ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 1,964
- 3,895
Mradi wa Bwawa la Nyerere tuliambiwa ungekamilika June 2022, lakini haikuwa hivyo.
Hata hivyo mwezi wa 12/2022 bwawa la mwalimu nyerere lilianza kujazwa maji, ambapo Ili bwawa kujaa kabisa linapaswa kufikia Mita 184 kutoka usawa wa bahari.
Kusua kusua Kwa mradi na kuchelewa Kwa kufungwa mashine za kuzalisha Umeme yaani mifumo ya turbine itapelekea na itawalazimu wizara ya nishati na TANESCO kufungulia maji Ili kuliepusha bwawa la mwalimu nyerere kujaa maji na kupitiliza kitu ambacho magufuli alikipinga katika bwawa la mtera.
Katibu Mkuu wa wizara ya nishati akiongea ikulu, amesema ni mashine mbili tu kati ya tisa ambazo zipo karibuni kuwashwa Kwa maana saba bado kabisa, na hata hizo mbili bado zinajaribiwa.
Chakusikitisha tu, na Kwa taarifa iliyopo Sasa , na hii ni mwezi wa pili tu hata masika hayajachangamka ya March na April.
Bwawa la mwalimu nyerere limejaa na kufikia Mita 179 kutoka usawa wa bahari huku zikibaki MITA 5 Ili kufikia ukomo na uwezo wa Bwawa wa MITA 184.5, hapo hapo hakuna mashine inayozalisha Umeme.
Hivyo kulingana na mvua za mwaka huu, haifiki mwezi wa nne, bwawa litakuwa limeshajaa na mashine ni chache, hivyo Ili maji yasizidi itabidi TANESCO wafungulie maji yapite bila kuzalisha Umeme , huu ni uzembe mkubwa.
Pia kwanini serikali isiongeze mashine ya MW 100 katika Bwawa la Mtera