Mtaala wa Elimu ya Taifa unairuhusu TAMISEMI ngazi ya Mkoa kuratibu na kusimamia shughuli za Shule ikiwemo ratiba za masomo

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Habari Wanabodi!

Ukisoma Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ukurasa wa 5 kuhusu Utekelezaji wa Ibara ya 146(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inayohusu ugatuaji. Katiba inatamka katika Sura ya Nane (kuhusu madaraka kwa umma), kwamba, madhumuni ya kuwapo Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi na hivyo kuwezesha Serikali za Mitaa kuwajibika kutekeleza kazi zake katika eneo husika.

Sheria za Serikali za Mitaa zinatoa majukumu kwa Halmashauri kuhusu elimu katika Kifungu cha 55 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Miji) ya 1982. Ni kwa mantiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Matangazo ya Serikali Na. 494 na 494A ya mwaka 2010 aligatua na kuiweka katika usimamiaji wa iliyokuwa OWM-TAMISEMI na sasa OR-TAMISEMI elimu ya awali, msingi na sekondari na kuacha iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushughulikia Sera katika masuala yote ya elimu na mafunzo.

Nimesoma pia hotuba mojawapo ya Mheshimiwa Simbachawene akiwa waziri wa TAMISEMI kuhusu majukumu ya TAMISEMI, kuna kipande namnukuu akiainisha majukumu ya TAMISEMI kitaifa na katika ngazi ya Mkoa:

TAMISEMI inatekeleza majukumu yafuatayo:
i)Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Ugatuaji Madaraka (D byD), Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikaliza Mitaa, Maendeleo Mijini na Vijijini;
ii)Kuziwezesha Tawala za Mikoa kutekeleza majukumu yake ya kisheria;
iii)Kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yake ya kisheria;
iv)Kuratibu shughuli za utoaji wa huduma mijini kama vile usafiri na usafirishaji, upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira;
v)Kusimamia shughuli za Tume ya Utumishi wa Walimu;
vi)Kusimamia shughuli za Elimu ya Msingi na Sekondari;
vii)Kujenga uwezo wa watumishi wa OR –TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi; na
viii)Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programuna Miradi iliyopo chini ya OR-TAMISEMI.

Mheshimiwa Spika,majukumu yanayotekelezwa na Mikoa ni kama ifuatavyo:
i)Kuhakikisha kunakuwepo amani, usalama na utulivu katika Mikoa na Wilaya;
ii)Kusimamia na kuratibu shughuli zote za maendeleo katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
iii)Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa ili zitekeleze majukumu yake kwa ufanisi;
iv)Kufuatilia utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali zinazotekelezwa na Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maeneo yake;
v)Kuratibu usimamizi na uendeshaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
vi)Kusimamia uendeshaji wa Afya ya Msingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
vii)Kuhakikisha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi utawala.

Tukija hapo kwenye Uratibum Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu sote tunafahamu kuwa kuwa kwa kiasi kikubwa Sera ya Elimu ni sera ya Taifa na Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia ndo yenye kuratIbu sera hii . Pia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndo inayoandaa mtaala wa Elimu kitaifa. Tunapaswa kukumbuka jambo moja kuwa ukisoma muhtasari wa Taasisi ya Elimu Tanzania. (2015). Mtaala wa Elimu ya Msingi Darasa la I–VII. Dar es Salaam: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia tunaona kuwa mtaala umetoa muongozo wa Idadi ya masomo pamoja na ya hiari .

Lakini pia umetoa muda ambao mwanafunzi anapaswa kufundishwa darasani. Pia huu Mtaala umeruhusu kuwa na shughuli za ziada mbazo zinaweza kupangwa hata na shule husika au mamlaka ya utekelezaji. Mfano wa shughuli hizo ni kama Michezo, Masomo kwa ajili ya kujijengea uwezo, sanaa, klabu za masomo, n.k . Haya masuala Mtaala haujayaweka bayana wala muda wake haujalaimishiwa kufuatwa bali kuna makadirio ya "At least" na hayana kuanzia muda gani mpaka muda gani. Hapa imetolewa idadi ya masaa kwa siku.

Kiuhalisia Muongozo ni Blueprint au Platform ya kufanyia jambo na huwa haijaweka masharti rasmi katika kutekeleza jambo bali umeweka vipengele muhimu tu vya kufuatwa. Hapa ndo kwenye shida, pale ninapokua muongozo na unaeleweka halafu umshauratibu then mimi nakuja na kukupangia namna ya uratibu ni lazima tutaona tatizo la ugatuaji madaraka.

Nanukuu ukurasa wa 49
"11.3 Shughuli za ziada katika MtaalaShughuli za ziada katika Mtaala zitafanyika kwa lengo la kuimarisha maarifa na stadi ambazo mwanafunzi amejifunza ndani ya darasa. Hii itamwezesha mwanafunzi kuchangamana na wanafunzi wengine pamoja na mazingira ya nje ya darasa. Muktadha huu huimarisha ujenzi wa maana kwa yale anayojifunza. Shughuli hizo zitajumuisha klabu za masomo na maeneo mengine ya kujifunza. Vilevile zitakuwepo shughuli za michezo, uzalishaji mali, utamaduni, malezi na unasihi. Shughuli hizi zitawezesha wanafunzi kujifunza kwa kina. Ufuatao ni ufafanuzi wa shughuli za ziada katika Mtaala:

a) Klabu za masomo
Klabu hizi zinahusisha masomo mbalimbali na klabu za masuala mtambuka. Hizi ni kama klabu ya mazingira, VVU na UKIMWI, jinsia na haki za mtoto. Nyingine ni kama klabu ya stadi za maisha, kupinga/kudhibiti rushwa, afya, uelimishaji rika, biashara na usalama barabarani.

b) Michezo na sanaa
Wanafunzi watahimizwa kucheza michezo mbalimbali ili kuibua vipaji na vipawa ambavyo vitapaswa kuendelezwa. Michezo itafanyika kwa wanafunzi wote kufuatana na ratiba itakayopangwa na shule husika. Michezo hiyo ni pamoja na: uigizaji, uimbaji na riadha. Mingine ni kama mpira wa miguu, pete, mikono, kikapu, wavu, meza, mchezo wa bao. Umahiri katika shughuli za michezo umegawanywa kimadarasa kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 20. - (Wale wa UMISETA na UMITASHUMTA, Mashairi, Ngonjera, Maigizo,n.k tunayajua haya na mpaka leo hii bado timu za shule zinafanya. Kuna wakati mnaweka kambi kabisa kwa ajili ya mashindano ya Volleyball tu)

c) Uzalishaji mali

Wanafunzi watafanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali shuleni. Madhumuni yake ni kuongeza kipato na kukuza stadi zao za ujasiriamali. Shughuli hizo ni kama kuendesha duka la shule na kulima bustani za mboga na maua. - (Nakumbuka enzi zetu tuliosoma Tosamaganga Tulikuwa tunakwenda kulima jioni na siku za wikiendi )

d) BurudaniBurudani ni shughuli anazofanya mtoto kujiburudisha mwili na akili awapo shuleni. Shughuli anuai zikiwamo ziara na matamasha zitafanyika mara moja kwa muhula. Kila shule itaainisha na kupanga shughuli za burudani zitakazoshirikisha wanafunzi wote wakiwemo wenye mahitaji maalumu. Hii itakuza usawa na ushirikiano miongoni mwa wanafunzi. Tuzo zitatolewa kwa wanafunzi watakaofanya vizuri ili kuwamotisha kuendeleza vipaji vyao. "

Analysis:
Tukilitazama hili katika SERA na Mtaala wa elimu, tunaona kabisa kuwa muda wa chini waliowekewa wanafunzi wa kufundishwa darasani ni masaa 6 kwa darasa la 3-7. Lakini pia mtaala umetoa nafasi ya shughuli zingine zinazoweza kufanyika na zinaitwa "Extra-Curricular Activities" , katika kutekeleza hizi shughuli Mtaala haujatoa kanuni au maelekezo maalum bali ni jukumu la shule kuratibu. Linapokuja jukumu la shule kuratibu maana yake tunaiongelea mamlaka ya uratibu kama OR TAMISEMI ngazi ya mkoa/Ofisi ya Mkuu wa Mkoa au Ngazi ya Wilaya kata au Shule husika . kama alivyosema Mh. Simbachawene. Nawakumbusha pia hata hizo tunazoziita Tuitions ni Extracurricular sababu hazipo ndani ya mtaala na hata muundo wake wa ufundishaji unaweza kuwa kinyume na mtaala.

Swali Fikirishi: Mwishoni najiuliza swali Je vipi kuhusu Makambi ya kuendeleza wanafunzi wanaoelekea kufanya mitihani yakiwa kama yameratibiwa na OR TAMISEMI katika mkoa au wilaya fulani.
 
Back
Top Bottom