Dk. Slaa: Si uhaini kumng'oa rais Kikwete kabla ya 2015

Dr. Slaa ametumia mantiki na si ngumu kuelewa; kama Mwenyekiti wa Mtaa amechaguliwa na anaweza kuondolewa na wananchi wake waliomchagua kabla ya muda wake (wakifuata taratibu zilizopo) basi yawezekana kabisa kumuondoa Rais aliyeko madarakani kabla ya muda wake kwa kufuata taratibu zilizopo. Hili haliitaji uanasayansi kulielewa vinginevyo tusingekuwa na vipengele vya impeachment au sheria inayoruhusu mtu akivuliwa uanachama wake anapoteza haki ya kuwa Mbunge au Rais.
Tofauti na alivyosema.tuache kutetea au kufabricate maneno ili yamake sense!.....that statement was kinda shallow.
 
Tuchukue mifano mingine inayofanana na ya mweyekiti wa mtaa ambapo Rais anaweza kugolewa kabla ya muda wa muhula wake kuisha :
  • Je Rais akipatikana na kashfa kubwa akapigiwa kelele zisizokwisha na kumnyima usingizi Rais na hatimaye akangoka kwa 'kujiuzulu' kama Edward Lowassa itakuwa Uhaini?
  • Je Rais akiona maandamano yasiyokwisha dizaini ya Tunisia na Egypt 'akangoka' ni uhaini?
  • Je Raisi akirukwa akili na kulazimishwa kungoka ingawa hataki ni uhaini?
  • Je tukijadili na kudai katiba mpya yenye kifungu cha kumpigia kura ya kutokua na imani na Rais aliyepo akangoka ni uhaini?
  • Je ndani ya CCM wakitumia vikao vyao wakamngoa Raisi kabla ya muda wake kama ambavyo walifanya kwa Mh. Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Aboud Jumbe Mwinyi alivyongolewa na vikao vya chama kwa sababu ya 'kuchafua hali ya hewa ya kisiasa' ni uhaini?
Mimi naona ni haki ya msingi kabisa wananchi kumgoa Rais wa Nchi kama atashindwa kutimiza majukumu ya kazi zake vizuri au kutokana na sababu hizo hapo juu (in bullet form) hata kama muhula (awamu) yake ya Uraisi haujaisha ili kuleta uwajibikaji kwa taasisi ya Urais kwani cheo cha Uraisi ni dhamana na si Usultani.
 
Tanzania si kigenge cha wahuni! Wananchi wa Tanzania msiwafanye waovyo! Ni miezi sita tu nyuma walipewa hiyari na kumchaguwa waliemuona anawafaa. Walipofanya hivyo walikuwa wakijuwa kwa hakika kuwa watakuwa nae kwa kipindi cha miaka mitano!
Hivyo hiki kipindi cha miezi sita kimeshatowa jawabu kuwa walikosea? na kipi kilichofanywa na CHADEMA cha kuwafanya wahisi walikosea kutokichagua?
sijakuelewa unauliza au unatoa jibu, kumtoa kiongozi kama kikwete majibu unayo hata kikwete anajijua kwa mimi watanzania wana hasira naye ndio maana alitangaza kuvua watu magamba lakini naona kaweza kwa makamba tu, point ni kwamba hii ni nchi hatujamkodishia kwa miaka mitano anaweza kutolewa muda wote , na kwa uongozi wake huu hatufai, sijui wewe unaishi Tanzania ipi unashindwa kuona matatizo yalipo na yanazidi kila kukicha
 
<br />
Kwako wewe demokrasia ni nini? Na nini maana ya chaguzi? Hizi kelele zinapoteza lengo sasa na hatimaye hata ile maana ya sensitisation inaondoka. Hivi kwanini kelele hizi zisipigwe kwenye katiba? Au kwanini nafasi hii na hizo rasilimali chache wangewekeza kwenye majimbo? Maana hii ni njia rahisi kujulikana kuwa chama kinataka kufanya nn kuliko sasa hivi msisitizo umekuwa ni vurugu.

crap pole sana, next time shirikisha ubongo
 
Rais kujiuzulu na rais kuondolewa madarakani kisheria inawezekana.Rais anaweza kujiuzulu kutokana na pressure au hiari yake,mradi tu aondoke madarakani rasmi.Pia kisheria kwa kupitia bunge.
Lakini huwezi kutumia sheria ya serikali za mitaa,1982 kumuondoa rais.Huwezi hata kujaribu kuihusisha hii sheria kuhalalisha vote of no confidence or some kind of a referrendrum ya kumuondoa rais madarakani,honestly that's treasonous or to be more liberal, that is seditious.
 
Sheria ( katiba) inaruhusu ila ni kupitia bungeni kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais, tatizo je wabunge wa ccm watapiga kura hiyo? Kumng'oa rais kabla ya uchaguzi ujao sio uhaini kama utaratibu wa kisheria utafuatwa, ni uhaini pale tu itakapotumika nguvu kumtoa (coup detat), nje ya hapo sio uhaini.
 
na Waandishi wetu
Tanzania Daima

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimehitimisha ngwe nyingine ya maandamano ya amani kuishinikiza serikali iboreshe maisha ya wananchi, kikielekeza mashambulizi kwa viongozi na watendaji wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwamba wanasababisha vifo na maisha magumu kwa wananchi.

Katika kusisitiza umuhimu wa serikali kuwajibika kwa wananchi na kutetea falsafa ya chama ya ”nguvu ya umma,” Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, na Naibu wake, Zitto Kabwe, jana na juzi waliwasha moto katika maeneo tofauti nchini, huku Dk. Slaa akisema, ”si uhaini kwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete kung’olewa kabla ya mwaka 2015, kama Watanzania wataamua kufanya hivyo.”

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo juzi jioni mkoani Iringa alipokuwa akizungumza na viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vya Mkwawa, Tumaini na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Ruaha.

Alisema katika nchi yoyote ya kidemokrasia wananchi wanayo haki ya kuuwajibisha utawala uliopo madarakani kwa njia mbalimbali hata ikilazimu kuuondoa kwa kura ya maoni kabla ya uchaguzi.

Alisisitiza kuwa haki hiyo ipo pindi wananchi wenyewe wanapoona utawala umeshindwa kabisa na hauonyeshi matumaini yoyote ya kutatua matatizo na kutimiza matakwa yao.

Alifafanua kuwa ingawa Katiba ya Tanzania haijatoa utaratibu wa moja kwa moja kama uliopo kwenye nchi nyingine, lakini bado Watanzania wakiamua wanaweza kuiondoa serikali isiyofaa madarakani kwani kwa mujibu wa katiba hiyo hiyo, wao ndio msingi wa mamlaka yote.

“Mfumo wa sheria ukiwa mbovu, mfumo wa kikatiba ukiwa unawanyima watu fursa ya kutekeleza haki zao za kikatiba, ukiwa ni wa kidikteta basi ridhaa ya wananchi walio wengi wakiamua kuukiuka mfumo huo hauwezi kuwa uhaini, maana wao ndio mamlaka ya mwisho ya katiba yenyewe,” alisema.

Akifafanua uhalali wa suala hilo iwapo litaamuliwa na wenyewe, Slaa alisema tayari sheria za nchi, kama sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982, imeshatoa mamlaka hayo kwa wananchi, kwani inawaruhusu kumwondoa mwenyekiti wa kijiji kwa kura ya maoni wakati wowote wakiona hawafai.
“Ibara ya 146 ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982, inasema wananchi ndio wenye mamlaka yote ya kumweka mwenyekiti wa serikali ya mtaa au kijiji na ndiyo wenye mamlaka ya kumwondoa wakati wowote kwa kupiga kura ya maoni.

“Wakitaka hata kabla ya kipindi rasmi cha uchaguzi kufika....kwa hiyo kama ni halali kwa ngazi ya kijiji basi ni halali pia kwa ngazi ya urais kama wananchi wenyewe walio wengi wakiamua kufupisha muda wa serikali yao,” alisema Dk. Slaa.

Kauli hiyo ya Dk. Slaa, imekuja siku chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, kusema kuwa Rais Kikwete hawezi kung’olewa kabla ya mwaka 2015 na kusisitiza kuwa kufanya hivyo ni uhaini.

Dk. Slaa alibainisha kuwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeshindwa kutatua matatizo ya msingi yanayovikabili vyuo vya elimu ya juu, badala yake imekuwa ikishughulika na mambo madogo madogo pamoja na kujaribu kuihusisha CHADEMA na migomo inayotokea vyuoni.

Aliwataka wasomi wa vyuo vikuu kuwa mstari wa mbele kushiriki siasa ili kuliletea taifa mabadiliko yenye tija huku akiwasisitizia kuwa mapinduzi ya umma kama yaliyofanyika nchini Misri na Tunisia ni hatua ya mwisho kabisa inayoweza kufanywa na jamii yoyote ambayo imechoshwa na uongozi usiowajibika kwa watu wake.

Mapema wiki hii, aliitoa kauli hiyo akiwa Songea, lakini Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, alimjibu kuwa huo ni uhaini kwa kuwa rais alichaguliwa na wananchi, na katiba inamruhusu kukaa madarakani hadi mwaka 2015 utakapofanyika uchaguzi mwingine.

Lakini Dk. Slaa anasema si lazima kiongozi kukaa madarakani hadi uchaguzi mwingine kama hatatimiza wajibu wake; na kwamba wananchi wakiamua wanaweza kutumia haki yao kumwondoa.

Naye Zitto alimvaa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hamis Kagasheki, akimtaka kukiri kuwa serikali inahusika na mauaji ya raia yaliyotokea katika mgodi wa Nyamongo wilayani Tarime, mkoani Mara.

Zitto alitoa kauli hiyo jana mkoani Mwanza ambapo alisema Kagasheki, hawezi kukwepa lawama kwani polisi ndio waliohusika kuwaua kwa risasi raia wasio na hatia na si chama cha siasa alichokituhumu.

Alisema anazo taarifa kwamba askari polisi wanaolinda mgodi huo wa Nyamongo wamekuwa wakipewa kitu kidogo kisha kuruhusu watu kuchukua mawe.
“Namshangaa Naibu Waziri Kagasheki kutuhumu chama cha siasa kwa mauaji haya. Polisi isikwepe lawama kwa hili. Inakuwaje polisi impige risasi mtu anayekimbia?” alihoji.

Alisema mtu anayekimbia ana lengo la kusalimisha maisha yake, kwa hiyo hakukuwa na sababu za kufyatuliwa risasi.
Alibainisha kuwa matukio ya polisi kuua raia yanalipaka matope taifa katika uso wa dunia, jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linaweza kuwakimbiza watalii.

Zitto aliitaka Polisi na serikali kuacha kuwapotosha Watanzania kwamba CHADEMA imeingiza mkono kwenye mauaji hayo badala yake serikali itekeleze ushauri wa Kamati ya Madini ya mzee Bomani kutoa asilimia 20 ya fedha.

Wakati huo huo, Zitto aliunga mkono msimamo wa Tanzania wa kuitaka serikali ya Uingereza kurejesha fedha za rada serikalini moja kwa moja badala ya kuzipitishia kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali. Alisema fedha hizo si msaada kwa Tanzania bali ni zake, hivyo hakuna sababu ya kuzipitisha kwenye mashirika hayo ambayo amesema nayo yamekumbwa na ufisadi.
 
Rais kujiuzulu na rais kuondolewa madarakani kisheria inawezekana.Rais anaweza kujiuzulu kutokana na pressure au hiari yake,mradi tu aondoke madarakani rasmi.Pia kisheria kwa kupitia bunge.
Lakini huwezi kutumia sheria ya serikali za mitaa,1982 kumuondoa rais.Huwezi hata kujaribu kuihusisha hii sheria kuhalalisha vote of no confidence or some kind of a referrendrum ya kumuondoa rais madarakani,honestly that's treasonous or to be more liberal, that is seditious.

Kobello unaniangusha bwana.. soma kilichonukuliwa - remember ni sehemu ya nukuu tu na hivyo hatuna kile hasa kilichosemwa in its proper context:

"Ibara ya 146 ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982, inasema wananchi ndio wenye mamlaka yote ya kumweka mwenyekiti wa serikali ya mtaa au kijiji na ndiyo wenye mamlaka ya kumwondoa wakati wowote kwa kupiga kura ya maoni.

"Wakitaka hata kabla ya kipindi rasmi cha uchaguzi kufika.... (premise ambayo imekatishwa) kwa hiyo kama (Dr. Slaa anaelekeza hitimisho kwa kutumia mantiki ) ni halali kwa ngazi ya kijiji basi ni halali pia kwa ngazi ya urais kama wananchi wenyewe walio wengi wakiamua kufupisha muda wa serikali yao,"

Hili linawezekana kisheria na sijaona mahali popote ambapo Dr. Slaa amedai kutumia njia nje ya zile zilizoko kisheria.
 
CCM wataendelea kutuma kila mbinu kuendelea kukaa madarakani lakini la mgambo limelia watatoa chozi la damu. Sio siri Watanzania wengi hawaipendi hii serikali dhalimu ambayo imewafanya Watanzania kuwa watumwa kwenye nchi yao wenyewe kwa mgongo wa M k w e r e .
 
Mwanakijiji unapotosha makusudi, Slaa alikuwa anatafuta kipengele kinachohalalisha kumng'oa rais kabla ya muda. Akataja sheria ya serikali za mitaa! Kadondokea pua! Constitutional law sio sawa na Cannon law! SLAA KACHEMKA MCHANA KWEUPE!
 
Daktari (PhD) wa ukweli amemjibu Mukama kuwa wananchi wanauezo kikatiba wa kumuondoa JK madarakani kabla ya 2015. “Ibara ya 146 ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982, inasema wananchi ndio wenye mamlaka yote ya kumweka mwenyekiti wa serikali ya mtaa au kijiji na ndiyo wenye mamlaka ya kumwondoa wakati wowote kwa kupiga kura ya maoni.

“Wakitaka hata kabla ya kipindi rasmi cha uchaguzi kufika....kwa hiyo kama ni halali kwa ngazi ya kijiji basi ni halali pia kwa ngazi ya urais kama wananchi wenyewe walio wengi wakiamua kufupisha muda wa serikali yao,” alisema Dk. Slaa.

Kauli hiyo ya Dk. Slaa, imekuja siku chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, kusema kuwa Rais Kikwete hawezi kung’olewa kabla ya mwaka 2015 na kusisitiza kuwa kufanya hivyo ni uhaini.

CHANZO: GAZETI LA TANZANIA DAIMA

Hapa dr Slaa kachemka kweli, huwezi kunukuu sheria za serikali za mitaa kwa mambo ya kikatiba, hivi hajui kuwa katiba ndiyo sheria mama?.
Bora kama hajui kifungu gani cha katiba kinaweza kumtoa raisi madarakani kabla ya muda wake angenyamaza kimya au angeacha kabisa kuhusisha sheria hiyo ya serikali za mitaa na raisi angeishia tu kwa wenyeviti wa serikali za mitaa,halmashauri na vijiji.
 
Kobello unaniangusha bwana.. soma kilichonukuliwa - remember ni sehemu ya nukuu tu na hivyo hatuna kile hasa kilichosemwa in its proper context:

"Ibara ya 146 ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982, inasema wananchi ndio wenye mamlaka yote ya kumweka mwenyekiti wa serikali ya mtaa au kijiji na ndiyo wenye mamlaka ya kumwondoa wakati wowote kwa kupiga kura ya maoni.

"Wakitaka hata kabla ya kipindi rasmi cha uchaguzi kufika.... (premise ambayo imekatishwa) kwa hiyo kama (Dr. Slaa anaelekeza hitimisho kwa kutumia mantiki ) ni halali kwa ngazi ya kijiji basi ni halali pia kwa ngazi ya urais kama wananchi wenyewe walio wengi wakiamua kufupisha muda wa serikali yao,"

Hili linawezekana kisheria na sijaona mahali popote ambapo Dr. Slaa amedai kutumia njia nje ya zile zilizoko kisheria.

Cheap politics!
Lengo kuu la kuunda chama cha siasa ni kushinda uchaguzi na kuongoza nchi! uchaguzi umekwisha.. wapeni CCM miaka mitani yao watawale.. mbona mnawapa excuses za kampeni ya 2015??
By nature watanzania hawapendi fujo.. hii tone itakuja kuwa backlash mbele ya safari. they better stick with policies!
CHADEMA inabidi ifanye kampeni za kuwaambia wananchi itawafanyia 1,2, 3 ,4... vitu ambavyo CCM kamwe haiwezi kufanya.. na inabidi wa-stick na hiyo message. Inabidi wairudie hiyo message until next election. Haya mengine ni unnecessary distraction ambayo itakuja kuwa-cost mbele ya safari.
 
Brutus, nadhani unashindwda kunipata; sijasema JK aondolewe kabla ya muda; naelezea nadharia ya mfumo wetu wa kibunge (parliamentary system). Serikali kuondoka madarakani kabla ya muda wake wa uchaguzi kufika si jambo geni hivi. Kuitisha uchaguzi kabla ya muda wa kawaida kupita jamani siyo jambo la ajabu wala isionekane ni uhaini au uasi. Ni mfumo tuliouchagua wenyewe na matokeo yake ni lazima tuwe tayari kuyapokea. Wananchi ndio wenye madaraka ya kutawala si Rais; Rais anatawala kwa kadiri ya kwamba wananchi wanakubali aendelee kutawala. Kama Serikali inaonekana mbele ya wananchi haiwezi kuendelea kutawala au kuongoza serikali na aidha inawatawala wananchi wake vibaya haiwezi kujitetea "mbona muda wetu haujafika".

Hivyo nilichokigusia ni kuonesha kuwa watu waondokane na dhana hii ya kusema kuwa serikali inapaswa kubakia madarakani hata ikiboronga kwa kisingizio "miaka yetu mitano haijafika". As a matter of fact ningependa kweli kwenye Katiba Mpya kuweka uraihis zaidi wa kuiwajibisha serikali na kuiondoa madarakani na kiongozi yeyote wa kuchaguliwa kuweza kuondolewa inapoonekana anashindwa kuwajibika. Hivi unafikiria kama Rais aje kugunduliwa kuwa anafanya biashara za uhalifu na chama chake hakitaki kumuwajibisha wananchi wafanye nini? wasubiri hadi miaka yake mitano iishe?
 
Kama kweli Dr Slaa kasema hivi,basi atakuwa amechemka na kajishushia hadhi.Mfano wa Rais na Mwnyekiti wa Kijiji wapi na wapi?

slaa ametoa a very logical reasoning ndugu. Usipinge tu bila mantinki pia. Be very careful na logical reasoning. Kuna umuhimu wa kufundisha logic kuanzia chekechea
 
Niaminicho ni kwamba Raisihakodishiwi hii nchi bali ni kama mgeni tu akiribishwavyo ndani mwa nyumba ya mtu,akichafua tu hali ya hewa si lazima ukashitaki polisi ili waje wamuondoe ndani kwako,bali wamtimua hata kama ni usiku wa manane..hii ni kwa simpo mantiki ya kifamilia vivohivyo kwa simpo mantiki ya kijamii katika ngazi ya vijiji,..namuunga mkono
 
Brutus, nadhani unashindwda kunipata; sijasema JK aondolewe kabla ya muda; naelezea nadharia ya mfumo wetu wa kibunge (parliamentary system). Serikali kuondoka madarakani kabla ya muda wake wa uchaguzi kufika si jambo geni hivi. Kuitisha uchaguzi kabla ya muda wa kawaida kupita jamani siyo jambo la ajabu wala isionekane ni uhaini au uasi. Ni mfumo tuliouchagua wenyewe na matokeo yake ni lazima tuwe tayari kuyapokea. Wananchi ndio wenye madaraka ya kutawala si Rais; Rais anatawala kwa kadiri ya kwamba wananchi wanakubali aendelee kutawala. Kama Serikali inaonekana mbele ya wananchi haiwezi kuendelea kutawala au kuongoza serikali na aidha inawatawala wananchi wake vibaya haiwezi kujitetea "mbona muda wetu haujafika".

Hivyo nilichokigusia ni kuonesha kuwa watu waondokane na dhana hii ya kusema kuwa serikali inapaswa kubakia madarakani hata ikiboronga kwa kisingizio "miaka yetu mitano haijafika". As a matter of fact ningependa kweli kwenye Katiba Mpya kuweka uraihis zaidi wa kuiwajibisha serikali na kuiondoa madarakani na kiongozi yeyote wa kuchaguliwa kuweza kuondolewa inapoonekana anashindwa kuwajibika. Hivi unafikiria kama Rais aje kugunduliwa kuwa anafanya biashara za uhalifu na chama chake hakitaki kumuwajibisha wananchi wafanye nini? wasubiri hadi miaka yake mitano iishe?

Mpiga kura wa kawaida anayeshindwa kupata milo mitatu kwa siku ni vigumu kuelewa hii conversation! Strategically ni vema waki-stick na messages walizokuwa nazo kipindi cha kampeni. Kumwambia mwenye njaa kuwa anaweza kumtoa madarakani rais hata kabla ya muda wake... u can tell mwenye njaa atakuwa anafikiria kitu gani!
 
Huyu Padri sasa amechanganyikiwa ni afadhali aende Loliondo kwa Babu akapate kikombe huenda akapona maradhi aliyonayo ya kutaka kupora Urais baada ya kupora mke wa mtu!
 
Tofauti na alivyosema.tuache kutetea au kufabricate maneno ili yamake sense!.....that statement was kinda shallow.

Duh! Slaa anawaacha wengi sana jamani, katumia analogy ndogo sana ili hata watu wa kijijini waweze kumuelewa lakini waliopo JF wengine wametoka kapa.Mifano tumeshaiona duniani na hata Africa lakini bado watu hawaelewi. Rais can go anytime as long as waliomuweka wanaona anawawekea kiwingu cha maendeleo kama anavyofanya Kikwete.
 
Rais kujiuzulu na rais kuondolewa madarakani kisheria inawezekana.Rais anaweza kujiuzulu kutokana na pressure au hiari yake,mradi tu aondoke madarakani rasmi.Pia kisheria kwa kupitia bunge.
Lakini huwezi kutumia sheria ya serikali za mitaa,1982 kumuondoa rais.Huwezi hata kujaribu kuihusisha hii sheria kuhalalisha vote of no confidence or some kind of a referrendrum ya kumuondoa rais madarakani,honestly that's treasonous or to be more liberal, that is seditious.
Mijitu mingine sijui inatumia MEDULA OBLONGATA kufikiri ? Mwanakijiji amekujibu soma hapa chini

Back
Top Bottom