Dr. Hussein Mwinyi kugombea Urais wa Tanzania 2015?

Ninyi wana JF msipoangalia mtapoteza mwelekeo. Ni sawa kila mtu ana maoni na maono yake humu ndani lakini kuandika tu kwamba kuna dalili kuwa Mwinyi ndiye Rais ajaye na ni zamu ya Zanzibar vinginevyo tunavunja muungano, ndio iwe hoja. Mimi nilikuwa nadhani mtu akitoa hoja kama hiyo atoe sababu za maana na zenye mantiki. Kama kuna dalili azionyeshe ili watu tuchangie kwa weredi. Mtu unashindwa uchangie kuanzia wapi? Dalili ni zipi? Mtu anakuwa Rais wa nchi kwa dalili ama uwezo? Mtu anakuwa Rais wa nchi kwa zamu ama uwezo na kama ni hiyo zamu basi ni kwa nini awe mwinyi na wala siyo Maalim Seif, Juma Shamhuna, Balozi Seiffu idd, Nahodha ama hata Seif Khatibu? Mtoa mada angejaribu kutupatia dondoo hizo ili kuonyesha ni kwa nini Mwinyi na siyo kuanzisha thread tasa.

Mweeee.....!!

JK sijui alikua na uwezo gani hadi wakampendekeza na kumchagua mweeee.....!
 
wakuu kuna dalili kwamba hussein ali hassan mwinyi ndiye chaguo lijalo maana ndo zamu ya zanzibar. La sivyo tunavunja muungano

Wewe kweli Mzanzibari, kwa mikwara mbuzi tu, nyinyi namba moja duniani, kuna siku nimeshudia zenji katoto ka kisukuma akimchapa Baunsa la Kizenji, baada ya mtoto kichimbiwa mkwara wa kizenji, akaamua poa auawe, kumbe kuguswa tu yakhheeee hata hajui apigane au ageuke, maskini bonge la mtu chini analia... tunawajua, bora msema kama watu wengine wenye akili.
 
Rais wa Tanzania anashughulikia mambo ya Tanganyika na ya Muungano, ya Zanzibar hayamhusu.

Rais wa Zanzibar anashughulikia mambo ya Zanzibar, ya Muungano hayamhusu.

Rais wa Tanzania akiwa Mzanzibar atashughulikia mambo ya Tanganyika ambayo hayamhusu, mimi Mtanganyika sikubali.



hata mawaziri wa zanzibar bara wanafanya nini? hawatupendi na wana nia wote ya kuvunja muungano, halafu tuwape tena vyeo watuongoze?
 
kama kutokumchagua hussein mwinyi au mzanzibari yeyote yule kuwa raisi wa muungano wa tanzania kutasababjsha muungano uvunjike ni bora iwe hivyo. Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi.
 
kwa cdm kushinda itabakia kuwa ndoto kubwa sana, chama kilisha poteza mwelekeo kama jana ulikuwa unamsikiliza katibu wako utakili alivokuwa akibabaika kujibu maswali ya muongoza kipindi, pale alizidi kujicholesha kwa wapiga kura

ccm oyeee!!! udini kwanza siasa baadae
 
Ninyi wana JF msipoangalia mtapoteza mwelekeo. Ni sawa kila mtu ana maoni na maono yake humu ndani lakini kuandika tu kwamba kuna dalili kuwa Mwinyi ndiye Rais ajaye na ni zamu ya Zanzibar vinginevyo tunavunja muungano, ndio iwe hoja. Mimi nilikuwa nadhani mtu akitoa hoja kama hiyo atoe sababu za maana na zenye mantiki. Kama kuna dalili azionyeshe ili watu tuchangie kwa weredi. Mtu unashindwa uchangie kuanzia wapi? Dalili ni zipi? Mtu anakuwa Rais wa nchi kwa dalili ama uwezo? Mtu anakuwa Rais wa nchi kwa zamu ama uwezo na kama ni hiyo zamu basi ni kwa nini awe mwinyi na wala siyo Maalim Seif, Juma Shamhuna, Balozi Seiffu idd, Nahodha ama hata Seif Khatibu? Mtoa mada angejaribu kutupatia dondoo hizo ili kuonyesha ni kwa nini Mwinyi na siyo kuanzisha thread tasa.

