Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

Ndugu yangu umeongea mambo ya msingi sana ambayo baaadhi ya wanajamvi humu hawayaoni kabisa kiasi kwamba nachelea kuwaita great thinkers, kimsingi wanastahili kuitwa mashabiki.

Maisha ya watu wanaokufa kamwe hayawezi kuwa ndio gharama ya madai ya maslahi ya madaktari. Najua serikali yetu ni dhaifu na imeshidwa kuboresha maisha ya watanzania wote (si madaktari pekee) lakini mtindo walioamua kutumia madaktari ni wa kuumiza wananchi ambao wanaodai wanawatetea.

Hata Ulimboka ambaye leo petty thinkers wanamwita shujaa, baada ya kusomeshwa kwa jasho la walalahoi hakukumbuka kuwatumikia hata kidogo badala yake akaenda kwenye shughuli zenye maslahi mazuri kwake.Leo anasema anatetea wananchi, uzalendo huu kaanza lini??Huu hauwezi kuwa ushujaa, huu ni u binafsi tu.

Siungi mkono mgomo wa madaktari wala serikali ya magamba

ukiona watu wa zima na akili zao hawajitambui na wapo kipropaganda zaidi kupindisha ukweli utambue kwamba tunawakati mgumu wa kujikomboa majinga mengi ambayo yanadhani madaktari ndio walioleta hali ya kukosa x-ray katika hospitali zetu za wilaya
CT-scan katika hospitali za rufaa
na vitanda bora vya kujifungulia wazazi katika zahanati zetu ndio wanaokwamisha maendeleo ya nchi kwa vile tuu wamekalia viti vya kuzunguka maofisini
hawa akili zao zimejaa nta lakini japo kwa kuchelewa na kwa kupitia njia ngumu ya akina Ulimboka kumwaga damu bado kuna siku tutafika,Sata kaingia Zambia juzi apa jambo la kwanza anafanya sasa ni kuboresha skta ya afya
Majambazi ya CCM yakiong'olewa fedha zinazokusanywa nina uhakika zitaboresha sekta hii muhimu kwa jamii
 
TWISUKI INGULUVI YE YILIKUCHANYA YITULEKE NI NZANANGIFU MBE SILI (Tunamwomba Mungu wa mbinguni aatusamehe na dhambi zetu zote)
 
Hata Ulimboka anatibiwa nje ya nchi. Zitto umesahau? Mbowe unajuwa kaanza kwenda checkups UK mwaka gani?

Ukiisoma hotuba ya Jakaya Mrisho Kikwete kwa umakini na vizuri, utaelewa kuwa ni haohao madaktari wanaogoma ndio wanatoa vibali vya watu kutibiwa nje. Soma vizuri.

Ni kweli madaktari wanadai mshahara ambao serikali haina uwezo kuulipa. Lakini serikali imeshindwa kuboresha huduma za afya. Leo miaka 50 ya uhuru huduma ni mbovu kuliko ilivyokuwa miaka 50 iliyopita. wakati wa utawala wa Nyerere pamoja na kukataa masharti ya IMF na World bank, serikali iliweza kupeleka dawa za kutosha ktk hospitali na zahanati. Leo ukienda hospitali utaambulia paracetamol tu. Wagonjwa wanalala wawili ktk kitanda kimoja na wengine wanalala chini. uthibitisho wa udhaifu wa serikali kuhusu huduma za afya ni msongamano mkubwa wa watu kuelekea kwa babu wa Loliondo kipindi kifupi kilichopita kupata kikombe. Hali hii inadhihirisha uduni wa huduma ktk hospitali zetu.

Dr Ulimboka anatibiwa nje ya nchi kwa sababu hospitali zetu hazina uwezo wa kumtibu. Zito alipelekwa nje na serikali baada ya kuona Muhimbili hawana uwezo wa kumtibu. Ni nani anayepaswa kuiwezesha Muhimbili iweze kutibu watanzania? ni Zitto au Mbowe?


Ni vizuri serikali ikatambua udhaifu wake ili iweze kusonga mbele.
 
Kwa maneno uake Dr ULIMBOKA ametoa kauli ya kishujaa na kutia shime na hamasa katika mapambano yanayoendelea ya kudai haki katika kuboresha huduma za afya na maslahi ya madaktari

"Naelekea nje ya nchi kwa matibabu, nawasihi madaktari wenzangu wanaobaki waendelee ma mapambano ya kudai haki ambayo kimsingi bado haijapatikana, nawaomba damu yangu iliyomwagika ikawe chachu na hamasa katika harakati hizi za kudai haki, asanteni sana"

Source: ITV HABARI
WAHENGA Waliwahi kunena kuwa inapoishia haki ya mtu mmoja ndipo panapoanzia haki ya mtu mwingine: Kwa hiyo si busara wala ubinaadamu kuacha binaadamu wanadhulumiwa haki ya msingi ya Kuishi, kwa kisingizio kuwa wapo katika mgomo wa kudai haki ya kuongezewa vijisenti na posho...SHAME ON YOU STRIKING INTERNS AND 'DOCTORS'. Najua hili jambo kwa kuwa limeanza lazima litaisha na taathira yake ni pamoja umma kupoteza imani yao ya muda mrefu waliyokuwa nayo kwa madaktari...kwani sasa wananchi wanawaona ni wanaharakati na si watumishi wa umma, na itawagharimu sana kujipangusa.
 
attachment.php

describe this face
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom