Dr Slaa hajui kutofautisha mvao wa kichama na wa shughuli za kitaifa?

Ukichunguza vizuri utagundua hilo gwanda la Slaa limechanika kwenye upande wa chini wa kulia. Hii ni aibu kubwa sana kwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania. Tujitahidi kuwa smart si kwa maneno tu bali hata mavazi. Sasa huyo mzungu atamchukulia vipi Slaa?
 
Mbona askari polisi wanakuwa na sare hata wakienda kutibiwa dispensary?
 
Ukichunguza vizuri utagundua hilo gwanda la Slaa limechanika kwenye upande wa chini wa kulia. Hii ni aibu kubwa sana kwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania. Tujitahidi kuwa smart si kwa maneno tu bali hata mavazi. Sasa huyo mzungu atamchukulia vipi Slaa?

Haaaaaaaaaaaaaaa,i like that.Bora atumie mda mwingi kulisha Roho na akili kuliko mwili usio na shkrani.
 
Mtoa mada amefikiri kutosha na kuona mbali zaidi ya wengi wanaochangia hoja hapa. Doctor ni taaluma yake lakini itakuwa kichekesho unapomwona anaingia na pima joto shingoni wakati yuko bar kunywa pombe. Mcheza mpira atawashangaza watu akiingia msikitini au kanisani na sare za mpira.

Sare ni utambulisho na pia sare inaweza kusababisha kujenga hisia fulani watu wawapo katika tuko lenye lengo moja la kujenga utaifa, kwani kila kitu kina nafasi na mahali pake.

Sitakuwa vuvuzela au kuishi kwa mtindo ambao wengi hapa wanadhani kuwa great thinker ni kushabikia, ila mwono wangu ni wenye manufaa ya kitaifa au umoja wa kitaifa na wa kujenga taifa letu. Kuna nafasi ya kuvaa mavazi ya shughuli za kichama na tuwapo katika majukumu ya kitaifa tunatakiwa kuwa na mvao usioleta tofauti za kiitikadi, maana yake itikadi za chama si vita ya vyama vya siasa, bali ni itikadi za ushindani wa kuleta na kujenga maendeleo kwa taifa letu.

Mara kadhaa tumelalamikia Kikwete kufanya vikao vya Chama kule Ikulu. Tumelalamika kutotumia vyombo vya umma kwa shughuli za chama, na mara kadhaa tumelalamikia mbunge, mawaziri au raisi kuwa na mwonekano wa kichama akiwa katika shughuli za kitaifa. Kwa CCM tunaona vibaya hivyo, kwa Chadema ruksa kuvaa uchadema po pote hata kwenye shughuli za kitaifa, hii ni kasoro kubwa kwa mwenye kufikiri kipana zaidi. Hapa kuna upungufu, na mimi si mtu wa aina hiyo.

Kukubali hilo si ukomavu wa kisiasa, ni mapungufu ambayo yanatakiwa kufanyia kazi. Na kwa kutetea utaifa sitetereki, viongozi licha ya uzalendo tunahitaji mshikamano katika masuala ya kitaifa badala ya kuonyesha matabaka tuwapo katika nafasi hizo. Naongea na kutetea hilo kwa uzoefu wangu, imani yangu kwa tifa langu, na moyo wangu wa kizalendo.

Utetezi wa wengi hapa hauonyeshi ukomavu katika mambo ya kisiasa, bali ni kama shabiki wa mpira uwanjani kama refa anakataa goli lililofungwa kimakosa wako tayari hata kumpiga kwa sababu ya ushabiki na wala si kwa haki. Sikubali utumwa wa kifikra wa aina hiyo. Na hata nikimwona ana kwa ana nitamtamkia hilo awe na utambuzi na uelewa wa wapi kuwa na sare za chama na nafasi ya mvao wa kawaida katika shughuli za kitaifa.
 
Ukichunguza vizuri utagundua hilo gwanda la Slaa limechanika kwenye upande wa chini wa kulia. Hii ni aibu kubwa sana kwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania. Tujitahidi kuwa smart si kwa maneno tu bali hata mavazi. Sasa huyo mzungu atamchukulia vipi Slaa?

kipaumbele katika imani yako ni wazungu?
 
Hali ya kifedha ya Slaa kwa sasa si nzuri kuweza kununua suti.
Hii imetokana na kubanwa na TRA kurejesha pesa ya kodi aliyokuwa akikwepa kulipa kwenye posho zake.
Kwa sasa posho inakatwa kodi, familia imeongezeka, hivyo haitatosha kununua suti.
Magwanda ndo kimbilio ili kumlinda katika uvaaji.

simple mind like you will always discuss of people!
Ndio maana kukawa na jukwaa la udaku!
 
This picture tells a lot about Slaa's apparent miserable life. Look carefully at his noticeable apathetic phizz and compare it to Makinda's cheerful countenance.
 
Kaka ni kweli, yaani kuna watu unapogusa hoja ya cdm tu, hata kama ina ukweli lazima wakuandame kwa mawe ya maneno. Ila wakubali wasikubali huo ndo ukweli wenyewe. Na sasa kaka kuna mpango nimeudaka toka bavicha kwamba mbowe anampango wa kumfanya mbaya dr slaa kutokana na slaa kuanzisha kampeni ya chinichini kwa wanachama wa cdm hasa kwa viongozi wa mikoa, kumshitaki mbowe kwa kitendo cha kwenda ikulu kufanya mazungumzo na jk tofauti na itikadi ya chama. Katika mpango huo amewatumia baadhi ya vijana wa bavicha ambao anawaamini.
 
huwez kumpangia mtu mavazi ya kuvaa.
Hayo aliyovaa kwenye picha wapi yameandikwa CDM?

Mara ngap Jk anavaa nguo za kijani na hamna anaesema kuwa anakosea?

Je kati ya wanabodi walio kuwepo,dr alizungumzia mambo ya cdm?hiyo ndo hoja ya msingi na si mavazi yake.
 
Kwa nini wengine wanapovaa ya CCM kwenye nafasi za mambo ya kitaifa tunalalamikia, lakini Chadema ni ruksa? Angalia pande zote za sarafu, si upande mmoja tu
 
Kwani shughuli za Chama si za Umma?

IMG_7637.JPG

Shughuli za chama zawahusu wanachama na shughuli za kitaifa zinawahusu wananchi wote bila tofauti za kiitikadi.
 
This picture tells a lot about Slaa's apparent miserable life. Look carefully at his noticeable apathetic phizz and compare it to Makinda's cheerful countenance.

Hapo panaongelewa serious issues watu wako serious kikazi lakini spika makinda anacheka cheka tu kama raisi wake, inawezekana magamba wanaugonjwa wa akili haiwezekani kuchekacheka tu hata pale pasipostahili. Anyway mtu ukilala maskini halafu unaamka billionea kwa pesa za ufisadi hakiya nani unaweza usichekecheke tu kama changu doa!!!!
 
Kwa nini wengine wanapovaa ya CCM kwenye nafasi za mambo ya kitaifa tunalalamikia, lakini Chadema ni ruksa? Angalia pande zote za sarafu, si upande mmoja tu

We mang'ati uwe mwelewa.

Content ya maneno yake yanatofauti na mavazi,kama alisifia mavazi aliyovaa sawa, mada yako haina mashiko humu.
 
Dr. Slaa anatakiwa kutofautisha akiwa katika harakati za kichama na shughuli za umma. Si kila anakokwenda ni magwanda tu, siku akiingia ikulu itakuwa ni ikulu nzima full sare za magwanda. Kwa vyo vyote viongozi wetu watofautishe nafasi za kuvaa sare za chama na nafasi ambazo za umoja wa kitaifa ambapo nguo za kwaida zinavaliwa ili mwingine asisikie vibaya kuchangamana kwa kufikiria kiitikadi.

Ulimanisha umoja wa kitaifa upi!? Maana mambo ya 'umoja' nayasikia katika serikali ya Mapinduzi ya Tanzania Zanzibar.
 
Dr. Slaa anatakiwa kutofautisha akiwa katika harakati za kichama na shughuli za umma. Si kila anakokwenda ni magwanda tu, siku akiingia ikulu itakuwa ni ikulu nzima full sare za magwanda. Kwa vyo vyote viongozi wetu watofautishe nafasi za kuvaa sare za chama na nafasi ambazo za umoja wa kitaifa ambapo nguo za kwaida zinavaliwa ili mwingine asisikie vibaya kuchangamana kwa kufikiria kiitikadi.

Pointi yako nimeikubali hapo nilipo highlight japo kwa bahati mbaya great thinkers wengi humu hawakubaliani na wewe lakini usikate tamaa hata Galileo aliposema kuwa dunia ni mviringo kwa mara ya kwanza aliishia lupango.

Tunatakiwa kudumisha umoja wa kitaifa hata kwa mavazi pia, ni bora mavazi yaendane na shughuli iliyolengwa. Hili lisiishie kwa wanasiasa tu bali liwe jukumu la kila mwanajamii hivyo wale watanzania wenzetu wanaovaa hijab, vibarakashehe, buibui au kanzu kwenye mashule ya serkali, bungeni na maofisi ya serikalini wanapaswa kutambua jinsi wanavyoathiri hisia za wanajamii wengine na inabidi waache tabia hiyo hasi kwa jamii mara moja.
 
Back
Top Bottom