Sure, "Kimbunga"
Thread za namna hii ni kugeuza JF kama kijiwe cha majungu na watu wasio na kazi, huku ni kupotosha maana ya dhima ya "home of great thinkers".
Kama huna hoja ni bora utulie, usome hoja za wengine na utafakari ili uandike kitu chenye mashiko....
Hamna atakayekulalamikia mbona hujatuma thread.
 
Ndugu zangu waJF,

Miezi kadhaa iliyopita nilipost thread mbili humu jamvini zote zikimtabiria Mzee Mukama kuwa ndiye possible candidate wa kikwete kwenye kiti cha ukatibu mkuu wa ccm. Hatimaye utabiri huo ulitimia. Chanzo changu cha uhakika kutoka kwenye system kilinipa guts za kupost hizo threads.

Sasa naomba kwa mara nyingine na mwisho niwaambie jambo moja. Kama mtakumbuka miezi kadhaa imepita tangu vijana wa ccm mkoa wa pwani walipotoa tamko lao la kulaani wazee hususan mawaziri wakuu wastaafu wanaokikosoa chama na serikali yake. Katika laana hiyo walitamka jambo moja ambalo huenda wengi wetu hatukulitilia maanani na tukalipuuza japo Mzee Sumaye alilitolea kauli kwenye mwitikio wake kuhusu laana hiyo ya vijana.

Wale vijana waliwatuhumu wazee wastaafu kuwa wanautafuta urais na wakawaonya kuwa wasipoteze muda kuusaka urais kwani anayemjua rais ajaye ni kikwete peke yake. Katika fukuafukua yangu nimebaini kuwa wale vijana hawakuwa wajinga kama wengi wetu tulivyowapuuza. Walitumwa kuwavunja mioyo siyo wazee wastaafu tu bali na wengine wanaofikiria kutangaza nia kwa tiketi ya CCM.

Kwa taarifa yenu na naomba msipuuze hata kidogo, mgombea urais kwa tiketi ya CCM atakuwa ni mtoto wa mzee mwinyi anayefahamika kwa jina la Husein Mwinyi ambaye kwa sasa ni waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa. Kwa wanaoijua vema siasa ya nchi yetu, watahitaji dakika chache tu kujikumbusha mambo kadhaa kabla ya kuunga mkono utabiri huu.

Kazi kwetu wanaJF kumjadili huyo jamaa.
 
nashukuru kwa kutupa huu utabiri pia hongera kwa utabiri wako wa kwanza uliokamilika
 
Okay okay ingekuwa mkristo anachukua mara nyingine ungeona moto wake :smile-big::smile-big::smile-big:
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Okay okay ingekuwa mkristo anachukua mara nyingine ungeona moto wake :smile-big::smile-big::smile-big:

Hehehehehe MR huyu kijana hastahili kabisa kutokana na kushindwa kuwajibika katika yale mabomu ya mbagala na Gongo la Mboto. Hali hii inasikitisha kusema kweli uchaguzi uliopita ulikuwa miezi sita tu iliyopita lakini watu wameshaanza vurumai za uchaguzi wa 2015! Na wakati huo huo nchi inazidi kudidimia kiuchumi na Watanzania wengi kuelemewa sana na gharama kubwa za maisha. Walioshika utamu wako busy kujivua magamba na kumtafuta wa kurithi kiti cha mfalme 2015.
 
kimsingi nakubaliana na hilo ingawa historia ya kenya inaweza ikajitokeza hapa kwetu. moi aliamua kumpatia nafasi uhuru yaliyotokea kila mmoja anajua.
 
Sheikh Yahaya in tha making! Enheee mnajimu wangu tuambie na mwisho wa dunia ni lini?au wewe unatabiri ktk siasa tu?okey kma ni siasi tu tutabilie mkuu wa mkoa mpya wa dsm ni nani?
 
They murders, killers and mafisadi. Who will vote for these people if not by stealing votes?
 
Husseni ni zao la 'Agenda ya Siri ya Pwani' na mpango mzima wa kurithishani uongozi kifalme kwa watoto wa wakubwa.

Ni wazo na mkakati wa kuleta rais TX jambo ambalo si tu kwamba halitonunuliwa Visiwani bali zaidi ndicho kitu kitakacholeta ANTICLIMAX YA UTABIRI WA MWL NYERERE CCM vyama vingine zaidi kipindi kifupi kabla uchaguzi wa 2015. Na katika hili hata zile janja za kutumia GENDER kuleta dhana zamu ya akina mama na kuzuia demokrasia kama ilivyotokea kwa uspika wala haitosaidia sana.

Nadhani wagombea urais watarajiwa wengi wenye busara zaidi na macho wala hawatosubiri kuambiwa ona, huko ndani ya CCM.
 
Gosbert, awali ya yote nikupongeze kwa utabiri wako kuhusu mzee mukama. Inawezekana kweli una chanzo cha uhakika cha habari.

Kuhusu Husein Mwinyi, kwa umbali naanza kushawishika kwa sababu zifuatazo:-

(i) Mzee Mwinyi ambaye ni baba wa huyo candidate unayemtabiria ndiye aliyemuibua kikwete kutoka chini hadi hatimaye akafikia ngazi ya kujiona kuwa anafaa kuwa rais wa nchi hii. Kikwete mwenyewe amewahi kutamka kwenye moja ya hotuba zake kuwa isingekuwa ni Mzee Mwinyi asingekuwa kwenye ngazi aliyopo sasa. Kwa hiyo, kikwete lazima aonyeshe fadhira kwa Mzee Mwinyi kwa kumsafishia njia mwanawe awe top leader wa nchi hii. Isitoshe kwa kufanya hivyo, hata yeye mwenyewe kikwete atakuwa amejihakikishia ulinzi wa miaka mingine 10 ijayo.

(ii) Husein Mwinyi mwanzoni alikuwa mbunge wa Mkuranga. Lakini baadaye akaenda kugombea ubunge visiwani. That was a calculated move. Lengo lilikuwa ni kuidhihirishia jamii kuwa yeye ni Mzanzibar na kwa hiyo hata kama katiba haitamki kuwa marais wa Muungano lazima wabadilishane kutoka Bara na Visiwani lakini busara na hekima vinatuongoza kuamini kuwa mgombea wa urais ajaye kwa tiketi ya ccm atatoka Visiwani.

(iii) Serikali ya Zanzibar kwa sasa ni ya mseto kati ya ccm na cuf. Kwa ujumla, visiwani sasa ni kama hakuna upinzani kabisa. Kwa hyo endapo ccm itamteua mgombea urais kutoka Visiwani cuf wanaweza hata wasisimamishe mgombea wao wa kiti cha urais wa serikali ya muungano.

(iv) Japo tunakatazwa tusiseme lakini UDINI ulioletwa na mwenye kiti cha enzi inawezekana ulisanifiwa kwa malengo mahsusi yanayompatia faida zaidi mlengwa wake wa kiti hicho cha enzi.

Huo ndiyo mtazamo wangu na kwa hiyo naunga mkono utabiri wa Bw. Gosbert kwa asilimia 80.
 
Sheikh Yahaya in tha making! Enheee mnajimu wangu tuambie na mwisho wa dunia ni lini?au wewe unatabiri ktk siasa tu?okey kma ni siasi tu tutabilie mkuu wa mkoa mpya wa dsm ni nani?

Inawezekana ni wewe unayenekana mwehu manake wakuu wa mkoa wa Dar wengi wao huwa wanakuwa na tabia ya wehuwehu hivi.

Anachosema Gosbert ni utabiri lakini in a way siyo utabiri. Anajaribu kuangalia mazingira yaliyopo na ku-predict future kwa basis ambayo is more scientific than utabiri unaofanywa na kipenzi chako shekhe yahaya.
 
Back
Top Bottom