Hatimaye katibu mkuu wa chadema dr slaa amemteua rasmi mbunge wa jimbo la ubungo JOHN MNYIKA kuwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA taifa na kumshusha ndg ERASTO TUMBO KUWA afisa ndani ya kurugenzi source TBC TAARIFA
Utakuwa ni uteuzi mzuri na makini kwani kurugenzi yetu ya habari na uenezi haikuwa active kiasi kinachotakiwa.
Ili afanye kazi zake vizuri zaidi na kwa uhakika inabidi wampunguzie majukumu ya ukurugenzi wa mambo ya nje.
Na kuanzia sasa wale watunga propaganda dhidi ya chadema wamepata kiboko yao, JJ amekuja kuwashika!
Chadema sasa mnachosha.... kwa nini mnawalimbikiza wabunge kazi zaidi wakati walizonazo tayari ni mzigo kwa chama?.. Vijana wengine wapo kwa nini hawatumiwi hawa!..Sipingi swala la Mnyika kuteuliwa nafasi hii, bali nadhani wapo vijana wengi sana wenye uwezo ari na wamejikita ktk media wanaweza kuifanya kazi hii kila siku masaa 16 kwa malipo madogo sana kuliko kumshindilia mtu mmoja majukumu kibao.. Mtamzeesha huyu dogo kabla ya wakati wake.
Swali langu ktk uteuzi huu, Je, Hawa viongozi wa chama na ni wabunge pia hawapokei mishahara miwili kwa kutoa huduma hizi?.. mathlan Mnyika leo hii pato lake haliongezeki kwa kupewa jukumu hili zaidi maana twende mbele turidu nyuma. Kupinga posho kepee haitoshi ikiwa chama kinawapa madaraka kundi la watu wale wale tu hii inaashiria zaidi kwetu kama ni ULAJI..
- Mtanisamehe nawakilisha mawazzo yangu.