Dkt. Mollel acha kupotosha maudhui ya hoja ya Mpina kuhusu makalio

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
214
686
Dk. Mollel Naibu Waziri wa Afya acha kutumia ofisi na kodi za umma kuendesha propaganda na kupotosha maudhui ya hoja ya Mheshimiwa Mpina kuhusu Hospitali za Umma kutoa huduma za kuongeza Makalio badala ya kutumia fedha hizo kuboresha huduma za afya za msingi.

Kama umeamua kumjibu Mpina hoja zake aliweka kwa maandishi na wewe kama umeamua kumjibu jibu hoja zake zote kwa maandishi usipotoshe maudhui ya hoja zake kuhusu sekta ya afya kwa kuchagua kipengele cha makalio ambacho nacho unakipotosha makusudi ukidhani watanzania ni wajinga.

Hujiulizi kwanini Waziri wako wa AFYA, Ummy Mwalimu amekwepa kumjibu Mpina kwa sababu anafahamu Mpina sio mbunge wa kukurupuka na hoja sasa umejiingiza wewe kujifanya unamjibu matokeo yake umepotosha na kuharibu zaidi.

"Hospitali za Serikali kuacha jukumu lake la msingi na kuanza kufanya kazi za anasa kama kuongeza ukubwa wa makalio badala ya kujishughulisha kikamilifu kutibu maradhi yanayosumbua wananchi, tunao uhaba mkubwa wa raslimali fedha katika kutatua matatizo ya huduma za afya, mfano leo ni zaidi ya miaka 3 tumeshindwa kutoa mtaji kwa MSD wa takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba kutokana na ukosefu wa fedha, hizi fedha za kununua mitambo na vifaa vya kuongeza ukubwa wa makalio zimetoka wapi?" -Mpina

Luhaga Mpina ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM) amezungumza hayo alipokutana na Wanahabari kwenye Uwanja wa New Amani Complex, Zanzibar wakati wa maadhimisho ya miaka Sitini (60) ya Mapinduzi ya Zanzibar
 
Ni jambo la heri mkiendelea kuparuana wenyewe kwa wenyewe. Maana inaleta faraja kwa sisi tunao kiombea njaa hicho chama chenu.
 
IMG_20231214_200958.jpg
 
Back
Top Bottom