Hii issue ukiitazama kwa makini naona kuna kitu serikali inaficha, na sijui wanafanya hivyo kwa manufaa ya nani.

Kama mtu kakosea awajibishwe lakini kumuacha ni sawa na kulea uozo kwa watendaji wa serikali, au labda wanasubiri atoke hospitali ndio hatua nyingine zifuate..
Halafu eti mtu kuvunjika kidole gumba Cha mkono tu ndiyo analazwa hospitali siku tatu!!! Je angevunjika kiuno angelazwa miaka mingapi?! Any way , serikali wanaficha kilichotokea kama busara kwa ajili ya kunusuru ndoa yake. Ukweli ukijulikana mke wa naibu waziri atazua mtafaruku ambao serikali hawataki jambo Hilo litikee
 
Kwani Polisi wanasemaje? Ajali ilitokea wapi? Saa ngapi? Gari ilikuwa na abiria wangapi? Evacuation mission ya majeruhi ilifanywa na nani?

Polisi walifika eneo la tukio? Waliwahoji mashuhuda na wakasemaje? Majibu kama haya, huwa yanatolewa na Polisi na inakuwa ndio taarifa rasmi ya ajali.
 
Viongozi nchi wepesi sana

We wategeee madem tu utawaokota sana

Ova
Hahaha.................wakifanyiwa maajabu tu huko vyumbani kazi inakuwa imeisha.

Watu wanafunguka hadi mipango ya 2030 huko 😄🙌
 
View attachment 2604901

JESHI la Polisi nchini limesema ajali iliyotokea Aprili 26, 2023 ikimuhusisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dk Festo Dugange ilisababishwa na Bodaboda aliyekuwa akivuka barabara ghafla bila kuchukua tahadhari.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP Martin Otieno imesema gari hilo lenye usajili wa T 454DWV aina ya Toyota Land Cruiser likiendeshwa na Naibu Waziri Dugange lilipoteza mwelekeo na kugonga kigo ya barabara ya Iyumbu maeneo ya St Peter Clever na kupinduka.

“Kulikuwa na mtu moja tu (dereva) kwenye gari hilo ambaye ni Naibu Waziri. Alivunjika kidole gumba cha mkono wa kulia na kupata majeraha katika mkono huo,” amesema Kamanda Martin.

Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amemjulia hali Dk Ndugage ambaye amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Doodma.

Pia, soma: Dodoma: Naibu Waziri wa TAMISEMI Festo Dugange apata ajali akiendesha gari
 
Back
Top Bottom