Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,170
Mimi narudia na kukuunga mkono kwamba mwenendo huu wa Chadema unaweza kuwafanya waonekane wana sinister motive, over and above kupigania haki na maisha bora ya watanzania na hupati shida kuona dhamira yao pale wanapokuwa mikutanoni na kuwauliza wananchi: "Mnataka kama Tunisia?". Hapa unaona kabisa kwamba lengo la chadema siyo kuiweka serikali katika mkondo unaotakiwa na wakati huo huo kutoa sera mbadala ambazo zitaifanya ikubalike na kuja kupewa ridhaa hapo baadae. Kwa kuleta analogy ya namna unavyoweza kuondoa kiongozi katika ngazi za serikali ya mitaa, inadhihirisha kabisa kwamba hiyo ndiyo dhamira waliyonayo katika ngazi ya juu ya utawala na pengine ndiyo maana slogan za ki-Tunisia Tunisia zinaimbwa sana. Hata ukiangalia na kupima sana, hupati hasa malengo ya mikutano yao na kile wanacholenga kukiwasilisha kwa wananchi. Je, ni mikutano ya kushukuru? Ni mikutano ya kuhamasisha kuchangia mjadala wa katiba? Ni mikutano ya kuishinikiza serikali iondoe kodi kwenye mahitaji muhimu? Au ni mikutano ya kulipua mabomu (ya mafisadi wapya) na kufichua majina ya waliokuwa waanzilishi wa CCJ na jinsi walivyopata vyeo CCM?
Kwa maoni yangu, Chadema wako kwenye hatari ya ku-squander goodwill wanayo-enjoy kutoka kwa wananchi, lakini kikubwa zaidi, along the way, wanapoteza watu ambao walikuwa na matumaini na kutiwa moyo na malengo yao, kutokana na kuingiza siasa ambazo zinaonekana kukosa mwelekeo wa kujenga umoja wa kitaifa na sasa hili lililo wazi: Kuchochea wananchi waikatae serikali yao na kumuondoa rais kabla ya wakati wake!
Staili ya kujibu hoja ya kiccm huwa inanichekesha sana, siku zote ni kutishia, kutishia...... Mkuu the biggest problem with you on Chadema ni kwamba you hate Chadema, you hate Dr. Slaa, you hate new ideas, you hate anyone that is either supporting chadema's opinions or the leaders at large. You are just a hater and you are in records humuhumu ndani ya JF. Hizo tisha tisha ni muelekeo wa namna gani mmeishiwa hoja!