Dr Slaa hajui kutofautisha mvao wa kichama na wa shughuli za kitaifa?

Matatizo ya Slaa na washamba wenzake yapo wazi sana. Haya ni matokeo ya kuzaliwa vijijini na kuja mjini ukubwani. Mtu kama Halima Mdee hawezi kufanya ushamba kama huo hata siku moja.
Ukiona mtu anajiita kazaliwa mjini ujue ana matatizo makubwa ya ushamba! Miji yenyewe hii michafu na foleni unajiona mjanja?
 
Ukiona mtu anajiita kazaliwa mjini ujue ana matatizo makubwa ya ushamba! Miji yenyewe hii michafu na foleni unajiona mjanja?

Miji ni michafu lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu aliyezaliwa Ocean Road na yule aliyezaliwa zahanati ya Ogeronjo kama Slaa. Mimi mwenyewe naweza kumwingiza mjini huyu mzee. Hana ujanja kabisa kwangu.
 
Kwa hiyo waliozaliwa hapo Ocean Road Hospital,Aga Khan na Muhimbili ni wajanja kuliko hao waliozaliwa vijijini?! Mawazo ya kitoto kabisa haya.
 
Hakuna vazi la taifa mpaka sasa. Mi naona kuvaa imported clothes sio sawa. Ni bora kuvaa nguo iliyotengenezwa na mafundi wetu wandani japo kipato watakachopata ni kidogo lakini ni nafuu kuliko kutopata kabisa.
 
Matatizo ya Slaa na washamba wenzake yapo wazi sana. Haya ni matokeo ya kuzaliwa vijijini na kuja mjini ukubwani. Mtu kama Halima Mdee hawezi kufanya ushamba kama huo hata siku moja.

Mwita25 this is absard weka heshima kidogo .JK wenu na wapuuzi wenzake wako mjini siku nyingi wamesaidia nini ? Kuja mjini kitambo kumelisaidia nini Taifa na wanyonge masikini ?Kila siku tunaona kwenye sherehe ama mikutano ya kiserikali mapambo yote ni rangi za CCM mbona hamjapiga kelele wakati ni pesa ya umma inatumika pale na hao akina JK wako mjini siku nyingi ?

Mind your language tafadhali .
 
Miji ni michafu lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu aliyezaliwa Ocean Road na yule aliyezaliwa zahanati ya Ogeronjo kama Slaa. Mimi mwenyewe naweza kumwingiza mjini huyu mzee. Hana ujanja kabisa kwangu.

We kalumbu utamwingiza nani mjini?

Kwanza dodoma ndo mjini?
We mang'ati kweli.
 
Nafikiri mtoa mada yuko sahihi. Ni vizuri viongozi wa CDM wakawa tofauti na ccm. Huwa naudhika kuwaona viongozi wa CCM wakivaa nguo za kijani kwenye shughuli za serikali na dhifa za kitaifa. Hivo kama inavokuwa mbaya upande wa ccm na cdm nao iwe hivohivo. Wajirekebishe.
 
Naomba mnijuze hv ukivaa gwanda la khaki tayari uko CDM mi nafahamu zile rangi za CDM Nyekundu ,Blue bahari,na ile Nyeusi. Hayo magwanda nilidhani ni vazi tu kama ambavyo kuna magwanda ya kijani, nyeusi nk
 
Sare ni utambulisho na pia sare inaweza kusababisha kujenga hisia fulani watu wawapo katika tuko lenye lengo moja la kujenga utaifa, kwani kila kitu kina nafasi na mahali pake.

Na hata nikimwona ana kwa ana nitamtamkia hilo awe na utambuzi na uelewa wa wapi kuwa na sare za chama na nafasi ya mvao wa kawaida katika shughuli za kitaifa.

Mkuu hilo si vazi la chama!! Ni aina ya vazi ambalo wanamapinduzi/wanaharakati uvaa kuonyesha jinsi walivyo rebellious na mfumo kandamizi na nyonyaji wa chama/kikundi/serikali iliyoshika hatamu. Ajabu, hata CCM nao uvaa vazi kama hili (la rangi ya kijani)--mfano, UVCCM vazi lao nalo linafanana na hili.

Pia mavazi kama haya uvaliwa na wafanyakazi/watumishi/watafiti/wasafiri katika nyanja ya viumbepori (misitu na wanyamapori). Mfano, wafanyakazi wa TANAPA vazi kama hilo ndio sare yao ya kazini.

Kwa hiyo mkuu, hilo si vazi rasmi la chama; ila watu hawaelewi na kufikiria kama ulivyofikiria wewe kwavile wanaCHADEMA wengi uvalia vazi hilo.
 
Matatizo ya Slaa na washamba wenzake yapo wazi sana. Haya ni matokeo ya kuzaliwa vijijini na kuja mjini ukubwani. Mtu kama Halima Mdee hawezi kufanya ushamba kama huo hata siku moja.

hivi Mwita umezaliwa wapi
 
Jamani kuuliza sii Ujinga.. hili ndio vazi la kitaifa ama nao ni magwada rangi tofauti tu...

cdm+%252828%2529.JPG

a1o1ua.jpg
hamad_rashid-564x272.jpg
 
kwani shughuli za chama si za umma?

acheni unafiki mbona ccm wakivaa yale manguo yao ya kijana kwenye shughuli za kitaifa huwa tunawachamba hapa?hivi leo tukimuona jakaya kavaa yale manguo yao halafu anatembelea muhimbili pengine akiwa na obama tutamnyamazia hapa....mapenzi yakizidi mpaka unakua ujinga!
 
CCBRT nayo ni shughuli ya kitaifa? au kwa kuwa umemuona spika? hujui kwamba anaondoka kwnye orodha ya wazalendo kwa kujali kundi moja na kuacha makundi mengi? any way tafuta kwanza maana ya shughuli ya KITAIFA.......Taarifa, Dr Slaa ndiye master mind wa CCBRT maana ndiye aliayandika proposal ya awali kabisa...aaheshimika sana kuliko AM,njo vile wakampa hata uwenyekiti wa BODI..
 
Tatizo ninaloliona katika mada hii wengi wetu ni mashabiki badala ya kujadili maudhui ya mada iliyoletwa. Inaonekana wengi wetu hawafahamu au kupambanua mahali na nafasi ya shughuli za umma na shughuli za kichama.

Chama ni jumuia au kikundi cha watu chenye kufuata itikadi na malengo waliyojiwekea ili kujenga umoja wa kufanikisha azima yao. Iwe katika siasa, social, kazi, nk. Kwa hoja hiyo itashtua na kushangaza watu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni kutoka chama cha CCM akijaa ikulu na sare za chama chake, au akiwa katika majukumu yake kama rais awe katika sare za chama chake.

Kwa vyo vyote inavyoonjeka kwa upande wa viongozi wa serikali kutoonyesha uchama katika shughuli za kiserikali na kitaifa, vivyo hivyo hata vyama vya upinzania ambavyo havijashika dola bado viongozi wake wawapo katika majukumu au matukio ya shughuli za kitaifa ambazo zinajumuisha watu wote bila kujali itikadi za kichama wanatakiwa kuweka kando mvao unaotambuliwa na chama chao na badala yake wavae mavazi ya kawaida.

Mkuki kwa nguruwe okay, lakini kwa binadamu ni machungu. Ushabiki wa aina hiyo siko tayari kuuruhusu katika dhamiri yangu safi kwa nchi yangu. Kesho hawa hawa Chadema wataweza fanya mambo ambayo hayakubaliki kama wafanyavyo CCM maana yake tutaendelea kushabikia tu kama watu tusio na akili timamu? Huu ni utoto maana yake hakuna ukomavu wa kifikra na kiupembuzi. Hata mpinge kwa nguvu zote jambo hilo halikubaliki, na kwa imani yangu Dr. Slaa kama amesoma mada hii amenielewa.

Hata hivyo naheshimu mawazo na mchango wa kila mmoja maana akili ni nywele na kila mmoja ana zake, hivyo pamoja na kutoa mada hii sikuwa na maana kwamba wote watakubaliana, kwani wengine wanahitaji muda kuelewa, na ipo siku wataelewa niongeleayo.
 
CCBRT nayo ni shughuli ya kitaifa? au kwa kuwa umemuona spika? hujui kwamba anaondoka kwnye orodha ya wazalendo kwa kujali kundi moja na kuacha makundi mengi? any way tafuta kwanza maana ya shughuli ya KITAIFA.......Taarifa, Dr Slaa ndiye master mind wa CCBRT maana ndiye aliayandika proposal ya awali kabisa...aaheshimika sana kuliko AM,njo vile wakampa hata uwenyekiti wa BODI..

Mzee umesoma vizuri kichwa cha thread lakini?!mbona unachanganya apples ana oranges!soma vizuri alichoandika mleta thread
 
kumbe watu siku hizi hamwezi kutofautisha kaunda suti na gwanda? Au kwa vile rangi ya kaki? Hiyo suti bwana, tena ya kizalendo
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom