Kwani kuna mtu kakataa wabunge wasihojiwe? hata JK wamhoji lakini wafate sheria na sheria ni msumeno hauchagui Huyu Richmond, EPA,Mwakyembe.... Mi naona TAKUKURU isafishe kwanza ndiyo waanze kuhoji watu maana ni wachafu wachafu..BENDERA KUFUATA UPEPO.
Mezeni nyembe mnaomchukia Dr Mwakyembe H, hatuna cha kuwasaidia ....anajua anachokifanya heko Harrison! Mafisadi na mapandikizi wao nafasi yao inazidi kuwa finyu kila mtego wao utawanasa wao wenyewe.
Jamani!!!!!!, TAKUKURU imeshindwa kuwaoji na kuwachukulia hatua stahili mafisadi sasa inawaoji wabuge? Naona hii ni mbinu ya mafisadi kuwaziba midomowabunge wanao piga vita ufisaidi nchini. Mbaya zaidi hawa wabuge wanadhalilishwa kwani watu wanaowaoji ni watu wa hali/nafasi ya chinikulingana na nafasi walizo nazo wabunge.
Masa...Huyo jamaa yenu naona sasa ananza kuchanganyikiwa,Yaani yeye tu ndo hawezi kukosea?Sasa ndo nimeelewa nani anayeleta ugomvi kule kwetu.
Kuna kashfa nyingine inakuja ambayo kwa msaada wa spika Sitta kalipwa mamilioni ya pesa kwa kusingizia kwamba alienda kutibiwa nje (Ujerumani) wakati ule baada ya ajali wakati alikuwa amejifungia nyumbani kwake Kunduchi.
Nchi hii inaliwa na hao hao wanaojifanya wanailinda.
Ambao hammjui Mwakyembe mtapata shida sana, jamaa ni mpambanaji kwa mambo anayopingana nayo lakini yeye mwenyewe ni fisadi mkubwa kwenye mambo mengine ambayo anafaidika nayo.
Kuna kashfa nyingine inakuja ambayo kwa msaada wa spika Sitta kalipwa mamilioni ya pesa kwa kusingizia kwamba alienda kutibiwa nje (Ujerumani) wakati ule baada ya ajali wakati alikuwa amejifungia nyumbani kwake Kunduchi.
Nchi hii inaliwa na hao hao wanaojifanya wanailinda.
Hii ya Ujerumani nasikia ni kweli,Mwakyembe alichukua pesa na wala hakusafiri kwenda uko Ujerumani,yeye ukimwuliza anasema watanifanya nini,kwani kati yenu nani anajua sheria kunizidi mimi....
Kutokana na kutojua sheria na kanuni za kazi zao matokeo yake ndio hayo yanayotokea sasa ..Tukukuru hawakuwa na sababu ya kuwapigia simu na kuwahoji waheshimiwa moja kwa moja kwa njia ya simu tena kwa muda wa zaidi ya masaa mawili,
Hata kama kile wanachokihoji ni ni wajibu wao. Ni uzembe wa hali yajuu. Hata kama ni mimi nisingekubali just kupokea simu kisha kuhojiwa kama mtoto mdogo kwenye mambo kama hayo ya kuchunguzana....Hapo ni kutafutana shida tu kwamba watu wana kidharau hiki chombo.. Si kweli ..Tukukuru wanajidharaulisha wenyewe.
Tena hii Tukukuru ni yakufungwa kwani pia wanapokea mishahara ya bure na humo humo wapo wale wenye kutajwa tajwa kwenye kashfa za Richmond.
kama ni vijana waliosoma sheria walishindwa nini kuanza na Richmond..Nasema Mwakyembe atakwenda kupambana na VIJANA wa TAKUKURU ambao nao wamesoma sheria na wanazifahamu Sheria.
Suala hapa siyo MTU KUWA MPAYUKAJI ili watu wakujue kwamba unajua VITU.
Unamkumbuka Dr. Masumbuko Lamwai- unakumbuka alivyokuwa anatesa na Sheria zake za Kidokta yuko wapi.