crap
hana akili anayesema maneno machafu juu ya slaa
Akamatwe kwa kosa lipi? labda la kupoka mke wa mtu? na hilo kisha lipanguwa kwa kulipa ugoni!
Naunga mkono mkuu, CCM walishazoa vyama dhaifu vinaonekana vinauhai wakati wa uchaguzi tu ,sasa CDM na stratagy ya hakunakulala ni kuchapa kazi katika kuonyesha madudu ya serikali na uwajibikaji sasa ccm wanaogopa kwani huu moto wa chadema ni mkali sana, na kwakuwa ccm wameishiwa hoja ya kuuzima wanasingizia amani na wanajenga mazingira ya kibabe kutaka kukidhibiti na jinsi tunavyokwenda huko mbele dola itangilia kati na kudhofisha CDM.
Ushauri.
Chadema lazima wajipange kubadilisha mbinu za upambanaji kadri mazingira yatakavyoruhusu mfano kumobulize watu wafungue matawi kakatika kila wilaya na na kuwalika vionguzi wa juu kuja kuyafungua, pia kuwatumiwa vingoozi wa wilaya katika kuanzisha matawi na kuwa karibu na wanachama wa eneo lao.
Pia kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua mara ikibainika kuwapo kwa mamluki na wasaliti ndani ya chama , jua hali hii imejitokeza sana kipindi cha uchaguzi na ikiachiwa itastawi na kuwa tatizo
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa amejibu mapigo ya Chama cha Mapinduzi(CCM) na kusema kuwa Chama chake hakitasitisha maandamano yanayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini na kwamba yupo tayari kwa lolote.
........
Kwa msisitizo akasema kuwa yeye na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe wako tayari kwa lolote hata kama ni kukamatwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya Watanzania.
.......
Hata hivyo, Dk. Slaa alisema CCM ndio inasababisha vitendo vya uvunjifu wa amani nchini kutokana na Serikali yake kutowajali wananchi maskini, hivyo lawama hizo hazipaswi kwenda kwa viongozi wa Chadema waliojitolea kufa kwa ajili kupiga kelele kwa kukataa ukandamizwaji huo.
"Mimi sina hofu na kauli wanazozitoa CCM, waache wapige kelele kwani inaonyesha ni jinsi gani serikali ilivyoshindwa kuongoza na sasa wanahitaji huruma za wananchi ambao kwa miaka mingi wamenyimwa haki zao," alisema Dk. Slaa.
Aliendelea kusema "Nchi ni sawa na tunda la amani, lilokuwa juu ya mti unaoitwa haki, nashangaa sana CCM inavyopaza sauti juu ya amani pekee ikiwa inakakataa kutoa haki, tunachohitaji ni haki ifanyike."
Hata hivyo, alisema kabla ya kwenda kushtaki kwa wananchi kwa njia ya maandamano katika mikoa mbalimbali, walitumia wabunge kuilalamikia Serikali ndani ya Bunge juu ya malipo ya Dowans, Kagoda na Meremeta, lakini serikali ilikataa kutoa majibu. Alisema, kama Serikali inaona maandamano wanayoyafanya yanavunja sheria ya nchi hakuna haja ya kukiadhibu Chadema, bali yeye na Mwenyekiti wake Mbowe wakamatwe.
Alimtaka Kapteni Chiligati kujifunza sheria na kusoma Katiba ya nchi kwanza kabla ya kuanza kutoa vitisho ambavyo vinaweza kuipeleka nchi katika sehemu mbaya.
"Naomba waache kukiadhibu chama, naomba wanitafute mimi na Mbowe watukamate tupo tayari kukamatwa kwa ajili ya kutetea wananchi, kinyume cha hapo moto huu hautazimika hadi kieleweke," aliongeza kusema.
Full Story: Home
SOURCE: NIPASHE, Jumapili, 06th March 2011.
Nyie bwana kwa mikwara, Slaa akikamatwa mtabaki mnaongea kwenye keyboard tu siku tatu nne na baada ya hapo mtasahau wala hamtaifanya kitu chochote serikali.
Wakoloni wa ccm hawaogopi kumtia slaa kolokoloni kwa sababu za wananchi waoga kama sie, wao wanachoogopa ni kupoteza reputation yao na madili yao kimataifa.
Slaa akiingia kwenye 18 zao ambayo ktk darubaini ya kimataifa itaonekana OK , na watamtia na uhakika hamtafanya lolotee wapiga mluzi.
Sasa mimi nashindwa kuelewa, Azimio la Arusha tuliandamana sana tu. Halafu CCM ni chama chama cha kudumu, inakuwaje sasa tuaogopa CDM. Maadui wa CCM wamo ndani, wafukuzeni muone kama watu hawakuandamana nchi nzima kuwaunga mkono. Ngoja niwape kidogo List.
RS
EL
AK
MK
AC
SS
sasa kuangaika na chadema, mnapoteza muda, hatutaki watu watakaotokea nsituni, heri hawa wanaosema tu. Chonde chonde safisheni nyumba ndani. Wakafanye biashara hawa.:hand: