Mpina: Hizi fedha za kununua mitambo na vifaa vya kuongeza ukubwa wa makalio zimetoka wapi wakati MSD imekosa mtaji?

adili2

JF-Expert Member
May 22, 2021
826
623
"Hospitali za Serikali kuacha jukumu lake la msingi na kuanza kufanya kazi za anasa kama kuongeza ukubwa wa makalio badala ya kujishughulisha kikamilifu kutibu maradhi yanayosumbua wananchi, tunao uhaba mkubwa wa raslimali fedha katika kutatua matatizo ya huduma za afya, mfano leo ni zaidi ya miaka 3 tumeshindwa kutoa mtaji kwa MSD wa takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba kutokana na ukosefu wa fedha, hizi fedha za kununua mitambo na vifaa vya kuongeza ukubwa wa makalio zimetoka wapi?" -Mpina

Luhaga Mpina ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM) amezungumza hayo alipokutana na Wanahabari kwenye Uwanja wa New Amani Complex, Zanzibar wakati wa maadhimisho ya miaka Sitini (60) ya Mapinduzi ya Zanzibar
 
Sio kila wakati kuwaza kutatua shida tu. Kuna baadhi ya shida zitaendelea kuwepo.

Ifike wakati pia tukubali kutatua namna ya kuishi maisha mazuri. Kama hivyo kuongeza urembo na ubora wa maisha.
 
Mpina ni mzalendo sana.hii ya kuongeza makalio ni upuuzi mtupu.huyo profesa aliyeanzisha huo mradi ni punguani kabisa.hospitali hazina dawa lakini wapuuzi wanaagiza mashine za kunenepesha matako Kwa ajili ya Nini?upumbavu kabisa
 
Back
Top Bottom