Dr. Hussein Mwinyi kugombea Urais wa Tanzania 2015?

TITAN

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
308
47
Kumekuwa na mkakati mkubwa na vikao vya siri sana vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM bara na CCM Zanzibar vikiongozwa na watu wanaosemekana kutumwa na Kikwete kwa ajili ya kumuandaa Dk. Hussein Mwinyi kuwa mrithi wa kiti cha Urais 2015.

Hii inatokana na madai ya 'kutaka kuunusuru Muungano' pamoja na 'kukilinda chama'.

Nina ushaidi wa kutosha kutoka kwa mmoja ya walioshiriki vikao vitatu vilivyotangulia. Wamepanga kikao kingine kufanyika May 05, 2011 mkoani Tanga na kutakuwa na shuguli ya kiserikali ambayo itakuwa inafyika kwa geresha ili waweze kukutana.

Wanajamii, mnaonaje ilo tutaweza kumkabili huyu kijana?
 
... my foot, akamalizane kwanza na Watanzania wenzetu waliochinjwa kinyama kule Gongolamboto bila huruma!!!
 
... my foot, akamalizane kwanza na Watanzania wenzetu waliochinjwa kinyama kule Gongolamboto bila huruma!!!

Hawa waaache usultani, kwani lazima awe yeye, mbona kama ni wa Zenji wako wengi? Ili mwinyi akipiga miaka yake kumi 1RIZ aingie naye? Hii ndio Tanzania kweli.
 
Jamani hebu musiigeuze hii kuwa uzushiforum!

Kuna mengi yatatokea baina ya sasa na 2015 Mungu atuweke hai tuyaone. Musianze kuzushia watu sasa hivi.
 
itakuwa sinema kwelikweli.Ina maana katika watanzania mamilioni kadhaa, hizi familia peke yake tu ndio zinaweza kuongoza na kukaa IKULU?
Sitaki kuamini huu uzushi.

Kwa taarifa rais ajaye hatatoka kwenye "UKOO WA KIFALME" -
 
Mbona hamuelewi? baada ya huyo ni RIZ>>>>>>>>>>>>>>ONE! Libya oyee, Misri oyee.
 
Na miye nitaanzisha chama changu,halafu nitagombea Urais.Naamini naweza kukubalika vizuri kwa Watanzania kuliko Hussein Mwinyi na kama hakutakuwa na uchakachuaji,nitazama magogoni kiulaiiini!!
 
wakuu kuna dalili kwamba hussein ali hassan mwinyi ndiye chaguo lijalo maana ndo zamu ya zanzibar. La sivyo tunavunja muungano
 
Yale yale kutuletea misukule,hana sifa wala uwezo wa kuongoza zaidi ya kuwa mtoto wa mwinyi,halafu why mgombea wa chichiem aka magamba ndio apigiwa chapuo la kuwa lazima ashinde?kwa shinikizo la kuvunja muungano kwa sababu ya urais utoke zenji mbona imekaa vizuri tu,maana sasa hata wakristo watadai zamu yao sasa kutoa rais,tushitishane ba ndugu
 
ajisafishe kwanza kashfa ya mabomu ya mbagala na gongo la mboto!!!hivi kwani nchi hii haina watu wengine?mpaka familia moja tu iwe inaongoza mara 2!mie nadhani iwekwe sheria kama baba alishika mtoto wake haruhusiwi sababu nchi hii sio ya kifalme haya mambo yanawezekana kule zanzibar tu kwa hapa bara hayatawezekana!
 
wakuu kuna dalili kwamba hussein ali hassan mwinyi ndiye chaguo lijalo maana ndo zamu ya zanzibar. La sivyo tunavunja muungano

Ninyi wana JF msipoangalia mtapoteza mwelekeo. Ni sawa kila mtu ana maoni na maono yake humu ndani lakini kuandika tu kwamba kuna dalili kuwa Mwinyi ndiye Rais ajaye na ni zamu ya Zanzibar vinginevyo tunavunja muungano, ndio iwe hoja. Mimi nilikuwa nadhani mtu akitoa hoja kama hiyo atoe sababu za maana na zenye mantiki. Kama kuna dalili azionyeshe ili watu tuchangie kwa weredi. Mtu unashindwa uchangie kuanzia wapi? Dalili ni zipi? Mtu anakuwa Rais wa nchi kwa dalili ama uwezo? Mtu anakuwa Rais wa nchi kwa zamu ama uwezo na kama ni hiyo zamu basi ni kwa nini awe mwinyi na wala siyo Maalim Seif, Juma Shamhuna, Balozi Seiffu idd, Nahodha ama hata Seif Khatibu? Mtoa mada angejaribu kutupatia dondoo hizo ili kuonyesha ni kwa nini Mwinyi na siyo kuanzisha thread tasa.
 
Hatutaki dalili tunataka ushahidi wacheni kufutinisha kama umetumwa umuharibie mtu hapa sipo tunaomba ushahidi, na ana haki pia kama mtanzania.
 
Sina hakika kama watafanya hivo. Lakin wacpo fanya hivo! Wazanzbr watanung'unika na mashekh hal kadhalka. Si chama kimewekeza huko kwa masheh na wazanzbar!! Fanya utafit. Unajua kwa nini mwenzangu!! Fuatilia matamsh ya mashehe, huwez kuta wanasema kamwe madhaifu ya chama tawala kamwe. Watacfia tu hata kama yako wazi. Saana watasema mkapa ndo kayaleta haya matatzo ya nchi.
 
Back
Top Bottom