Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,035
Mbunge wa kyela Dr. Harison Mwakyembe amekataa kuhojiwa na TAKUKURU kama baadhi ya wabuge wengine walivyohojiwa na taasisi hiyo kwa madai kuwa hizo ni mbinu za kutaka kuwaziba midomo wabunge. Katika maojiano yake na vyombo vya habari, Mwakyembe amesema, TAKUKURU anawapigia simu wabunge (Mmoja mmoja) na kuwaoji kwa takriban masaa hadi matatu kinyume na sheria kwani maojiano hayo hayawekwi kwenye maandishi.

Source Nipashe/ITV
 
Kama ulikuwa unafuata sheria Dk Mwakyembe nakupa big up.Tatizo letu waTZ wengi hatujui sheria wala haki zetu za msingi tunaburuzwa tu na kila mtu matokeo tunapoteza mali zetu hata utu wetu.TAKUKURU wakifuata sheria sidhani kama mwakyembe angekataa.Mwito kwa waTZ wote tujifunze sheria jamani na haki zetu tuzijue.
 
Jamani!!!!!!, TAKUKURU imeshindwa kuwaoji na kuwachukulia hatua stahili mafisadi sasa inawaoji wabuge? Naona hii ni mbinu ya mafisadi kuwaziba midomowabunge wanao piga vita ufisaidi nchini. Mbaya zaidi hawa wabuge wanadhalilishwa kwani watu wanaowaoji ni watu wa hali/nafasi ya chinikulingana na nafasi walizo nazo wabunge.
 
Mwakyembe kala haya mapesa ya UMMA. Ayarudishe. Haimsaidii sana kurukaruka hivi.
 
Jamani Watanzania tusichanganye MADAWA- Hapa TAKUKURU inataka kutekeleza wajibu wake. Sheria na Kanuni za malipo ya Posho zinasema Mtumishi au Mtu au Taasisi haiwezi kulipwa zaidi ya mara moja kwa ajili ya suala hilo hilo. Sasa hawa Wabuneg wanalipwa Posho za kujikimu (Subsistance Allowance) na Ofisi za Bunge, Lakini wakienda kwenye Taasisi au Mashiriki ya Umma au Serikali za Mitaa wanalipwa tena posho za kujikumu (Subsistance Allowance) kwa shughuli hiyo hiyo ambayo Bunge imeshawalipa.

Hapa kuna posho za aina mbili ambazo tusizishanganye. Posho ya kujikimu (Subsistance Allowance) na posho ya Kikao (Sitting Allowance). Wao Wabunge walitakiwa kulipwa posho za Vikao (Sitting Allowance) kama wanatembelea Mashirika ya Umma na kukawepo na Vikao vya kupitia taarifa ya Mashirika au Taasisi hizo na siyo kulipwa posho ya Kujikimu.

Suala la kuhojiwa kwa Wabunge na TAKUKURU- Huu ndiyo urasimu ambao hata wabunge wenyewe wanaihoji Serikali kutowachukulia hatua watuhumiwa wa sakata la RICHMOND. Unajua kila unapotaka kufanya suala la maendeleo Tanzania unakuta kuna URASIMU MKUUUUUUBWWWWAAAAAA!!! ambao mpaka unapo kamilisha taratibu zake kunakuwa hakuna maana tena. mini nasema acha wahojiwe.

Mapadri wa Roma wanamsemo wao mzuri sana nami hua naupenda nami leo nawapeni unasema hivi:

"MBWA HUBWEKA SANA ANAPOONA CHAKULA CHA BWANA WAKE KINALIWA NA MTU MWINGINE. LAKINI MBWA HUYO HUYO ANAPOKULA CHAKULA HICHO CHA BWANA WAKE BILA RIDHAA YA BWANA WAKE - HUWA MKALI PALE ANAPOKATAZWA KUENDELEA KUKILA"

Kama ufisadi ni kutumia Tshs. 10,000/- za wanakijiji na kunapelekea Afisa Mtendaji wa Kijiji ahojiwe na kufuikishwa Mahakamani, inakuwaje suala la Wabunge kuchukua Posho mara 2 na wanapotakiwa kuhojiwa INAKUWA SUALA LA OOOO!!!!, UNAJUA!!!. Jamani ACHENI UMBUMBUMBU fungeni macho na msiwe BENDERA KUFUATA UPEPO.
 
Kweli wa TZ hatujui sheria

Kama kuna mtu alimsikiliza Mwakyembe vizuri amefafanua vizuri, Hawa Takukuru naona wamekurupuka bila kusomas heria vizuri na mbaya zaidi wamekutana na Mwalimu wa Mwanasheria

Hapo Kazi ipo......watanzania tunatakiwa kuzijua sheria na haki zetu bila hivyo tutaburuzwa
 
Mwakyembe kala haya mapesa ya UMMA. Ayarudishe. Haimsaidii sana kurukaruka hivi.

Kwa hiyo wewe unaridhia TAKUKURU kuwaoji wabunge? Walikuwa wapi siku zote wasiwaoji?, eti sasa kwa sababu wameona wabunge wamesimama kidete kwa ajili ya Richmond n.k., serikali inawaburuza (TAKUKURU) kwaziba midomo wabunge.
 
WEWE BWANA KIFIMBOCHEZA- Suala hapa siyo kuwa Mwalimu wa Sheria suala hapa ni MANTIKI. Kinachojiwa na TAKUKURU siyo malipo yao ya posho za Vikao bali ni malipo yao ya posho za kujikimu. Mtu hawezi kulipwa posho ya kujikimu zaidi ya mara moja kwa siku zile zile na kwa kazi hiyo hiyo au nyingine.

Nasema Mwakyembe atakwenda kupambana na VIJANA wa TAKUKURU ambao nao wamesoma sheria na wanazifahamu Sheria.

Suala hapa siyo MTU KUWA MPAYUKAJI ili watu wakujue kwamba unajua VITU.

Unamkumbuka Dr. Masumbuko Lamwai- unakumbuka alivyokuwa anatesa na Sheria zake za Kidokta yuko wapi.

Ndugu kaa chini tafakali na kama hujuwi vitu kasome Sheria na Kanuni zinazozungumzia masuala ya malipo ya posho ndipo uweze kuzungumza wewe!!! KAA CHONJO.
 
Kama ulikuwa unafuata sheria Dk Mwakyembe nakupa big up.Tatizo letu waTZ wengi hatujui sheria wala haki zetu za msingi tunaburuzwa tu na kila mtu matokeo tunapoteza mali zetu hata utu wetu.TAKUKURU wakifuata sheria sidhani kama mwakyembe angekataa.Mwito kwa waTZ wote tujifunze sheria jamani na haki zetu tuzijue.

"Mkuu naomba nielekeze kitabu cha sheria za nchi zinazohusu mwananchi naweza kukipata wapi?"
 
Kwa hiyo wewe unaridhia TAKUKURU kuwaoji wabunge? Walikuwa wapi siku zote wasiwaoji?, eti sasa kwa sababu wameona wabunge wamesimama kidete kwa ajili ya Richmond n.k., serikali inawaburuza (TAKUKURU) kwaziba midomo wabunge.
Sio WABUNGE tu wanaotakiwa kuhojiwa! Mawaziri wanazitafuna zaidi TAASISI zilizo chini ya wizara zao. Nao wahojiwe kama sio kushtakiwa kabisa. Mapesa yanayotafunwa kwa mtindo huu na WANASIASA wetu ni mengi kuliko haya ya EPA tunayopigia kelele humu. Tumechelewa mno kuliangalia hili.
 
Huo ndio utawala wa sheria dk mwakyembe, hakuna aliye juu ya sheria.nenda takukuru kasaidie uchunguzi unaogopa nini kwani?
 
HAPA ndipo Watanzania tunapo onyesha UMBUMBUMBU. TAKUKURU siyo HOSEA, hapana TAKUKURU ni Taasisi ITAENDELEA KUFANYA KAZI KAMA Taasisi na siyo kama HOSEA. Kwa Hosea kutaka kuhojiwa na Wabunge kuhusu RICHMOND hakuizuwii TAKUKURU kuendelea kutekeleza majuku yake ndugu yangu tambua hilo. TAKUKURU siyo Mke wa HOSEA kusema kwamba akikamatwa HOSEA basi TAKUKURU isendelee kufanya kazi sababu Bwana wao kakamatwa HAPANA.
Suala la TAKUKURU kuona leo ndiyo wakati muafaka wa kuwahoji Wabunge. elewa kwamba suala lolote la kisheria linahitaji TAFAKURI ya kina ili kuweza kulichukua. TAKUKURU imefanya uchunguzi na imejirisha kwamba, kuna hoja za kuwauliza Waheshimiwa kwamba kuna suala hili la wao kupokea posho za KUJIKIMU MARA MBILI KWA TAREHE ZILE ZILE sasa ni kazi ya WABUNGE kusema kwamba oooooooooooooooeeeeeeeeeeeeeeeeeeuuuuuuuuuuuuuuuu n.k

Halafu hivi wabunge hao kusema sema kuhusu UFISADI ni TIKETI YA WAO KUWA JUU YA SHERIA ETI??? KWA NINI BADO UMELALA.
 
1. Tangu Dkt Harrison George Mwakyembe ajigambe kwamba anapambana na ufisadi, hasa baada ya Ripoti ya Richmond mwenendo wake katika upambanaji huo bado haujaeleweka hasa katika kauli zake na matendo yake!

2. Baada ya Ripoti ya Richmond alidai kwamba kuna mambo ambayo wao (wanakamati teule) waliyaacha (hawayakuyafanyia kazi) "ili kulinda heshima ya Serikali!" Hii Serikali ni ipi ambayo heshima yake ilitakiwa ilindwe maana Waziri Mkuu wa wakati huo, Edward Lowasa alitakiwa apime uzito mwenyewe, na kweli Lowasa alipima uzito na kuachia ngazi. Vile vile mawaziri Msabaha na Karamati waliachia ngazi. Sasa Serikali ipi ambayo Kamati Teule ilikuwa inailinda? Hapa tuliachwa vinywa wazi kuhusu dhamira hasa ya "wapambanaji" hao.

3. Kabla vumbi halijatua tukasikia kwamba Dkt Mwakyembe alijihusisha na umeme wa upepo na haku-declare interest wakati alipokuwa anaongoza Kamati Teule kuhusu Richmond. Japokuwa Mwakyembe alijitahidi kueleza sana kwamba alitakiwa a-declare "pecuniary interest" (financial interest) na sio vinginevyo kulingana na Kanuni za Bunge, katika suala nyeti kama hilo alitakiwa aliweke wazi ili kusionekane kuwa kuna mgongano wa maslahi! Hata hiyo aliyodai kuwa ni "pecuniary interest" ni subject to interpretation kiasi kwamba suala la umeme wa upepo linaweza kuwekwa kwenye mukhtadha huo!

4. Dkt Harrison George Mwakyembe aliitwa majuzi na TAKUKURU kwa ajili ya kueleza uhalali wa kupokea posho mara mbili akadai, tena kwa dharau kubwa kwamba, amekataa kwenda kwa sababu eti Dkt Edward Hosea, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, suala lake bado linachunguzwa na kwamba nia ya TAKUKURU ni kuwaziba midomo "wapambanaji." Hoja iliyopo ni kwamba, Je, kupokea posho mara mbili toka kwenye Serikali hiyo moja kwa kazi ile ile sio kosa? Katika maelezo ambayo Dkt Mwakyembe amekuwa anayatoa kwa waandishi wa habari ameeleza kwamba suala la kupokea posho zaidi ya mara moja kwa kazi ile ile limeanza muda mrefu! Huyu Mwalimu Mwanasheria akumbuke kwamba hatuongelei practice (mazoea) bali tunaongelea sheria na uhalali wa malipo hayo. Maelezo yake kwamba TAKUKURU nao waliwahi kuwalipa posho mara mbili hayana mshiko kwa sababu TAKUKURU ndio waliowaita kwenye Semina hizo na walistahili kuwalipa. Sasa kama waliapply posho kule Bungeni TAKUKURU wangejuaje kama wamelipwa Bungeni. Kwa nini Wabunge hawakuzikataa hizo posho?

5. Kuhusu Dkt Harrison George Mwakyembe kukataa kuhojiwa na TAKUKURU kwa madai ya kuwa na kinga na kwamba bunge ni muhimili kamili! Kama Bunge ni muhimili kamili, mbona Kamati Teule ya Bunge iliwahoji Utawala ambao pia ni muhimili kamili wa dola? Hivi mipaka ya kinga ya wabunge inaishia wapi? Mbona wakati akina Mramba walipohojiwa hatukusikia juu ya kinga za bunge na wabunge? Hii kinga inawahusu "wapambanaji" tu! Hebu tuangalie Ibara ya 100(1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria na. 15 ya mwaka 1984 kuhusu kinga ya Bunge kama alivyodai Dkt Mwakyembe: "100 (1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge. (2) Bila kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo."
Ukisoma between lines utaona kwamba kinga ya Bunge ni ndani ya Bunge wakati wa majadiliano na kinga hiyo inahusu uhuru wa kutoa mawazo tu! Sasa hapa mambo ya kulipwa posho zaidi ya mara moja yanaingiaje?
Kwa hiyo Dkt Mwakyembe asijifiche kwenye kivuli ambacho hakipo, atekeleze Kifungu cha 10 (1) (a) na (c) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, 2007, Na. 11/2007 kinachomtaka aitikie wito anapoitwa kuhojiwa! Akisubiri aje akamatwe kwa kukataa kuitikia wito asifikiri kwamba ndio karata ya kisiasa ya kupanda chati, asome alama za nyakati, haziko upande wake kwa sasa!

6. Kwa maelezo hayo machache hapo juu, bado sijaelewa upambanaji wa Dkt Mwakyembe na wenzake katika vita dhidi ya ufisadi ambayo inapiganwa bila kuwafahamu kwa majina mafisadi wenyewe!
 
HAPA ndipo Watanzania tunapo onyesha UMBUMBUMBU. TAKUKURU siyo HOSEA, hapana TAKUKURU ni Taasisi ITAENDELEA KUFANYA KAZI KAMA Taasisi na siyo kama HOSEA. Kwa Hosea kutaka kuhojiwa na Wabunge kuhusu RICHMOND hakuizuwii TAKUKURU kuendelea kutekeleza majuku yake ndugu yangu tambua hilo. TAKUKURU siyo Mke wa HOSEA kusema kwamba akikamatwa HOSEA basi TAKUKURU isendelee kufanya kazi sababu Bwana wao kakamatwa HAPANA.
Suala la TAKUKURU kuona leo ndiyo wakati muafaka wa kuwahoji Wabunge. elewa kwamba suala lolote la kisheria linahitaji TAFAKURI ya kina ili kuweza kulichukua. TAKUKURU imefanya uchunguzi na imejirisha kwamba, kuna hoja za kuwauliza Waheshimiwa kwamba kuna suala hili la wao kupokea posho za KUJIKIMU MARA MBILI KWA TAREHE ZILE ZILE sasa ni kazi ya WABUNGE kusema kwamba oooooooooooooooeeeeeeeeeeeeeeeeeeuuuuuuuuuuuuuuuu n.k

Halafu hivi wabunge hao kusema sema kuhusu UFISADI ni TIKETI YA WAO KUWA JUU YA SHERIA ETI??? KWA NINI BADO UMELALA.
Nakubaliana na wewe mkuu, TAKUKURU wanatekeleza majukumu ya kazi, wabunge wanatapatapa tu au ndio mambo ya mkuki kwa nguruwe......?
 
Nilimsikia Mwakyembe jana akilalama kwamba vijana wanaowahoji WABUNGE wetu ni "very junior". Alitaka wahojiwe na nani kwa mambo ya kijinga kama haya kupokea posho mara mbilimbili. Ninachofahamu mimi ni kwamba PCCB ni moja ya taasisi za UMMA zinazoajiri vijana wasomi wazuri sana.
 
Mwaga vitu, tujifunze sheria. tuwekee attachment ya katiba maana huku kwetu hatujawahi kuiona
 
Nilimsikia Mwakyembe jana akilalama kwamba vijana wanaowahoji WABUNGE wetu ni "very junior". Alitaka wahojiwe na nani kwa mambo ya kijinga kama haya kupokea posho mara mbilimbili. Ninachofahamu mimi ni kwamba PCCB ni moja ya taasisi za UMMA zinazoajiri vijana wasomi wazuri sana.

ilinikera sana hii jana nilipoangalia kwenye tivii yaani ni arrogance ya kifala sana, wewe unategemea makosa kama ya kula posho mara mbili uhojiwe na nani sasa? mijitu mingine sifa sana, huyu jamaa sijui hata hiyo pihechidii yake aliipata vipi..very low of him aaaaghrrrrr.
 
Hii nadhani sasa inamrudia na ni matokeo ya ile ripoti alosoma na alivyoendelea kujigamba. Lakini si kwamba yeye ndo mwenye makosa yanayotupeleka hapa tulipo.
takukuru kwani imeundwa jana au juzi, imeibua mangapi? na hata kutetea mangapi?
Au ndo kwa vile hawa wamewaandama ndo wanafanya debate! Hii nchi imekwisha Kabisa.
Waziri Mkuu naye anasema hili ni agizo Kutoka ikulu, HIVI IKULU SI NDO ILIMTEUA hOSEA na alistahihili kuwajibishwa!, Mbona wanababaika kusema lolote kuhusu hilo hadi mda wa bunge kusikiliza maamuzi ya serikali umefika, serikali haijaamua, eti itafanya hivyo ikifika Bngeni, Matokeo tunayoyasikia ni wabunge kuhojiwa na huyuhuyu mtuhumiwa wa ufisadi ambaye bado Jibu halijapatikana.
nadhani itatubidi maranyingine tuangalie tusiwe wamezaji wa mambo yote kwa pupa- Tutatapika. waamue moja maana hili nalo si la leo ni la siku nyingi.
Mimi nashauri tusishabikie sana maana hii serikali yetu sasa haina utofauti na KOMEDI
TUSIDANGANYIKE!!
 
Buchanan,

hivi umeshawahi kufanya kazi Serikalini? Mbona mambo ya kupokea mgao mara mbili kwa kazi moja wakati wa warsha, semina, kongamano, mikutano, mafunzo kazini, ziara n.k ni mambo ya kawaida sana.

kama kuna tatizo katika hili basi takukuru ilipaswa kuchukua hatua kuanzia zamani zile, vinginevyo kuna kila dalili ya kutaka kukomoana katika hili.

Ndo mambo yaleyale, ukininyima jua, mimi nakunyima mvua.
 
Back
Top Bottom