Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Mwakyembe Harrison, amemruhusu Hosea na watu wake watangulie mahakamani, kua amechukua posho za vikao mara mbili, sasa sioni kwanini mpaka muda huu Hosea hajaenda mahakamani.
Watu tunamwomba Hosea atoe majibu ya vitu vya maana, hasa Kagoda , Meremeta , ndege za jeshi, anakuja na upuuzi huu wa posho za vikao, mbona wao walimlipa Mwakyembe posho ya kujikimu kama yuko mkoani.
Hosea anacheza mchezo wa Siasa wakati yeye yuko kwenye payroll ya watuymishi wa UMMA pale hazina, ni pensionable huyu.
akachukue fomu agombee Ubunge
 
Mwakyembe knows what is doing.....! safi sana

Akili nyingi uondoa maarifa. Mwakyembe has goofed big time on this. Yeye kama kiongozi hasingeweka hadharani kwamba ameitwa na chombo halali cha dola kuhojiwa na amekataa. Mwakeyembe anajua hayuko juu ya sheria. Kwa nini ahofie kuojiwa in the first place. Hata kama anaona ni upuuzi angekwenda and he should have told PCCB point blank that all this is bull crap! Lakini kugoma kuhojiwa na kuweka hadharani sio jambo la kujivunia hata kidogo. Anaonyesha mfano gani? Nadhani jeri yake imepanda sana kichwani mwake and this could be his Achilles' heel. Poor Mwakyembe!
 
Hivi hii TAKUKURU ni chombo cha Serikali au ni chombo cha chama au cha serikali, kwani vitu wanayo fanya ni kukilinda chama cha mapinduzi na mafisadi walioko huko. Mi naona kifutwe tu maana tangu kianzizwe sijawahi kusikia kimemchukulia hatua kigogo yeyote aliyetwajwa/usika na ubadirifu wa mali za serikali, wakijitahidi sana utasikia "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA". Lakini kwa watu wachini - dagaa wananyanyaswa sana na hukumu zao haziitaji uchunguzi wa kina unaofanyika kwao. Haya yoteni kuwapiga changa la macho wananchi.
 
Akili nyingi uondoa maarifa. Mwakyembe has goofed big time on this. Yeye kama kiongozi hasingeweka hadharani kwamba ameitwa na chombo halali cha dola kuhojiwa na amekataa. Mwakeyembe anajua hayuko juu ya sheria. Kwa nini ahofie kuojiwa in the first place. Hata kama anaona ni upuuzi angekwenda and he should have told PCCB point blank that all this is bull crap! Lakini kugoma kuhojiwa na kuweka hadharani sio jambo la kujivunia hata kidogo. Anaonyesha mfano gani? Nadhani jeri yake imepanda sana kichwani mwake and this could be his Achilles' heel. Poor Mwakyembe!

This is very low! TAKUKURU si ndio hao hao walisema RichMonduli haina tatizo mchakato wake hauna shida? Mwakyembe na tume yake wakaangalia tofauti leo hao hao wamwite Mwakyembe kumhoji....teh teh teh huhitaji kuwa Sheikh Yahaya kujua nini kinaandaliwa.....Mwakyembe huna sababu khojiwa na hao vilaza wa PCB sijui TAKUKUNGURU
 
Akili nyingi uondoa maarifa. Mwakyembe has goofed big time on this. Yeye kama kiongozi hasingeweka hadharani kwamba ameitwa na chombo halali cha dola kuhojiwa na amekataa. Mwakeyembe anajua hayuko juu ya sheria. Kwa nini ahofie kuojiwa in the first place. Hata kama anaona ni upuuzi angekwenda and he should have told PCCB point blank that all this is bull crap! Lakini kugoma kuhojiwa na kuweka hadharani sio jambo la kujivunia hata kidogo. Anaonyesha mfano gani? Nadhani jeri yake imepanda sana kichwani mwake and this could be his Achilles' heel. Poor Mwakyembe!
jambo moja umesahau ni haki yako kukataa kuhojiwa na chombo ambacho huna Imani nacho, inawezekanaje TAKUKURU ambayo kamati ya Mwakyembe imewanyoshea kidole kuja kumuhoji na kumtendea haki Harrison Mwakyembe(mb),
alichofanya ni sahihi, na ndio maana amemwambia Hosea akiwa tayari wakakutane mahakamani.
kumbuka Mengi aliwahi kumgomea Waziri Masha kua hawezi kutoa maelezo yake polisi akiweza atangulie mahakamani, ni haki yako Mtanzania mwenzangu kukataa kuhojiwa na vyombo unavyohisi havitakutendea haki.
 
This is very low! TAKUKURU si ndio hao hao walisema RichMonduli haina tatizo mchakato wake hauna shida? Mwakyembe na tume yake wakaangalia tofauti leo hao hao wamwite Mwakyembe kumhoji....teh teh teh huhitaji kuwa Sheikh Yahaya kujua nini kinaandaliwa.....Mwakyembe huna sababu khojiwa na hao vilaza wa PCB sijui TAKUKUNGURU

Two wrong can not make a right. Never. If PCCB was wrong on Richmond it does not mean that Mwakyembe should also do wrong to make it right! Ni kosa kukataa amri halali ya chombo cha dola kuhojiwa hata kama ni upuuzi. Hata kama Mwakyembe alipata ushujaa katika kufumua kashfa ya Richomnd haimfanyi kuwa juu ya sheria na baya zaidi kuliweka hadharani. Ni kwa nini aliweke hadharani ili iweje kama sio kutafuta cheap popularity? It think it is being low to be zealot supporter of Mwakyembe even when it is clear he has goofed. I think He is overstreched himself this time around.
 
Two wrong can not make a right. Never. If PCCB was wrong on Richmond it does not mean that Mwakyembe should also do wrong to make it right! Ni kosa kukataa amri halali ya chombo cha dola kuhojiwa hata kama ni upuuzi. Hata kama Mwakyembe alipata ushujaa katika kufumua kashfa ya Richomnd haimfanyi kuwa juu ya sheria na baya zaidi kuliweka hadharani. Ni kwa nini aliweke hadharani ili iweje kama sio kutafuta cheap popularity? It think it is being low to be zealot supporter of Mwakyembe even when it is clear he has goofed. I think He is overstreched himself this time around.

What is your point hapa?
 
Leo TAKUKURU Mwanza wanamfikisha mahakamani Fundi Bomba wa Dawasco ya Mwanza kwa rushwa ya laki moja. Upuuzi mtupu!
 
Kwa hali ilivyo inaonesha wazi kuwa hii TAKUKURU ni chombo cha kuwalinda mafisadi na si vinginevyo, kwani hawana mamlaka ya kumhoji kiongozi wa ngazi za juu serikalini na kwenye chama cha mapinduzi.
 
Mkuu sio wabunge tu hata rais na makamu wa rais wanapokea posho mara mbili alafu wakifika kwenye halmashauri husika wanagharamiwa pia. si unakumbuka karatu walivyokataa kumlipia msosi makamu wa rais wakisema safari yake imeshagharamiwa na ofisi yake
 
WEWE BWANA KIFIMBOCHEZA- Suala hapa siyo kuwa Mwalimu wa Sheria suala hapa ni MANTIKI. Kinachojiwa na TAKUKURU siyo malipo yao ya posho za Vikao bali ni malipo yao ya posho za kujikimu. Mtu hawezi kulipwa posho ya kujikimu zaidi ya mara moja kwa siku zile zile na kwa kazi hiyo hiyo au nyingine.

Nasema Mwakyembe atakwenda kupambana na VIJANA wa TAKUKURU ambao nao wamesoma sheria na wanazifahamu Sheria.

Suala hapa siyo MTU KUWA MPAYUKAJI ili watu wakujue kwamba unajua VITU.

Unamkumbuka Dr. Masumbuko Lamwai- unakumbuka alivyokuwa anatesa na Sheria zake za Kidokta yuko wapi.

Ndugu kaa chini tafakali na kama hujuwi vitu kasome Sheria na Kanuni zinazozungumzia masuala ya malipo ya posho ndipo uweze kuzungumza wewe!!! KAA CHONJO.

taratibu wasegese,

mwakyembe ameweka wazi kuwa takukuru haina hadhi wala uhalali (moral legitimacy) ya kumhoji yeye kwani yenyewe imechafuka na inaongozwa na mtu mchafu...kama wanaona mwakyembe kavunja sheria, waende mahakamani.

kuhusu kulipwa posho mara mbili, hili si jipya serikalini, mkuu wa mkoa anapanda ndege kuja Dar kuhudhuria semina y autawala bora wakati huo huo anamwagiza dereva wake achome mafuta na shangingi wakutane Dar...kwanini asingepanda shangingi akaokoa nauli ya ndege au akapanda ndege akaokoa mafuta ya shangingi na posho amabayo angelipwa dereva?

kama ni kweli takukuru wamedhamiria kuchunguza hili basi iwe ni katika sekta yote ya uma, si bungeni tu na kama alivyoshauri mwakyembe, takukuru ianze kujichunguza yenyewe...mwakyembe anaishi dar lakini alipotakiwa kuhudhuria semina yao alilipwa na posho ya malazi why? ina maana takukuru hakuwa hata wakijua wajumbe ya hiyo semina walikuwa wakitokea wapi?....

UPAYUKAJI.....give me a break...

Masumbuko Lamwai....alikuwa NCCR, akashindwa na sasa amerudi CCM....huyu ni tofati na Mwakyembe ambaye ameamua kupambana ndani ya CCM....hawafanani...

maswali....?
 
Mitanzania yote ni mijizi tu, angalia watu hapa wanavyotetea uwizi wa wazi wazi wa mali ya umma.

Wengi wetu hapa tunafanya hivyo hivyo huko makazini kwetu kwa kuchukua rushwa, takrima au posho zisizo na maana.

Nchi hii haiwezi kuondokana na ufisadi kwasababu kila anayepata nafasi ya kufisadi anafanya hivyo. Wengi wa wanaopinga hapa ni wale waliokosa nafasi za ulaji.

Huyo msomi Mwakyembe mbona anafundisha miaka 30 na bado ni dokta tu? Wenzake wamekuwa maprofesa yeye bado anajiona ndiye msomi kuliko wote. Sijawahi kuona mitaani vitabu vya Mwakyembe vya sheria, sijawahi kusikia kashinda kesi kubwa kubwa kama alivyokuwa Lamwai au Shivji, sasa huu usomi uko wapi?

Hapa Kyela anashindwa hata kuongoza vikao vya halmashauri na badala yake ni ugomvi tu kila siku, kuteka vijana, hiyo elimu yake ni ya kubwata tu kwenye Luninga? Yeye anapoteka vijana na kusingizia walitaka kumuua, hiyo ni sheria ya chuo kikuu gani?

Mbona 2010 inachelewa tuondokane na huyu msanii. Tumefyekelea mbali makamanda wake, anajua panga linakuja kwake.

Mitanzania ni mipumbafu kabisa!
 
Hawa jamaa waniachaga hoi sana!

Masanilo aka Ze Comedy,
Wewe beba tu mabox ya Wazungu huko Majuu; unashangaa hilo mbona hushangai mtu kuchukua posho mbili na bado akajiona hajakosea?

Wewe lipwa mara mbili kwenye hizo boksi zako tuone kama hutatupwa mpaka huko kwenu Mwanza.
 
Hizi ni habari 2 zilizoandikwa ukurasa wa mbele wa gazeti la Tanzania Daima la leo 28/10/2009. nimeziweka kwa kufuatana, ikianza ya Dk Mwakyembe kisha spika sitta

Sometimes nashindwa kuelewa hivi mhariri mkuu wa gazeti hili naye hupokea posho toka kwa Mafisadi?


Tanzania Daima - 28/10/2009

Porojo za Dk. Mwakyembe
• Atamba anajua sheria, ataibwaga TAKUKURU

na Sauli Giliard, Dodoma


MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, jana aliwashangaza waandishi wa habari wanaohudhuria mkutano wa 17 wa Bunge mjini Dodoma, baada ya kuitisha mkutano nao na kuhoji kwanini wanakunywa chai ya wabunge wakati wamelipwa posho na vyombo wanavyofanyia kazi pasipo kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), badala ya kutoa ufafanuzi wa kama alipokea posho mara mbili au la.

