Juzi niliona katika taarifa ya habari ya ITV wananchi wa vijiji mbalimbali bondeni mwa Bwawa la Mwalimu Nyerere wakihaha kuokoa maisha yao baada ya kuzingirwa na maji ya mto Rufiji. Hii inatokana na kujaa kwa bwawa hivyo kulazimisha kufungulia maji kutoka bwawani.
Pia tumekwisha fahamishwa kuwa mtambo mmoja kati ya tisa ya kuzalisha umeme bwawani hapo umewashwa na kuzalisha MW 235. Kwa hiyo bado mitambo nane ambayo baada ya kukamilika kufungwa itawashwa na bwawa kuanza kuzalisha MW 2115. Hakika ni jambo jema sana.
Wasiwasi ni kuwa kama kuwashwa kwa mtambo mmoja tu kumesambaratisha wanavijiji na kuanza kuhama makazi yao, hali itakuwa vipi pale mitambo yote tisa itakapowashwa? Je, vijiji vilivyopo bondeni mwa Bwawa vitaendelea kuwepo? Je, wananchi wamekwisha taarifiwa lo lote kuhusu hali ya baadaye ya makazi na mashamba yao?
Ikumbukwe kuwa mitambo yote itakapokuwa inafanya kazi hakutakuwa na kupungua maji tena kwa kuwa maji yatafunguliwa kwa kiwango kile kile mwaka mzima.