Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Hivi mnaposema TAKUKURU wanaacha kufuatilia rushwa kubwa wanawafuatilia wabunge na posho wanazopewa mnamaanisha nini?? Hizi hizi kamati za bunge ndizo zinazokagua mashirika ya umma, taasisi, halmashauri, n.k sasa kama wajumbe wa kamati hizo wanahongwa tutegemee nini??
Mwakyembe namuheshimu kwa jinsi alivyofanya kazi kama mwenyekiti wa kamati teule iliyochunguza mchakato wa kuipata richmond, lakini hilo halinizuii kumkosoa pale anapokosea!! Mbona Lowassa kafanya mambo mengi mazuri lakini alipohusishwa na richmond tulitaka ajiuzulu????
PCCB just do your job, mna mamlaka ya kumhoji mtu YOYOTE bila kutoa taarifa kwa YEYOTE!!!
 
Hosea ni FISADI.

Wabunge ni MAFISADI (waliopokea Posho).

Hivi Dr. Slaa pia alipokea? Maana wangelikuwa wameshambeba siku nyingi na kumrunda Keko.

Acha wazichape, siri nyingi ya ULAJI zitafumuka. Waandishi wa habari nao wanakomba..

Kumbe hii Tanzania nchi TAJIRI saana.

Simuonei huruma Hosea na Mwakyembe. Acha waburuzane tu na Mungu bariki wote wapakana MAJI TAKA.

Kama wamechukua Posho Mara Mbili waachwe eti kisa ni akina Mwakyembe
 
mmh Nyie ongeeni yooote but Mwakyembe yupo juu na aendeleee hivyo,
acheni kumkatisha tamaa MAFISADI

Mbona wewe wamkatisha tamaa HOSEA? Hakuna aliyesema Mwakyembe akate tamaa. Yeye aendelee kuwashughulikia akina HOSEA na Richmond ila akumbuke milele maneno ya KIKWETE kuwa " UKITAKA KULA BASI KUBALI NA WEWE ULIWE KIDOGO".
Sasa yeye wakimgusa kidogo anaruka utafikiri bikira, ehhh Kaza moyo Mwakyembe, ndiyo SIASA hiyo na hapa si sheria tena.
 
HIYO HELA ALIYOLIPA INALINGANA NA KAGODA, RICHMOND AU EPA? Tukifatilia vi kashfa mnavyotoa hakuna serikalini atakayepona.

HAPA TUNAJADILI ZAIDI MAHELA MAKUBWA.

Na haya yote yanakuja leo why?

Kwa hiyo yeye tumwite fisadi mtoto?
 
Mwakyembe kama alivyo raia mwingine yeyote Tanzania kama Chenge, Lowasa, etc akivunja sheria anatakiwa apelekwe mahakamani. Wapo ambao wanajulikana kabisa kuiibia nji hii kiasi cha kuua mamilioni ya raia kwa kuwakosesha huduma za msingi na hadi tunaposhabikia hata mmoja wao hajatuhumiwa na vyombo husika achilia mbali kupandishwa kizimbani. Sababu ni kwamba ushahidi wao haupo. Sishangai kwahiyo, kwamba kuna uwezekano wa kumkuta Mwakyembe na kosa na asishtakiwe vile vile kwa sababu ni mpaka 'ushahidi' upatikane. Bado nina ile imani ya binadamu wote ni sawa (at least mbele ya sheria) kwa hiyo sioni sababu ya ushahidi wa Mwakyembe kuonekana kuliko wa wengine.

Tumezoea hata hivyo wala hakuna astaajabishwaye tena na mwizi wa kuku kufungwa maisha wakati mwizi wa kiwanda cha serikali cha kutotolea kuku anapewa ulinzi na serikali.
 
Sio WABUNGE tu wanaotakiwa kuhojiwa! Mawaziri wanazitafuna zaidi TAASISI zilizo chini ya wizara zao. Nao wahojiwe kama sio kushtakiwa kabisa. Mapesa yanayotafunwa kwa mtindo huu na WANASIASA wetu ni mengi kuliko haya ya EPA tunayopigia kelele humu. Tumechelewa mno kuliangalia hili.

Jamani kama ni kuchukua allowance mara mbili au sitting allowance mara mbili basi hakuna takayepona serikalini, itabidi Takukuru waombe kuongezewa wafanyakazi kukabili kirusi hicho kibaya hapa Tanzania.

Wenzangu jamvini nakumbuka kuna mkurugenzi wa wilaya alisimashwa kazi kwa kukataa kulipa malazi kwa mkuu mmoja serikalini, akisema kuwa hakuona sababu kwani ziara hiyo mkuu huyo aligharimiwa???
 
Katika HILI, Watetezi wa Mwakyembe mmekosa Mlingoti wa Kujishikia
 
Dr. Mwakiyembe anaogopa kivuli chake mwenyewe. Kwanini asiende akahojiwe kama yeye ni innocent kuna shida gani? Eti anapambana na ufisadi, wenyewe ndiyo mafisadi sema ya kwao hayajawekwa juani bado, lakini ipo njiani...Hakuna aliyejuu ya sheria, aende asitatfute sypmathy ya wananchi kwa mgongo wa mpiganaji wa ufisadi. Mbona Mwenyekiti wa kamati yake ya Nishati na Madini alikwenda akahojiwa?
 
Ni ishu ya kujua haki yako ya msingi. Besides, nchi haina uongozi ukiwa confident basi hakuna wa kukugusa. Whether ana kosa au hana, it doesn't matter. Wangapi tunawajua wenye makosa na hakuna wa kuwafanya chochote?
 
This is very low! TAKUKURU si ndio hao hao walisema RichMonduli haina tatizo mchakato wake hauna shida? Mwakyembe na tume yake wakaangalia tofauti leo hao hao wamwite Mwakyembe kumhoji....teh teh teh huhitaji kuwa Sheikh Yahaya kujua nini kinaandaliwa.....Mwakyembe huna sababu khojiwa na hao vilaza wa PCB sijui TAKUKUNGURU

Ushabiki utakuuwa we jamaa!!!yani kwa kuwa uliichunguza polisi kwaiyo ata ukitenda kosa la jinai kama kuua usihojiwe na polisi? Eti dokta wa sheria!!!wakati hajui kuwa yeye ni mmoja wa wabunge waliopitisha sheria hii hii ya PCCA namba 11/2007 ambayo ukisoma section 10 (1) An officer of the Bureau investigating an offence under this Act may-
(a) order any person to attend before him for the purpose of being interviewed orally or in writing in relation to any matter which may assist investigation of the offence
halafu wandai wao ni wabunge eti ni watu wakubwa hawatakiwi kuhojiwa!!!!
Yaani huyu dokta ni kichekesho sana....ktk sheria hiyo hiyo kuna offence of disclosure of identity yani wakati uchunguzi unaendelea kuhusu jambo flani hakuna mtu anayepaswa kufichua utambulisho wa mtu anayechunguzwa au kitu kinachochunguzwa bila mamlaka ya kisheria kufanya hivyo!!Mwakyembe anapiga kelele kuwa anachunguzwa!hajui kuwa anajiongezea makosa... eti dokta wa sheria tene aliyeipitisha sheria yenyewe halafu haijui.
 
Hiyo sheria inasemaje mtu akikataa kuhojiwa?
 
Angalia reaction ya Takukuru kuhusu Mwakyembe kukataa kuhojiwa.

"Kwa upande wao, TAKUKURU wamesema hakuna njia yeyote ambayo Mwakyembe anaweza kuitumia kukwepa kuhojiwa kuhusu tuhuma za kupokea posho mara mbili..

Akizungumza na Mtanzania ofisini kwake jana, Ofisa Mahusiano wa TAKUKURU, Doreen Kapwani, alisema Dk. Mwakyembe atakataa kuhojiwa, basi sheria itachukua mkondo wake, kwa sababu hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria.

Ofisi ya Bunge ndio ilituandikia barua ikituomba kuchunguza tuhuma dhidi ya wabunge ambao wanatuhumiwa kuchukua posho mara mbili wanapokuwa kwenye shughuli za Kamati ya Bunge. Sasa Wabunge wengine wamekubali kuhojiwa, yeye Dk. Mwakyembe anaogopa nini kama anajua hana tatizo lolote?" alihoji Ofisa Uhusiano huyo.

Alisema ikiwa Dk. Mwakyembe anayo kinga kama alivyodai, basi aeleze ni sheria ipi inayompa kinga hiyo ndani ya Katiba ya nchi.
 
Ushabiki utakuuwa we jamaa!!!yani kwa kuwa uliichunguza polisi kwaiyo ata ukitenda kosa la jinai kama kuua usihojiwe na polisi? Eti dokta wa sheria!!!wakati hajui kuwa yeye ni mmoja wa wabunge waliopitisha sheria hii hii ya PCCA namba 11/2007 ambayo ukisoma section 10 (1) An officer of the Bureau investigating an offence under this Act may-
(a) order any person to attend before him for the purpose of being interviewed orally or in writing in relation to any matter which may assist investigation of the offence
halafu wandai wao ni wabunge eti ni watu wakubwa hawatakiwi kuhojiwa!!!!
Yaani huyu dokta ni kichekesho sana....ktk sheria hiyo hiyo kuna offence of disclosure of identity yani wakati uchunguzi unaendelea kuhusu jambo flani hakuna mtu anayepaswa kufichua utambulisho wa mtu anayechunguzwa au kitu kinachochunguzwa bila mamlaka ya kisheria kufanya hivyo!!Mwakyembe anapiga kelele kuwa anachunguzwa!hajui kuwa anajiongezea makosa... eti dokta wa sheria tene aliyeipitisha sheria yenyewe halafu haijui.
.
mkuu jumboplate,
tangu mwanzo tulisema huyo masanio ni mjinga na anaushabiki wa kipumbavu.nafikiri ata baba yeke alikua hivyo hivyo.mwakyembe kwa sasa hana pa kukimbilia.watu wake wa karibu wote wamemwagwa serikali za mitaa.sasa leo hii anaongea kwa hasira eti hakuna wa kumtoa jimbon kwake,yeye ana hati miliki hapa kyela?
 
Kifungu cha 10(1) cha PCCA na vifungu 10(2) na 2A vya sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 kwa pamoja na kifungu cha 8(1) cha PCCA vinawapa mamlaka ya kumtaka mtu yoyote kufika kutoa maelezo na iwapo mtu atakataa wito huo anakuwa anatenda kosa la jinai hivyo anaweza kushtakiwa mahakamani.
 
Ambao hammjui Mwakyembe mtapata shida sana, jamaa ni mpambanaji kwa mambo anayopingana nayo lakini yeye mwenyewe ni fisadi mkubwa kwenye mambo mengine ambayo anafaidika nayo.

Kuna kashfa nyingine inakuja ambayo kwa msaada wa spika Sitta kalipwa mamilioni ya pesa kwa kusingizia kwamba alienda kutibiwa nje (Ujerumani) wakati ule baada ya ajali wakati alikuwa amejifungia nyumbani kwake Kunduchi.

Nchi hii inaliwa na hao hao wanaojifanya wanailinda.

Inategemea sana..! unaweza kusafiri wewe au kumsafirisha doctor kuja kukutibu nyumbani kwako kwa gharama zile zile au zaidi ..!!! Akikuletea riport ya frying Doctor utasema je ? Swala si kwenda Ujerumani bali Fedha zilizotolewa ziliendana na gharama za matibabu yake?
 
.
mkuu jumboplate,
tangu mwanzo tulisema huyo masanio ni mjinga na anaushabiki wa kipumbavu.nafikiri ata baba yeke alikua hivyo hivyo.mwakyembe kwa sasa hana pa kukimbilia.watu wake wa karibu wote wamemwagwa serikali za mitaa.sasa leo hii anaongea kwa hasira eti hakuna wa kumtoa jimbon kwake,yeye ana hati miliki hapa kyela?

Huyu Mwakyembe ni siasa tu!!!!kwani lazima uwe mbunge ndio uweze kupambana na ufisadi??? yani anataka apewe takrima kwa fedha zetu halafu sisi tucheke tu kama wajinga???!!!
 
.
mkuu jumboplate,
tangu mwanzo tulisema huyo masanio ni mjinga na anaushabiki wa kipumbavu.nafikiri ata baba yeke alikua hivyo hivyo.mwakyembe kwa sasa hana pa kukimbilia.watu wake wa karibu wote wamemwagwa serikali za mitaa.sasa leo hii anaongea kwa hasira eti hakuna wa kumtoa jimbon kwake,yeye ana hati miliki hapa kyela?

Changia kitu cha msingi kama huna cha kuchangia kaa kimya achana na personal issues za mtu.
 
Inaonyesha ni huyu huyu Mwakyembe tu. Namwita hivyo maana nimeondoa ile title ya Dr. maana haimfai na hastahili. Anasema maneno kama mtu hakwenda shule!!!

Hivi Takukuru kwanini haitoi WARRANT OF ARREST kama anakataa kuhojiwa. Hapo ndio atakoma ubishi. Lazima wale nae sahani moja mapaka aache ufisadi.
unachekesha mzee DR sio ule wa dr matunge wa kijiweni. labda wewe ndio uitwe Dr maana unaonyesha unafaa kuwa DR ( LOL)
 
Back
Top Bottom