Dk. Mwakyembe alihoji hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari wa Bunge, baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, wakati akitoa ufafanuzi wa kukataa kuhojiwa na TAKUKURU kuhusu kuchukua posho mara mbili kwa kufanya kazi moja.

Akizungumza kwa ghadhabu, Dk. Mwakyembe alisema kitendo cha kuhojiwa na TAKUKURU wakati huu ambapo wajumbe wa kamati iliyochunguza suala la Richmond wakitaka Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk. Edward Hoseah, ahojiwe, ni mbinu za kutaka kuwanyamazisha.

Dk. Mwakyembe alisema kupokea posho ni utaratibu wa siku nyingi na wa kawaida, hivyo kuhojiwa sasa ni mbinu tu ya TAKUKURU kutaka wabunge wasimhoji Dk. Hoseah.

Alisema kwa uelewa wake wa kisheria, ikizingatiwa kuwa yeye ni mwalimu wa sheria, pamoja na kubaini mchezo huo, hakukubali kuhojiwa kama alichukua posho mara ya pili katika kikao cha kamati ya Bunge kilichofanyika mjini hapa na alitamba kuwa hata kama TAKUKURU itaamua kumpeleka mahakamani, ataibwaga vibaya.

"Lunch allowances ni utaratibu wa siku nyingi na wa kawaida. Hata waziri akitembelea mikoani huwa anaandaliwa vizuri, licha ya kwamba amepewa posho. Kwani inawezekana kutomwandalia kwa sababu amekwishapewa posho?" alihoji Dk. Mwakyembe.

Aliwashangaza waandishi wa habari alipowahoji kwanini hawajawahi kuhojiwa na TAKUKURU kwa kunywa chai ya wabunge huku ikijulikana kuwa wametumwa na vyombo vyao wanavyovifanyia kazi, huku akidai kushangazwa na hatua ya wabunge kufanyiwa hivyo sasa.

Huku akilifananisha gazeti lililochapisha habari yake ya kukataa na kuomba msaada wa Spika wa Bunge, Samuel Sitta ili asihojiwe na TAKUKURU kuhusu madai ya kupokea posho mara mbili, alisema kama hilo ni kosa, TAKUKURU ndio vinara wa kutoa posho.

Alitoa mfano wa hivi karibuni katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo, ambapo licha ya kufahamu kuwa anaishi jijini Dar es Salaam, ilimpa posho ya malazi.

"Hawa TAKUKURU ndio vinara wa kutoa posho. Inafahamika mimi naishi Dar es Salaam, wananipatia posho, leo hii pamoja na mambo mengi yanayotaka majibu wanataka kutuhoji, kama hii si kuwadhalilisha wabunge ni nini?" alihoji huku akionekana kukasirika.

Mbunge huyo mara kwa mara akihusisha kitendo hicho na mchezo mchafu unaofanywa na aliowaita mafisadi. Alisema TAKUKURU imewaita wabunge kwa kutaka kuwahoji huku wao wakitaka serikali imchukulie hatua Dk. Hoseah na kwamba hilo ni lengo mahususi la kukwamisha juhudi za wabunge.
"Sisi tunataka utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge, mojawapo ni lile la kuhojiwa kwa viongozi wa TAKUKURU," alisisitiza.

Dk. Mwakyembe alibainisha kwamba, kukaidi wito wa TAKUKURU wa kuhojiwa juu ya suala hilo kunatokana na kinga aliyonayo kama ilivyobainishwa katika kanuni za Bunge sehemu ile ya 100 pamoja na 101, ambayo inamlinda kama mtumishi wa chombo hicho cha kutunga sheria.

Aliendelea kujigamba kuwa kamwe hakuna mtu wa kumng'oa jimboni mwake na aliwataka wale aliowaita mafisadi waelewe kuwa hawawezi kumng'oa, labda wapige kambi kwa miaka mitano wakiwa pamoja na wake zao.

"Mafisadi kuning'oa Kyela ni kazi ngumu, labda washinde Kyela kwa miaka mitano pamoja na wake zao, ndiyo wanaweza kufanya hivyo," alijigamba.

Alisema wakati TAKUKURU inaendelea kung'ang'ania kuwahoji, zipo hoja za msingi zinazotakiwa kujadiliwa, ikiwa ni pamoja na ile ya nani mmiliki wa Kagoda na Richmond.
Taarifa zilizotufikia kutoka ndani ya kikao cha ndani ya kamati ya wabunge wa CCM, muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni zilieleza kuwa wabunge hao wamegawanyika kuhusu suala la kuhojiwa na TAKUKURU, baadhi wakikubaliana na hatua hiyo na wengine wakipinga na kutaka isitishwe mara moja.

Taarifa hizo zilieleza kuwa kundi la kwanza linaloungwa mkono na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, linaunga mkono hatua hiyo ya TAKUKURU, kwa hoja kwamba fedha nyingi za serikali zimepotea kwa kuwalipa posho mara mbili wabunge. Kundi la pili linalodaiwa kuungwa mkono na Spika Sitta linadaiwa kuipinga hatua hiyo ya TAKUKURU, kwa madai kuwa inawadhalilisha wabunge. Hata hivyo habari hizo zilidai kuwa, licha ya Spika kutaka hatua hiyo isitishwe, Pinda alitangaza msimamo wake kuwa ni lazima kazi ya kuwahoji wabunge wote wanaotuhumiwa kuchukua posho mara mbili iendelee.



Spika Sitta kigeugeu
• Akana kauli zake, barua rasmi ya ofisi yake

na Charles Mullinda

SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, sasa ameanza kutoa kauli tatanishi baada ya jana kuzungumza na Tanzania Daima Jumatano na kueleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekiuka taratibu kwa kuwaita na kuwahoji baadhi ya wabunge wanaotuhumiwa kuchukua posho mara mbili, baada ya kufanya kazi moja.

Sitta ambaye yuko mjini Dodoma anakoongoza mkutano wa 17 wa Bunge, alihojiwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu msimamo wake dhidi ya TAKUKURU kuwahoji wabunge na kutoa ufafanuzi wa barua iliyoandikwa na Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah, ambayo gazeti hili limeiona, kwenda kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, Edward Hoseah, ikimtaka alitafutie ufumbuzi suala la wabunge kulipwa posho mara mbili. Katika majibu yake Spika Sitta alikana kuifahamu barua hiyo na kueleza kuwa si jambo la ajabu kwa ukarimu wa Kitanzania wabunge kulipwa posho mara mbili na aliwashutumu baadhi ya viongozi wa juu wa serikali bila kuwataja majina kwa kulitisha Bunge ili lisitekeleze majukumu yake inavyotakiwa.

Kauli hii ya Sitta imekuja siku chache baada ya Jumatatu wiki hii kunukuliwa katika baadhi ya vyombo vya habari akilalamika kuwa TAKUKURU inawadhalilisha wabunge inapowaita na kuwahoji bila kufuata utaratibu wala kanuni na jana alinukuliwa tena na baadhi ya vyombo vya habari akitoa mwongozo kwa wabunge kukubali kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU inapowaita kuwahoji.

Awali alinukuliwa akieleza kuwa hatua iliyofikiwa na TAKUKURU kuwaita wabunge na kuwahoji ni uhdalilishaji na imekiuka utaratibu, kanuni na sheria za nchi dhidi ya Bunge kama taasisi inayojitegemea.

Katika kauli hiyo, Sitta pia alieleza kuwa hajui kuwapo kwa jambo hilo kwa sababu hajataarifiwa na kwamba hajui kinachohojiwa na TAKUKURU kwa sababu taarifa hizo anazisoma katika vyombo vya habari.

Alitoa tahadhari kwa taasisi nyingine za uchunguzi ikiwamo TAKUKURU kutoa taarifa ya maandishi ofisini kwake linapotokea jambo kama hilo ili Bunge liwe na taarifa na litoe utaratibu.

Siku moja baada ya Spika kunukuliwa akitoa kauli hiyo, jana alinukuliwa akitoa kauli nyingine aliyokuwa ikipingana na ile ya kwanza.

Gazeti moja la kila siku liliandika habari za ndani kutoka katika kikao cha wenyeviti wa kamati za Bunge, ambapo Spika Sitta alitoa mwongozo kwa wabunge kutoa ushirikiano kwa maofisa wa TAKUKURU wanaowaita kuwahoji.

Hata hivyo alipozungumza na gazeti hili jana, Spika Sitta alisema msimamo wake halisi kuhusu suala hilo ni kupinga TAKUKURU kuwaita wabunge na kuwahoji bila yeye kutaarifiwa.

"Ninayoyaongea sasa, ndiyo unapaswa kuyachukua kwa sababu ndio msimamo wa Spika. Kwanza mimi siijui barua hiyo. Pili, TAKUKURU wamekosea kulifanya suala hili la kawaida sana, wabunge si watu wa kuchezea, ni watu wakubwa na muhimu sana wanaopaswa kuhojiwa kwa heshima na viongozi wa juu wa vyombo vya usalama.

"Na kabla ya kuhojiwa, ni lazima Spika ningetaarifiwa kwanza na kuandaa mazingira ya kuhojiwa kwao. Haiwezekani watu wa chini wasiojua maana ya mbunge kumhoji mbunge pasipo Spika kujua. Na kikawaida, takrima kwa ukarimu wa Kitanzania ni jambo la kawaida, ni ukarimu wa Kitanzania, hivyo hakuna posho mara mbili hapo. Ni ukarimu tu na wabunge wanaruhusiwa kuchukua," alisema Spika Sitta.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Katibu wa Bunge, Kashililah kama ni wa shaka kiasi cha kuandika barua nyeti inayoomba msaada wa taasisi nyingine pasipo kumtaarifu, Spika Sitta alisema haamini kama Kashililah aliandika barua hiyo na kama aliandika, basi alilazimishwa na viongozi wa juu wa serikali.

Katika hatua ya kushangaza, Spika alitoa kauli nyingine kuwa hata kama Kashililah aliandika barua hiyo, basi alikuwa anatekeleza majukumu yake ya kiutalawa hivyo anaweza asimtaarifu lakini TAKUKURU walipaswa kutochukua hatua zozote kulingana na barua hiyo kabla ya kumtaarifu.
"Mambo ya utalawa sishiriki kila jambo, mhusika mkuu ni katibu na nadhani alilichukua kiutawala zaidi. Lakini TAKUKURU kabla ya kuanza kuifanyia kazi barua hiyo ni lazima wangenitaarifu kwanza Spika.

"Hili jambo tumelijadili sana jana na juzi, tumebaini kuwa Katibu wa Bunge alitishwa sana. Watu wakubwa serikalini wamekaa vikao vingi tu, wamemtisha sana katibu kuwa ni lazima aandike barua hiyo, oh… eti ni maagizo ya rais, wakamlazimisha kuandika barua ile. Hili mimi siliafiki na tumefikisha malalamiko kwa waziri mkuu leo.

"Bunge haliwezi kuendeshwa kwa vitisho, serikali iache kabisa kulitisha Bunge…. Bunge litakataa. Kama mbunge anatuhumiwa kuna Kamati ya Maadili ya Bunge, itashughulikia tuhuma hizo, si mambo haya yanavyofanyika sasa. Ni njama tu, lakini kamwe hatulegezi kamba, Bunge litaendelea na kazi yake pamoja na vitisho vyote," alisema Spika Sitta. Wakati Sitta akitoa kauli tatanishi kuhusu barua iliyoandikwa na Kashililah kwenda kwa Hoseah huku akisisitiza kutoifahamu, Tanzania Daima Jumatano imefanikiwa kuiona barua hiyo yenye kumbukumbu namba CEB.50/155/05/81 ikiwa na kichwa kinachosomeka: ‘Baadhi ya kamati za Bunge kuomba takrima serikalini na katika mashirika ya umma.'
 
Masanilo aka Ze Comedy,
Wewe beba tu mabox ya Wazungu huko Majuu; unashangaa hilo mbona hushangai mtu kuchukua posho mbili na bado akajiona hajakosea?

