Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Mezeni nyembe mnaomchukia Dr Mwakyembe H, hatuna cha kuwasaidia ....anajua anachokifanya heko Harrison! Mafisadi na mapandikizi wao nafasi yao inazidi kuwa finyu kila mtego wao utawanasa wao wenyewe.


wewe ndiye umeze nyembe.kabanwa sasa shoga yako na umma umeanza kuamini kuwa kumbe na yeye ni fisadi na phd yake aiendani na ujinga alionao
 
Kuna tatizo kubwa kwenye hili gazeti na tayari limeshapoteza mwelekeo kwa sababu ya uswahiba wa wahariri na mafisadi. Hivi vichwa vya habari huwa wanaelekezwa kutoka MONDULI au IGUNGA. Si mnajua agenda ya hawa mafisadi! BURIANI Tanzania Daima! Tuliwapenda, lakini mafisadi waliwapenda zaidi...
 
Masanilo aka Ze Comedy,
Wewe beba tu mabox ya Wazungu huko Majuu; unashangaa hilo mbona hushangai mtu kuchukua posho mbili na bado akajiona hajakosea?

Wewe lipwa mara mbili kwenye hizo boksi zako tuone kama hutatupwa mpaka huko kwenu Mwanza.

Engineer,
Masanilo kashaachana na Wazungu. Yuko mbioni kugombea ubunge huko kwao Mwanza kwa sasa. Ila na yeye mpinzani wake ni mtu wa Mtandao na kwa hilo kwa kweli ana kazi ngumu sana.

Masa, vipi sasa wale Sato uliniahidi utatuma? Acha hiyo bwana. Au ndiyo mikiki ya uchaguzi imeshaanza? Kaza uzi basi maana uchaguzi si mchezo.
 
Hii kitu safi sana. Hatimaye Tanzania kuna JOTO kwenye level kubwa.

Hivi, kama kweli Wabunge ni Watakatifu na Mawaziri/Rais na wao hupokea posho mara mbili, kwa nini wasilivalie njuga mbungeni na hii practical IPIGWE MARUFUKU? Atakayefanya iwe basi ashitakiwe kama mwizi. Hata Rais akienda vijijini basi afanye catering na au apeleke pesa sehemu atakayokula ili wamuandalie chakula/Pa kulala. Haya mambo ya wanapewa fedha halafu wakiwa ziarani wanapikiwa na kulala bure (sintashangaa wengine wakienda kulala shule za wasichana kama Marehemu Mgonja).

Hii kitu ILITAKIWA sasa bunge liseme STOP. Ila, tangu hii kitu isemwe kwenye ile kesi ya Makamu wa rais, hadi leo ziii. Sasa unakuta hata Sitta analalamika, jamani. Mwakyembe na serikali kwa ujumla na kama sikosei hata Rais, wote wanamuogopa HOSEA maana nafikiri huyu jamaa anakuwa na siri nyingi sana za kwao. Ila uchaguzi mwakani, kuna watu wanataka kujitupa. Ni kama ile safari ya wanyama kutoka Kenya kuja Tanzania. Wakifika kwenye mto, inabidi kujirusha tu na humo ndani kuna mamba kibao. Wengine watafanikiwa na wengine wataliwa. Wabunge ni au wamuache Hosea na waanguke kwenye uchaguzi (hasa timu ya Mwakyembe) au waamuwe KUFA NAYE. Kwa sasa hivi watakuwa wamechelewa sana na hasa Mwakyembe ambaye kama kweli alichukua pesa eti anaenda kutibiwa German na kumbe kalala Kunduchi, basi heri yeye ANYAMAZE KABISA na atangaze tu mwakani hagombei tena ubunge......... HUWEZI KUWATUMIKIA MABWANA WAWILI.
 
Kuna tatizo kubwa kwenye hili gazeti na tayari limeshapoteza mwelekeo kwa sababu ya uswahiba wa wahariri na mafisadi. Hivi vichwa vya habari huwa wanaelekezwa kutoka MONDULI au IGUNGA. Si mnajua agenda ya hawa mafisadi! BURIANI Tanzania Daima! Tuliwapenda, lakini mafisadi waliwapenda zaidi...
Hii inatuonyesha dhahiri kwamba sio kila kinachopitiwa na editor in material. Wakatimwingine kuna agenda zao au hata ulevi tu wa kifisadi. Kuna siku nilisoma kuhusu tikio ambalo mimi nilikuwepo. Kilicho ripotiwa baadae klikuwa tofauti kwa kila reporter. Ukisoma katikati ta mstari utaona kuwa wanaunganisha "values" zao na habari. Kama vile tunavyoweza kucheza na data.....ukitata number ziseme JF ni mbaya unaweza tena bila shida
 
Umesema sawa kabisaaa! Mawaziri na viongozi wengine kupokea mshiko mara mbili wala si la ajabu! Lakini cha kushangaza ni timing ya Takukuru! Na jinsi walivyotilia "UMUHIMU" kumbe hata wao waliwapa huo mshko huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria?? Mbona contradiction??
 
Hivi wabunge wangine wote waliojiwa au kuna ambao walikataa kuojiwa kamwa mwakyembe?
 
Hii ya Ujerumani nasikia ni kweli,Mwakyembe alichukua pesa na wala hakusafiri kwenda uko Ujerumani,yeye ukimwuliza anasema watanifanya nini,kwani kati yenu nani anajua sheria kunizidi mimi....

HIYO HELA ALIYOLIPA INALINGANA NA KAGODA, RICHMOND AU EPA? Tukifatilia vi kashfa mnavyotoa hakuna serikalini atakayepona.

HAPA TUNAJADILI ZAIDI MAHELA MAKUBWA.

Na haya yote yanakuja leo why?
 
Wakatae wana ubavu? Si unajua wabongo? Badala ya kuwasiliana na wanasheria (WAO), wakajiendea TAKUKURU kwa uoga wa kishamba!
 
Umesema sawa kabisaaa! Mawaziri na viongozi wengine kupokea mshiko mara mbili wala si la ajabu! Lakini cha kushangaza ni timing ya Takukuru! Na jinsi walivyotilia "UMUHIMU" kumbe hata wao waliwapa huo mshko huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria?? Mbona contradiction??


viongozi wangapi ni board members wa mashirika na wanalipwa salaries sehemu moja na wakienda vikao vya board wanalamba mshiko. Uchunguzi wa hili ulitakiwa uanze kwa mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wa serikali uone kama kuna watakaopona.

Hili la kina mwakyembe linafanya purposely kwa malengo fulani ila kama wameshituka vile. Ukifatilia vizuri zaidi ya wabunge asilimia sabini wataguswa na ukifuatilia huko nyuma hata pm na president wakiwa mawaziri watakuwa walilamba.
 
HIYO HELA ALIYOLIPA INALINGANA NA KAGODA, RICHMOND AU EPA? Tukifatilia vi kashfa mnavyotoa hakuna serikalini atakayepona.

HAPA TUNAJADILI ZAIDI MAHELA MAKUBWA.

Na haya yote yanakuja leo why?

Shangazi,
Kitu chochote very complicated, huanza kidogo kidogo. Umeshaambiwa na PINDA kuwa ukichokoza huko nchi italipuka. Sasa basi kwa kuanzia na hivi visenti, tutafika hadi kwa akina KAGODA. Wabunge kama Dr. Slaa sasa ndiyo muda wao wa kuanza kutesa Tanzania. Kama Hosea akiwakamata wala posho mara mbili, wabunge na wao watamkalia koo Hosea na kufumua madudu yao. Na yeye atasema sifi peke yangu ..... hadi mwisho tunawakuta wazee wa Deepgrean, KAGODA nk. Sasa unafikiri kama KAGODA ilichota hela na hizo hela Wabunge woote wa CCM walipewa 5M, mwaka 2005, unategemea leo CCM watasema kitu kuhusu KAGODA? Ila Hosea kwa sababu ni mfa maji, atarusha kila konde ili wamuache.

Wengine waliondoka madarakani kasoro Chenge (mwana sheria mkuu) na Hosea. Hawa Ngosha unaweza kusema ndiyo kama wameshika nchi. Mtu hawezi kuwafanya chochote. Wao wameshika MPINI na Serikali/bunge limeshika makali. Wakijifanya wajanja, Ngosha wanavuta mpini kidogo tu, watu huku ni kilio. Sasa wee Mbunge kama Mwakyembe kulialia kwa wananchi kweli ili uonewe huruma, MHHHH!!!!!!!!
 
Hivi wabunge wangine wote waliojiwa au kuna ambao walikataa kuojiwa kamwa mwakyembe?

Inaonyesha ni huyu huyu Mwakyembe tu. Namwita hivyo maana nimeondoa ile title ya Dr. maana haimfai na hastahili. Anasema maneno kama mtu hakwenda shule!!!

Hivi Takukuru kwanini haitoi WARRANT OF ARREST kama anakataa kuhojiwa. Hapo ndio atakoma ubishi. Lazima wale nae sahani moja mapaka aache ufisadi.
 
Kuna tatizo kubwa kwenye hili gazeti na tayari limeshapoteza mwelekeo kwa sababu ya uswahiba wa wahariri na mafisadi. Hivi vichwa vya habari huwa wanaelekezwa kutoka MONDULI au IGUNGA. Si mnajua agenda ya hawa mafisadi! BURIANI Tanzania Daima! Tuliwapenda, lakini mafisadi waliwapenda zaidi...


Mkuu Mzee Punch hiyo imeniacha hoi, "Maelekezo toka Monduli na Igunga"

Uchaguzi wa 2005 nakumbuka hiki kijarida kilikuwa mstari wa mbele kweli kweli kushabikia Mafisadi. Hakika mafisadi wanapambana. Huyu mmiliki wa hili gazeti hajayaona haya au ndo na yeye ni mrengo uleule wa kifisadi?
 
Kumbe ufisadi una mipaka? Mamilioni yaliyoenda kwa wabunge kwa njia ya "double payment" kwa kazi ile ile kumbe sio ufisadi? Kweli vita dhidi ya ufisadi haina mwenyewe kwa Tanzania!
 
Hosea ni FISADI.

Wabunge ni MAFISADI (waliopokea Posho).

Hivi Dr. Slaa pia alipokea? Maana wangelikuwa wameshambeba siku nyingi na kumrunda Keko.

Acha wazichape, siri nyingi ya ULAJI zitafumuka. Waandishi wa habari nao wanakomba..

Kumbe hii Tanzania nchi TAJIRI saana.

Simuonei huruma Hosea na Mwakyembe. Acha waburuzane tu na Mungu bariki wote wapakana MAJI TAKA.
 
ukitaka kujua ilikua mchezo wa mafisadi dhidi ya Dr Harrison Mwakyembe angalia tu habari ilivyopokelewa na machapisho ya pale Kijiweni, Sinza. walijuaje hizo habari kama si Hosea kuwajulisha kua Dr Mwakyembe aligoma kuhojiwa na TAKUKURU.
Katuika ujumla wake TAKUKURU ilipaswa kuanza na Mawaziri, maana hakuna hata mmoja ambae hajawahi kupokea posho mbilimbili, wala haiitaji uchunguzi.
Serikali kuu inawalipa Per diem, kisha wanalipwa posho za kuishi huko bungeni Dodoma, aende Mawizarani akaulize kama kuna waziri hajalipwa posho yakujikimu akiwa Dodoma, kisha akamuulize Muhasibu wa Bunge kama hawajalipa posho nyingine kwa mawaziri hao wakiwa DODOMA.

Lakini huwezi jua kama Hosea hajawaita mawaziri na watu wengine. Takukuru ufanya kazi yao kimya kimya. Kwa mtizamo wangu hata PCCB kama walikuwa na hila ndani yao kumwita Mwakyembe kuhojiwa angeitikia na kwaonyesha kwamba ni wapuuzi hilo lingekwa na mantiki zaidi. Hata kama ana haki ya kukataa kuhojiwa angekwenda tu and it would have made PCCB very look radiculous. In this particular case it is more of bravado than being level headed on the part of honourable MP.
 
mmh Nyie ongeeni yooote but Mwakyembe yupo juu na aendeleee hivyo,
acheni kumkatisha tamaa MAFISADI
 
Ambao hammjui Mwakyembe mtapata shida sana, jamaa ni mpambanaji kwa mambo anayopingana nayo lakini yeye mwenyewe ni fisadi mkubwa kwenye mambo mengine ambayo anafaidika nayo.

Kuna kashfa nyingine inakuja ambayo kwa msaada wa spika Sitta kalipwa mamilioni ya pesa kwa kusingizia kwamba alienda kutibiwa nje (Ujerumani) wakati ule baada ya ajali wakati alikuwa amejifungia nyumbani kwake Kunduchi.

Nchi hii inaliwa na hao hao wanaojifanya wanailinda.

Hivi habari hii ni kweli. Hebu toa details zaidi ili Takukuru, CAG na Cheyo wafuatalie. Unajua pengine hawa jamaa huwa hawasomi JF. Inabidi wapewe hizo details through other means.

Kwa hali ilivyo mimi sioni ajabu kwa hili maana wote Sitta na Mwakyembe kwa vipimo vyote ni mafisadi.
 
Hivi habari hii ni kweli. Hebu toa details zaidi ili Takukuru, CAG na Cheyo wafuatalie. Unajua pengine hawa jamaa huwa hawasomi JF. Inabidi wapewe hizo details through other means.

Kwa hali ilivyo mimi sioni ajabu kwa hili maana wote Sitta na Mwakyembe kwa vipimo vyote ni mafisadi.


Nyie ndo mafisadi bwana jamaa wako safi!!
yaani mnataka kusema hii nchi hakuna watu walio safi nyie mnachochea ufisadi zaidi! na mnataka dhambi zenu zionekana mpo wengi. No kama ni dhambi mpo nyie tuu na wahindi waliokamata uchumi wa nchi na mnadanganyika nao!!!
 
Back
Top Bottom