DOWANS, The End Justify The Means!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu Zangu,

Yafuatayo yalipata kutamkwa na Mh. Harrison Mwakyembe;

"MOJA ya sifa kuu za nchi za kipato cha kati ni kilimo cha kisasa na maendeleo ya kati ya viwanda, shughuli ambazo haziendi bila nishati ya kutosha na ya bei nafuu. Msingi wa kujenga uwezo wa kutosha wa nishati ili kuendesha viwanda, unatakiwa uanze kujengwa sasa na si baadaye.

Kamati Teule inakubaliana na ushauri uliotolewa na Kamati ya Uwekezaji na Biashara katika taarifa yake kwa Bunge kwa mwaka 2006 kuwa Serikali sasa iandae mpango madhubuti wa muda wa kati na muda mrefu ( power system master plan) ukionesha ni namna gani nchi itatekeleza na kukabiliana na tatizo la mfumo mzima wa uzalishaji na usambazaji wa umeme.

Mpango wa aina hii utaipunguzia Serikali gharama ya kuingia mikataba ya dharura mara kwa mara kila kukitokea ukame. Aidha mpango huo ujumuishe pamoja miradi kama ya Stieglers George ya kuzalisha umeme wa MW 2100 na zaidi, makaa ya mawe ya mchuchuma, umeme wa nishati ya gesi asilia, upepo, jua, taka n.k. Hapo tutakuwa tumejijengea msingi mzuri wa kupokea changamoto za maendeleo ya nchi za kipato cha kati"
( Ripoti ya Tume Teule ya Uchunguzi wa Richmond)

Hakika, hitimisho la ripoti ndefu ya Tume ya Mwakyembe limenifanya niumize kichwa kutaka kujua zaidi mbali ya mambo mengine, juu ya mradi wa Stieglers George ambao kama ungekamilika, ungekuwa na uwezo wa kuzalisha MW 2100 na zaidi. Kiasi hicho cha umeme kingetosha kwa mahitaji yetu ya ndani na hata kupatikana ziada ya kuuza nje.

01.jpg

Pichani ni picha ya juzi tu, maji ya mto Lukosi eneo la Ruaha Mbuyuni, Morogoro. Mto Lukosi unaunganika na mto Kilombero na hata kufika kwenye maporomoko ya Stieglers George yenye kumwaga maji yake kwenye mto Rufiji. Ni kwenye maporomoko hayo ambapo tatizo la umeme Tanzania lingekuwa historia kwa miaka mingi sana.

Lakini ni kwanini basi viongozi wetu, tena wasomi wazuri tu, wameweza kuhalalisha mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kule Kiwira, Mbeya na kuachana na miradi kama ya umeme wa maji kama huu wa Stieglers George? Wameweza kuhalalisha ujio wa Richmond na baadae Dowans na baadae tufahamu kuwa ni makampuni yenye utata?

" The end justify the means"- hatma ya jambo huhalalisha njia za kufikia hatma hiyo. Kwa mafisadi, kama hatma ya jambo hilo lina maslahi kwao, basi, hawajali kama njia itakayotumika itakuwa na madhara makubwa kwa walio wengi au la. Haya ndiyo tunayoyaona katika Richmond na Dowans, lakini yapo pia katika mikataba mingine ya kifisadi kama vile IPTL.

The End Justify The Means, na hilo ni Neno La leo.

Maggid,
Iringa
 
Lakini ni kwanini basi viongozi wetu, tena wasomi wazuri tu, wameweza kuhalalisha mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kule Kiwira, Mbeya na kuachana na miradi kama ya umeme wa maji kama huu wa Stieglers George? Wameweza kuhalalisha ujio wa Richmond na baadae Dowans na baadae tufahamu kuwa ni makampuni yenye utata?

" The end justify the means"- hatma ya jambo huhalalisha njia za kufikia hatma hiyo. Kwa mafisadi, kama hatma ya jambo hilo lina maslahi kwao, basi, hawajali kama njia itakayotumika itakuwa na madhara makubwa kwa walio wengi au la. Haya ndiyo tunayoyaona katika Richmond na Dowans, lakini yapo pia katika mikataba mingine ya kifisadi kama vile IPTL . The End Justify The Means, na hilo ni Neno La leo.
Maggid,
Iringa.

Wakati wa uchaguzi ulikipigia CCM debe la nguvu huku ukijua ni chama cha mafisadi sasa haya malalamiko na manung'uniko yanatoka wapi?
 
Kamati Teule inakubaliana na ushauri uliotolewa na Kamati ya Uwekezaji na Biashara katika taarifa yake kwa Bunge kwa mwaka 2006 kuwa Serikali sasa iandae mpango madhubuti wa muda wa kati na muda mrefu ( power system master plan) ukionesha ni namna gani nchi itatekeleza na kukabiliana na tatizo la mfumo mzima wa uzalishaji na usambazaji wa umeme.

Huwezi kuwa Power Master Plan wakati serikali haijawachukulia hatua wote wanaofaidika na hizi DHARURA za umeme!

Mpango wa aina hii utaipunguzia Serikali gharama ya kuingia mikataba ya dharura mara kwa mara kila kukitokea ukame. Aidha mpango huo ujumuishe pamoja miradi kama ya Stieglers George ya kuzalisha umeme wa MW 2100 na zaidi, makaa ya mawe ya mchuchuma, umeme wa nishati ya gesi asilia, upepo, jua, taka n.k. Hapo tutakuwa tumejijengea msingi mzuri wa kupokea changamoto za maendeleo ya nchi za kipato cha kati" ( Ripoti ya Tume Teule ya Uchunguzi wa Richmond)

Hakika, hitimisho la ripoti ndefu ya Tume ya Mwakyembe limenifanya niumize kichwa kutaka kujua zaidi mbali ya mambo mengine, juu ya mradi wa Stieglers George ambao kama ungekamilika, ungekuwa na uwezo wa kuzalisha MW 2100 na zaidi. Kiasi hicho cha umeme kingetosha kwa mahitaji yetu ya ndani na hata kupatikana ziada ya kuuza nje.

Hii ya Stiegler George na MW 2100 kila siku uwa najiuliza ni kwanini basi tusielezwe kwanini tusiutekeleze na badala yake tuendele kuangaika na hivi vi-miradi vya MW 100, 60, 200, 300!

Kwa projection ya wataalam wa nishati, mahitaji ya nishati katika nchi yetu yanakua kwa kasi sana na hivyo hii miradi MW 200, 300, 100 n.k si mipango ya muda mrefu. Kwasababu baada ya miaka 8 bado tutarudi pale pale kwenye vi-miradi vidogo vidogo na watawala watanufaika na 10% zao!

Lakini ni kwanini basi viongozi wetu, tena wasomi wazuri tu, wameweza kuhalalisha mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kule Kiwira, Mbeya na kuachana na miradi kama ya umeme wa maji kama huu wa Stieglers George? Wameweza kuhalalisha ujio wa Richmond na baadae Dowans na baadae tufahamu kuwa ni makampuni yenye utata?

Ni kwasababu wanaonufaika na miradi hiyo ni viongozi!

" The end justify the means"- hatma ya jambo huhalalisha njia za kufikia hatma hiyo. Kwa mafisadi, kama hatma ya jambo hilo lina maslahi kwao, basi, hawajali kama njia itakayotumika itakuwa na madhara makubwa kwa walio wengi au la. Haya ndiyo tunayoyaona katika Richmond na Dowans, lakini yapo pia katika mikataba mingine ya kifisadi kama vile IPTL . The End Justify The Means, na hilo ni Neno La leo.
Maggid,
Iringa.

"The end justify the means" - Here the means is not justified by the end!
 
Wakati wa uchaguzi ulikipigia CCM debe la nguvu huku ukijua ni chama cha mafisadi sasa haya malalamiko na manung'uniko yanatoka wapi?

Ruta,
Huo ni mtazamo wako, hata kama sikubaliani nao, nitauheshimu.
 
kwahiyo this is based on the FISADIs Point of View, Fisadi's End.... yaani kuneemeka kwa Mafisadi...

What About wananchi Point of View? How Can This Be Justified.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom