Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,847
2,669
Nadhani wadau wengi humu mtakuwa mmeshamsikia au kumwona huyu bwana machachari ambaye ni dokta, mchungaji, mshauri, mwalimu, n.k. binafsi napenda kumsikiliza kila wakati anapotoa mada hasa ukichangia na ile spidi yake ya kuongea bila kukosea. tatizo lake ni mtu ghali sana linapokuja suala la matibabu. zaidi ya kumwona kwenye kioo, kuna ya ziada juu yake? tumzungumzie kwa wema tu kwani ni mtume yule
 
Huyu Dokta/Mchungaji tena kijana ni mfano wa kuigwa.Napenda vipindi vyake vya redio na TV kwa maana anazungumzia mambo ya maisha ya kawaida kabisa.Kipindi chake cha juzi Jumatano kuhusu namna ya kuchagua mchumba kwa vijana wa kike na kiume kilinivutia sana.Laiti angejiunga hapa akaweza kuchangia hizi mada kwenye jukwaa la mahusiano na JF Dr.
 
umeongea pwent. Huyu Dr. ni public speaker mzuri sana. Kwa wenzetu huko nje angekuwa mtu muhim sana. Na usemavyo kuhusu kujiunga humu lingekuwa jambo la busara. Labda yupo ila ni kwa vile hatujuani
 
Laiti angejiunga hapa akaweza kuchangia hizi mada kwenye jukwaa la mahusiano na JF Dr.

weeeeeeeeeeeeeeee bili yake atalia nani?????????
 
Kwani cha ajabu yeye kuja na kuchangia ni nini? Kwani unadhani wanaochangia humu hawana bei? Si ni kujitolea tu na hata yeye mbona anaalikwa sehemu mbalimbali kama makanisani kuzungumza na halipwi?
 
Ila kwa anavyosema wachumba watazamane na kuongea tu bila kujiexpres kwa karne hizi ni ngumu
 
Ni ujinga kwa kila mganga wa kienyeji kujiingiza katika mambo ya kiuchungaji ili watu wawakubali!Alianza Yahaya Hussein,akaja Ndodi sasa Joseph Kalokola Buberwa wa JKB international nae eti anatoa neno la mungu!Acheni kukufuru mungu kwa kutaka ufalme wa hapa duniani.Kalokola mke kamshinda na wametengana kwa kupigana magumi pale ubungo plaza mimi pamoja na wafanyakazi wake akina Vick,Mrutu na Ndutu ndio tulioamulia hizo ngumi leo nae anafundisha watu jinsi ya kuishi katika ndoa!Aibu.Hawa ni wafanyabiashara tuu wala hawatendi mambo ya mungu,achaneni nao.
 
Hawa watu wana akili sana.Wanajua kuwa kwa hali iliyopo sasa watu wanahitaji msaada kutokana na shida zao mbali mbali.Sasa situation inapokuwa hivyo wanawamanipulate wenye shida zao kutokana na mvuto wao wa kulonga.End of the day wanaliwa hela zao na hakuna lolote la maana.
 
Laiti angejiunga hapa akaweza kuchangia hizi mada kwenye jukwaa la mahusiano na JF Dr.

weeeeeeeeeeeeeeee bili yake atalipa nani?????????
Unajua Dr Ndodi ni wa gharama kwa sababu vipindi vyake vinavyo rushwa kwenye runinga na radio anavilipia mwenyewe.Na kila week nilazima apande ndege kwenda mwanza kufanya kipindi.Unategemea hizo pesa anatoa wapi kama sio kucharge wateja wake kiasi kikubwa cha pesa ili aweze kuendelea kutuelimisha kupitia vyombo vya habari?
 
Ni ujinga kwa kila mganga wa kienyeji kujiingiza katika mambo ya kiuchungaji ili watu wawakubali!Alianza Yahaya Hussein,akaja Ndodi sasa Joseph Kalokola Buberwa wa JKB international nae eti anatoa neno la mungu!Acheni kukufuru mungu kwa kutaka ufalme wa hapa duniani.Kalokola mke kamshinda na wametengana kwa kupigana magumi pale ubungo plaza mimi pamoja na wafanyakazi wake akina Vick,Mrutu na Ndutu ndio tulioamulia hizo ngumi leo nae anafundisha watu jinsi ya kuishi katika ndoa!Aibu.Hawa ni wafanyabiashara tuu wala hawatendi mambo ya mungu,achaneni nao.

mkuu umenena. Hata mi nashangaa ni lini buberwa kawa mchungaji. Hii inamaanisha dini ina influence sana ktk kutimiza mambo flani. Ndodi nae asiwe kwenye mkumbo huo. Tofauti zao ni bei za dawa zao. Ndodi ni ghali mno. Sijajua kama zinatibu kiukweli
 
Hizo trip ni za kujitangaza zaidi. Wanaomwalika wangemchangia kidogo ili gharama zipungue. Kuhusu kumanipulate mawazo ya watu ni kweli kabisa. Wabongo tuna matatizo mengi ambapo ni fursa kwa wajanja kama hao.
 
inakuwaje mtu anakuwa ni Mchungaji na pia Mganga wa kienjeji? tiba zake nyingi si za kweli, mfn ndimu kutibu malaria!, wengi wamejaribu na kuishia na malaria kali wakaponea kwinini hospitalini, halafu bei zake ni aghali kuliko kwenda kutibiwa Apollo Hosp. INDIA, ila namkubali kuwa he is a good orator, which fits well with preaching the word of god.
 
unadhani hakuna tofauti kati ya tiba mbadala na uganga wa kienyeji? nadhani kabobea zaidi katika hizo tiba na ushauri zaidi ya uchungaji. huo uchungaji ni katika kujijengea imani kwa wateja. anasema ana tiba ya macho ili usivae miwani tena, ila inataka moyo! ni unga wa ndimu, unautia machoni. just imejin
 
Ni ujinga kwa kila mganga wa kienyeji kujiingiza katika mambo ya kiuchungaji ili watu wawakubali!Alianza Yahaya Hussein,akaja Ndodi sasa Joseph Kalokola Buberwa wa JKB international nae eti anatoa neno la mungu!Acheni kukufuru mungu kwa kutaka ufalme wa hapa duniani.Kalokola mke kamshinda na wametengana kwa kupigana magumi pale ubungo plaza mimi pamoja na wafanyakazi wake akina Vick,Mrutu na Ndutu ndio tulioamulia hizo ngumi leo nae anafundisha watu jinsi ya kuishi katika ndoa!Aibu.Hawa ni wafanyabiashara tuu wala hawatendi mambo ya mungu,achaneni nao.

acha majungu na umbea, halafu umetoka nje ya mada.
 
Binafsi nimekuwa mfuatiliaje wa Vipindi vya Dr Isaack Ndondi kuanzia vile Channel 10 mpaka StarTv. Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mambo ya msingi katika jamii ambayo uwepo wake kwenye screen kumewasaidia wengi. Vipindi vyote hivyo anavifanya kwa gharama zake mwenyewe, kwa hiyo hata gharama zake kimatibabu lazima ziwe juu. Laiti kama watanzania wasingeendelea kuifanya mioyo kuwa migumu na kumsaidia huyu bwana kama basi angekuwa msaada mkubwa jamii

Binafsi huwa napata burudani saaaaafi napokuwa naangalia kipindi chake. Ni zaidi ya comedy . Pamoja na kujaliwa kipaji cha kuongea haraka haraka, pia huwa anajaribu kutumia lugha ambayo inaweza kueleweke kwa kila mtu.
 
Binafsi nimekuwa mfuatiliaje wa Vipindi vya Dr Isaack Ndondi kuanzia vile Channel 10 mpaka StarTv. Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mambo ya msingi katika jamii ambayo uwepo wake kwenye screen kumewasaidia wengi. Vipindi vyote hivyo anavifanya kwa gharama zake mwenyewe, kwa hiyo hata gharama zake kimatibabu lazima ziwe juu. Laiti kama watanzania wasingeendelea kuifanya mioyo kuwa migumu na kumsaidia huyu bwana kama basi angekuwa msaada mkubwa jamii

Binafsi huwa napata burudani saaaaafi napokuwa naangalia kipindi chake. Ni zaidi ya comedy . Pamoja na kujaliwa kipaji cha kuongea haraka haraka, pia huwa anajaribu kutumia lugha ambayo inaweza kueleweke kwa kila mtu.[/QUOTE]

umesema pwent. alienda mabibo hostel kutoa mada zake za ujana na uchumba kuelekea ndoa siku ya ijumaa fulani then nadhani jumamosi yake yakatokea yale mauaji ya kinyama. watu hawamsikilizi. kuhusu kutumia lugha. angekuwa muwazi kiivyo ingekuwa balaa hasa kwa watoto. mwenyewe huwa anasema hutumia tafsida hasa yanapokuja mambo ya kiutu uzima. "unamlamba chenga golikipa hadi anakuwa hoi kisha unafunga bao lako saaafi!"
 
Wakuu naomba muone angalizo hapa chini.

tumzungumzie kwa wema tu kwani ni mtume yule

Inatakiwa tumzungumzie kwa wema!!!!!

inakuwaje mtu anakuwa ni Mchungaji na pia Mganga wa kienjeji? tiba zake nyingi si za kweli, mfn ndimu kutibu malaria!, wengi wamejaribu na kuishia na malaria kali wakaponea kwinini hospitalini, halafu bei zake ni aghali

umesema pwent. alienda mabibo hostel kutoa mada zake za ujana na uchumba kuelekea ndoa siku ya ijumaa fulani then nadhani jumamosi yake yakatokea yale mauaji ya kinyama. watu hawamsikilizi. kuhusu kutumia lugha. angekuwa muwazi kiivyo ingekuwa balaa hasa kwa watoto. mwenyewe huwa anasema hutumia tafsida hasa yanapokuja mambo ya kiutu uzima. "unamlamba chenga golikipa hadi anakuwa hoi kisha unafunga bao lako saaafi!"

Huyu ni mfanyabiashara - sishangai mbinu anazotumia

Utaona moja kwa moja sina nafasi ya kuchangi wema juu ya mtu huyu. Naomba upanue wigo ya mada hii ili tuweze toa mabaya pia.
 
Wakuu naomba muone angalizo hapa chini.

Inatakiwa tumzungumzie kwa wema!!!!!

Utaona moja kwa moja sina nafasi ya kuchangi wema juu ya mtu huyu. Naomba upanue wigo ya mada hii ili tuweze toa mabaya pia.

mkuu uwanja ni wenu kwani tunataka kufundishana hapa. yawezekana kuna kundi flani linavaa ngozi ya kondoo nasi tukaamini katika ukondoo wao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom