Msumbiji kujenga Bwawa la kuzalisha umeme. Litakamilika kabla ya JNHP

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,168
MAPUTO, Msumbiji: MSUMBIJI imesaini mkataba na muungano unaoongozwa na kampuni kubwa ya umeme ya Ufaransa EDF kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme wa Mphanda Nkuwa wenye thamani ya Dola bilioni 5.

Bwawa na kiwanda cha kuzalisha umeme wa maji kitajengwa kando ya mto Zambezi katika jimbo la Tete Kaskazini mwa Msumbiji, na kitazalisha megawati 1,500 za umeme katika awamu ya kwanza.

"Hii ni hatua madhubuti ya kwanza kwa Msumbiji kunufaika na uwezo mkubwa wa kufua umeme wa mto Zambezi na rasilimali nyingine za nishati nchini." Waziri wa Nishati Msumbiji, Salvador Namburete alisema.

Muungano ulioshinda unaoongozwa na EDF unajumuisha TotalEnergies na Sumitomo Corporation, na utaendeleza, kujenga na kuendesha mradi wa kufua umeme wa Mphanda Nkuwa
 
The resistance of communities to Mphanda Nkuwa Dam in Mozambique

Wananchi wahoji maswali magumu, vyanzo vingine vya nishati endelevu kama gesi ipo wapi ?

View: https://m.youtube.com/watch?v=TiLEBzYPYLc
Mozambique haioni tena fursa ya kupata umeme utokanao na gesi nyingi ya jimbo la Capo Delgado na kuamua kama sisi kujenga bwawa la umeme kwa fedha nyingi, je gesi yao yote imeuzwa kwa mikataba mibovu ?

2022 23 November
Rovuma offshore gas project.

Rais Felipe Nyusi akitembelea mradi wa gesi katika bahari kuu ya Mozambique


View: https://m.youtube.com/watch?v=CV9es5zj_uc
Katika hotuba yake mheshimiwa Rais Felipe Nyusi anasema tunauona mradi huu ni ushahidi wa mfano wa dunia kuja pamoja kwa mafanikio ya wote.

Mradi huu wa gesi LNG Rovuma basin Mozambique unaendeshwa na kampuni kubwa kutoka Italia ikitumia meli ya kisasa iliyotengenezewa na kampuni ya Samsung Korea kama mtambo (platform)wa kuchimba gesi katika bahari kuu.
 
Hongera zao sie kwetu umeme umekuwa anasa anakata sa mbili asubuhi unarudi sa moja jioni no maelezo Wala nn na viongozi wanalichukulia poa tu
 
Back
Top Bottom