Nafikiri kuna mambo muhimu yanayohitajika kujadiliwa hapa siyo kutangaza biashara za watu hapa.
Management ya JF ina mipango gani kuwaalika watu kama hawa jamvini kwa manufaa ya wanamvi wengine? anaweza kuruhusu haki zake kama video kutumika hapa kuelemisha wengine ambayo wanayohitaji elimu zaidi.
Mie nashauri JF kuwa na utaratibu wa kuwapa mwaliko kutoa mada hapa kama wageni waalikwa, si lazima wawe memba.
Star Tv ina ofisi zake Dar, sio lazima aende Mwanza. Ni kweli ni ghali na kwa mwananchi wa kawaida ni vigumu kupata service zake. Kama mtumishi angetakiwa afanye matibabu asilia kwa bei nafuu, lakini ni ghali hata kuliko virutubisho vya GNLD n.k.
umeongea pwent. Huyu Dr. ni public speaker mzuri sana. Kwa wenzetu huko nje angekuwa mtu muhim sana. Na usemavyo kuhusu kujiunga humu lingekuwa jambo la busara. Labda yupo ila ni kwa vile hatujuani
Kwani cha ajabu yeye kuja na kuchangia ni nini? Kwani unadhani wanaochangia humu hawana bei? Si ni kujitolea tu na hata yeye mbona anaalikwa sehemu mbalimbali kama makanisani kuzungumza na halipwi?[/QUOTE]
Huko japo halipwi, huwa anatafuta wateja kama nyie hamfahamu hilo.
Binafsi nimekuwa mfuatiliaje wa Vipindi vya Dr Isaack Ndondi kuanzia vile Channel 10 mpaka StarTv. Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mambo ya msingi katika jamii ambayo uwepo wake kwenye screen kumewasaidia wengi. Vipindi vyote hivyo anavifanya kwa gharama zake mwenyewe, kwa hiyo hata gharama zake kimatibabu lazima ziwe juu. Laiti kama watanzania wasingeendelea kuifanya mioyo kuwa migumu na kumsaidia huyu bwana kama basi angekuwa msaada mkubwa jamii
Binafsi huwa napata burudani saaaaafi napokuwa naangalia kipindi chake. Ni zaidi ya comedy . Pamoja na kujaliwa kipaji cha kuongea haraka haraka, pia huwa anajaribu kutumia lugha ambayo inaweza kueleweke kwa kila mtu.
hapo umenenna ni Ze KOMEDI !, hasa kwa wanaoweza kuchambua na kuchagua yanayofaa, kumbuka watanzania walio wengi wanachukua na kuamini yote anayoyasema Ndodi.
Ni ujinga kwa kila mganga wa kienyeji kujiingiza katika mambo ya kiuchungaji ili watu wawakubali!Alianza Yahaya Hussein,akaja Ndodi sasa Joseph Kalokola Buberwa wa JKB international nae eti anatoa neno la mungu!Acheni kukufuru mungu kwa kutaka ufalme wa hapa duniani.Kalokola mke kamshinda na wametengana kwa kupigana magumi pale ubungo plaza mimi pamoja na wafanyakazi wake akina Vick,Mrutu na Ndutu ndio tulioamulia hizo ngumi leo nae anafundisha watu jinsi ya kuishi katika ndoa!Aibu.Hawa ni wafanyabiashara tuu wala hawatendi mambo ya mungu,achaneni nao.
Huyo bwana kwa wasiomfahamu utamuona ni mujuzi. Lakini kwa taarifa huyo bwana hajasomea taaluma ya utabibu. Ukifuatilia mada zake utagundua kuwa anaongea mambo ambayo hana ujuzi nayo. Kwa taarifa halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilimpiga marufuku kuendesha Kliniki yake iliyokuwa magomeni Kagera na kumpiga marufuku kuendesha biashara ya Kliniki eneo lolote la Manispaa hiyo kwa sababu nilizozitaja hapo awali.
Jamani kuweni makini na watu kama hawa ambao wanajiita "Doctor" Wakati hawakuusomea hata hiyo kozi ya 'Rural Medical Aid' nako hawakupita.
Kwa hiyo suala si kujua kuongea au kuwa na ushawishi; Suala hapa je ana taaluma inayotambulika? au ni comedian!!!!!!!
hapo umenenna ni Ze KOMEDI !, hasa kwa wanaoweza kuchambua na kuchagua yanayofaa, kumbuka watanzania walio wengi wanachukua na kuamini yote anayoyasema Ndodi.
Huyu bwana anajiita Dr, hakuna lolote. Ufahamu wake wa kutibu maradhi mbalimbali kwa kutumia lishe, kwa mfano mtu ana matatizo ya macho anamwambia kula sana matunda na mboga za majani, hakikisha mboga huzichemshi sana na kama una mafuta ya mawese weka. Jamani ni daktari gani wa muhimbili au hospital yoyote asiyejua umuhimu wa matunda na mboga za majani? Nakumbuka hata shule za msingi wanafundishwa haya. Sasa unatwambia tulipe Tshs. 50,000 kumuona huyu bwana!!! Wizi mtupu.
Mimi nimemuona mara nyingi kupitia star TV na channel ten, sijaona ujuzi wake zaidi ya kuchomoa pesa za watanzania. Nilikuwa nataraji kama wanavyofanya wachungaji wengine kama kakobe, mzee wa upako n.k atowe huduma hiyo bure kwa kondoo wa bwana.