba uwasamehe kwa sababu hawajui walitendalo"
Kristo alijifanya mtu, akauvaa ubinadamu, ili atuoneshe tunavyostahili kuenenda. Kuitwa mkristo maana yake ni kufuata maisha ya Kristo. Japo kwa nguvu zetu, hatuwezi, lakini kwa msaada na neema yake, tunaweza kujaribu kuyafuata maisha ya mfano aliyotuachia.
Papa John Paulo II, alishambuliwa kwa risasi na mturuki Mehmet Ali Agka. Akafanyiwa surgery iliyochukua masaa 10, alipopata tu fahamu, kauli yake ya kwanza ilikuwa:
"Kwanza namsamehe aliyetaka kuniua. Nayaunganisha mateso yangu na ya Kristo Bwana wetu. Nawapa pole waliojeruhiwa pamoja nami". Hivyo ndivyo watu wenye imani tunavyostahili kuwa. Lakini siyo jambo rahisi.
Baadaye Rais Sadat wa Misri akamwandikia barua ya wazi Papa akimwomba msamaha Papa. Barua ile ilikuwa na kichwa cha habari, "NAOMBA MSAMAHA KWA KUTAKA KUMWUA PAPA". Maelezo yake ya ndani, Rais Sadat wa Misri akasema kwamba anamwomba msamaha kwa kutaka kumwua Papa kwa sababu Mehmet ni muislam kama yeye, hivyo waislam wamediriki kutaka kumwua Papa. Japo kiuhalisia, Mehmet hakuwa ametumwa na waislam, na wala hakuwahi kutamka kuwa ni imani yake ndiyo iliyompelekea kutaka kumwua Papa. Bali alisema alifanya jambo lile akiamini baada ya kufanya hivyo, Dunia nzima itamfahamu.
Kauli hizi mbili, ya Kristo na ya Papa John Paulo II, itufikirishe sisi tunaoona tulionewa sana wakati wa utawala wa marehemu. Kuna baraka nyingi katika kusamehe kuliko kulipa kisasi.
Katika maovu, uovu mkubwa kabisa ni kumwua mtu. Na mtu akitaka kukuua halafu ukanusurika, kumsamehe mtu huyu, na ikiwezekana ukamfanya kuwa rafiki yako, hakika inahitaji neema ya Mungu. Lakini Kristo aliwasamehe wauaji wake. Hii ndiyo tafsiri ya lile neno lake, 'njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo ya dhambi, nami nitawapumzisha, hata kama dhambi zenu zitakuwa nyekundu kama damu".
Sijaanzisha mada kwaajili ya kumsema marehemu. Na nawaomba wengine pia mkiweza msifanye hivyo, baki kuwakumbusha ndugu zangu kuwa kuna neema na baraka nyingi katika kusamehe kuliko kulipa kisasi.
Mandela alikuwa mtu maarufu sana, na watu wote Duniani walimstaajabia sana, kwa sababu ya kuwasamehe makaburu, watu waliomfanya karibia maisha yake yote amalizie gerezani. Waafrika ndani ya chama chake hawakutegemea. Waliamini baada ya Mandela kuwa Rais ulikuwa muda sahihi kwao kulipiza kisasi. Lakini Mandela aliwaambia,
"Kama ubaguzi wa kaburu dhidi ya mtu mweusi haukuwa mzuri, basi pia ubaguzi wa mtu mweusi dhidi ya mzungu hauwezi kuwa mzuri".
Nami nasema, kama tunaamini marehemu alikuwa na kauli mbaya dhidi yetu, nasi tukiwa na kauki mbaya dhidi yake au wale tunaoamini ni watu waliokuwa wake, tutakuwa na tofauti gani na yeye? Tutakuwa na haki gani ya kudai sisi ni bora kuliko yeye? Kama tunaamini kuwa yeye alikuwa mbaguzi au alikuwa na upendeleo, nasi tukafanya jambo lolote la kuwatenga tunaoamini walikuwa ni watu wake, na sisi si tutakuwa pia ni wabaguzi? Tutakuwa na haki gani ya kusema kuwa marehemu alikuwa mbaguzi?
Kwa upande mwingine, kama kuna ukweli wowote wa jambo lolote tunalojua marehemu alilitenda ambalo halikuwa sawa, basi wale waliokuwa karibu sana na marehemu, japo si lazima, wanaweza kuwaomba msamaha hao walioumizwa sana na marehemu. Lakini hata wasipofanya hivyo, haiwi sababu ya wale walioumizwa sana kutosamehe.
Lisu, familia ya Ben Sanane, Azory, Rugemarila, Mbowe, n.k; kwa neema ya Mungu, siku moja wafike Chato, wakafanye ibada na kutamka kusamehe yote. Na tangu siku hiyo, ikawe mwisho kumnena kwa mabaya marehemu, maana ukishasamehe, unakuwa mwisho wa uadui.