Wewe lipwa mara mbili kwenye hizo boksi zako tuone kama hutatupwa mpaka huko kwenu Mwanza.
MMMH ni mawazo yako, sahihi kwa upeo wako, fikra dhalili, na mwakyembe amekiri kupokea Posho mara mbili, jamani siwampeleke basi mahakamani. kasema haoni haja ya kuhojiwa, ni haki yake kwanza, TAKUKURU ni chombo halali kabisa chini ya sheria, sasa ameisha amua kugoma kutoa taarifa. na wakutane mahakamani ambako haki hutafsiriwa kwa kina na mapana yake.
kwa taarifa yako mawaziri wote wanapokea posho mbili, kwanini atajwe sana Mwakyembe....ooh kalaghabaho mjomba
 
Ehhh,
Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana. Mbona mnashabikia namna hii Mwakyembe kunyanyaswa? Kwani Mwakyembe hana makosa? Kwani wabunge wa CCM hawana makosa? Kwanza TAKURURU ianze na hii habari kuwa kila mbunge wa CCM wakati wa uchaguzi alimegewa 5M kutoka kwa mshika kapu la fweza, homeboy Rostam Azziz. Na homeboy alivyo na akili, akawasainisha wote ili wasimruke, hahahaaaaaaa........ Wote waliopokea 5M wahojiwe nao. Homeboy Hosea wembe ule ule.

Hosea (TAKURURU), weee fanya kazi yako bila kitisho kwa mtu yeyote. Hata nduguyo Sitta na yeye mlime tu madudu yake. Kama wao wanataka kukuDO basi na wewe ni kama wimbo wa P-Square yaani "If you do me, i do you". Maadamu walikuwa na muda wa kukudeal na wakawa wanazembea hiyo si tatizo lako sasa. Uchaguzi unakuja na wabunge wengi wa CCM wanataka pa kutokea na wa kumtoa MHANGA utakuwa wewe. Usikubali kabisa. AU mnakufa wote au WANYAMAZE MIELE na watafute kingine cha kutokea. Na kwa sababu hawana na Richmonduli inauzika kirahisi kwa wananchi na hasa kwa Mwakyembe, basi lazima atalia nayo ili Watanzania wamuoneehuruma.

Na nyie wabunge vipi? Mnakubali kuendeshwa na Hosea? Mlililea JINI mnaona sasa? Jini limeshakuwa kubwa sana na haliwezi kuingia kwenye chupa tena. Sasa lenyewe ndiyo litaanza kuwsulubu. Mlitakiwa kuwa mmeshamuondoa Hosea zamani sana ila tatizo huyu Ngosha ni NGOSHA kweli. Hamumuwezi kwa sababu amewakamata PABAYA na kumkolimba inakuwa ngumu maana huko yeye ndiyo maeneo yake ya kujidai. Sasa mmebaki kulialia kwa wananchi. Lenyewe liko kimya tu LINAFANYA VITU VYAKE, hahaaaaaa Safi sana.

Kama huna akili utakuwa hukunielewa. Ila kama una akili na unaipenda nchi yako ya TANZANIA, basi amini kuwa hii ni HABARI nzuri sana nchini. Ili nchi iende, inabidi Static Energy ibadilishwe na iwe kinetic energy. Na hii bahati mbaya kila siku inaleta FRICTIONS. Kukiwa na friction (msuguano) kunatokea JOTO ambalo sasa tunaliona akina Mwakyembe na Sitta wanatokwa. Ila bila friction, basi hakuna joto na hakuna movement. Ombi kwenu wahusika.

1. Wabunge, msipomuwahi Hosea, atawawahi nyie na kuwamaliza kisiasa na hata mkaenda Jela.
2. HOSEA (TAKURURU), usipowawahi wabunge na kuwanyamazisha, mwisho wako utakuwa mbaya. WANASIASA HAO!!
 
Kwa hiyo wewe unaridhia TAKUKURU kuwaoji wabunge? Walikuwa wapi siku zote wasiwaoji?, eti sasa kwa sababu wameona wabunge wamesimama kidete kwa ajili ya Richmond n.k., serikali inawaburuza (TAKUKURU) kwaziba midomo wabunge.

suala la richmond walikuwa wapi siku zote?
 
Back
Top Bottom