Dr. Slaa amteua Mnyika kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.

USTAADHI

JF-Expert Member
May 10, 2011
1,516
136
Hatimaye katibu mkuu wa chadema dr slaa amemteua rasmi mbunge wa jimbo la ubungo JOHN MNYIKA kuwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA taifa na kumshusha ndg ERASTO TUMBO KUWA afisa ndani ya kurugenzi source TBC TAARIFA
 
Hakunaga kama Dr. wa ukweli....JJM your the best!! We are proud of You.....
 
Hakuna malalamiko hapo. nadhani wale magamba waliokuwa wanasema eti Zitto kawekwa pembeni nadhani watakuwa wameelewa sasa kuwa CDM haifanyi kazi kwa majungu
 
Safi sana Dr wa ukweli, hiki kilio kilikuwa cha muda mrefu cha kumuondoa Tumbo na kuliweka jembe lingine.
Vipi ukurugenzi wa mambo ya nje hawajasema kapewa nani au mnyika atashika zote mbili?
 
Sasa tunategemea kuona Infomation flow inayoeleweka. Napendekeza pia akishakalia kiti atupatie mpango mkakati wa jinsi ya kuwafikia watanzania kupitia vyombo vya habari vya CHADEMA.
 
Hatimaye katibu mkuu wa chadema dr slaa amemteua rasmi mbunge wa jimbo la ubungo JOHN MNYIKA kuwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA taifa na kumshusha ndg ERASTO TUMBO KUWA afisa ndani ya kurugenzi source TBC TAARIFA

Utakuwa ni uteuzi mzuri na makini kwani kurugenzi yetu ya habari na uenezi haikuwa active kiasi kinachotakiwa.

Ili afanye kazi zake vizuri zaidi na kwa uhakika inabidi wampunguzie majukumu ya ukurugenzi wa mambo ya nje.

Na kuanzia sasa wale watunga propaganda dhidi ya chadema wamepata kiboko yao, JJ amekuja kuwashika!
 
Chadema sasa mnachosha.... kwa nini mnawalimbikiza wabunge kazi zaidi wakati walizonazo tayari ni mzigo kwa chama?.. Vijana wengine wapo kwa nini hawatumiwi hawa!..Sipingi swala la Mnyika kuteuliwa nafasi hii, bali nadhani wapo vijana wengi sana wenye uwezo ari na wamejikita ktk media wanaweza kuifanya kazi hii kila siku masaa 16 kwa malipo madogo sana kuliko kumshindilia mtu mmoja majukumu kibao.. Mtamzeesha huyu dogo kabla ya wakati wake.

Swali langu ktk uteuzi huu, Je, Hawa viongozi wa chama na ni wabunge pia hawapokei mishahara miwili kwa kutoa huduma hizi?.. mathlan Mnyika leo hii pato lake haliongezeki kwa kupewa jukumu hili zaidi maana twende mbele turudi nyuma. Kupinga posho pekee haitoshi ikiwa chama kinawapa madaraka kundi la watu wale wale tu hii inaashiria zaidi kwetu kama ni ULAJI zaidi kwao..
- Mtanisamehe nawakilisha mawazzo yangu.
 
Kati ya vichwa ninavyovikubal CDM Mnyika ni mmojawapo,hayo ni maandalizi ya 2015
 
Mnyika,

Binafsi napenda kukupongeza kwa jukumu hili jipya na gumu kwako. Kwa muda sasa umekuwa mtendaji mzuri, mwadilifu na mkweli katika wadhifa wako kabla ya hapo.

Ninachopenda kukuasa ni kuwa karibu zaidi na mawazo ya wananchi, wanachama na makada katika kujenga chama chetu. Nina matumaini sana na wewd na ni imani yangu kwamba utakiinua chama chetu juu zaidi. Katika utendaji kazi wako utakutana na hoja nyingi chafu, zenye lengo la kukupotezea muda na heshima yako, daima simama imara na kuwa muwazi ukikwepa kwa hali na mali kutumika kama mpotoshaji mkuu na mpindishaji wa malengo na sera za chama.

Katika kipindi hiki mijadala ni mingi mno itaibuliwa mingine ikiwa na lengo la kukukwamisha wewe binafsi na chama, nakusihi songa mbele na daima toa kauli sahihi ili kuepuka malumbano yasiyo lazima ya ndani ya chama.

Utakutana na makundi na mitazamo tofauti, yenye kulenga maslahi binafsi hasa itakayoishia kukishushia chama, nakuomba usiwe mwepesi wa kujibj kila jambo litakaloelekezwa chadema, hii itakuwa busara kuu na iliyotukuka kwako na kwa uongozi uliokukasimu wadhifa huo.

Chama kwetu sisk makada, kitakusikiliza kama msemaji mkuu na mjuvi wa kila jambo na kwa hakika wewe sasa u daraja baina yetu na chama.

Mungu akusaidie, mungu anisaidie na mungu awasaidie watanzania wote wapenda mabadiliko popote walipo.

Ni mimi,
Pangu Pakavu
Nakusalimia.

Utakuwa ni uteuzi mzuri na makini kwani kurugenzi yetu ya habari na uenezi haikuwa active kiasi kinachotakiwa.

Ili afanye kazi zake vizuri zaidi na kwa uhakika inabidi wampunguzie majukumu ya ukurugenzi wa mambo ya nje.

Na kuanzia sasa wale watunga propaganda dhidi ya chadema wamepata kiboko yao, JJ amekuja kuwashika!
 
Chadema sasa mnachosha.... kwa nini mnawalimbikiza wabunge kazi zaidi wakati walizonazo tayari ni mzigo kwa chama?.. Vijana wengine wapo kwa nini hawatumiwi hawa!..Sipingi swala la Mnyika kuteuliwa nafasi hii, bali nadhani wapo vijana wengi sana wenye uwezo ari na wamejikita ktk media wanaweza kuifanya kazi hii kila siku masaa 16 kwa malipo madogo sana kuliko kumshindilia mtu mmoja majukumu kibao.. Mtamzeesha huyu dogo kabla ya wakati wake.

Swali langu ktk uteuzi huu, Je, Hawa viongozi wa chama na ni wabunge pia hawapokei mishahara miwili kwa kutoa huduma hizi?.. mathlan Mnyika leo hii pato lake haliongezeki kwa kupewa jukumu hili zaidi maana twende mbele turidu nyuma. Kupinga posho kepee haitoshi ikiwa chama kinawapa madaraka kundi la watu wale wale tu hii inaashiria zaidi kwetu kama ni ULAJI..
- Mtanisamehe nawakilisha mawazzo yangu.

Kimsingi mawazo yako ni mazuri sana.Lakini kwa jinsi tunavvyomfahamu Mnyika ni kijana mtulivu,damu inachemka na anaupeo wa hali ya juu kwa siasa za nchi hii.Kwa mahali ambapo chama chao kimefikia kinahitaji mtu kama yeye kwa hiyo nafasi.Naamini atamudu kubeba majukumu yote mawili bila matatizo.Na kuhusu hoja ya ULAJI binafsi sina jibu.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom