Dk. Slaa Ajibu Mapigo ya CCM

Haki kwanza, amani itakuja tu!!
Aluta continue......................
 
You are very right Dr Slaa, endapo wanaona mnavunja sheria za nchi , why are the security forces not arresting you (Dr Slaa) and Mr Mbowe? ninavyowafahamu hawa CCM endapo kungekuwa na uvunjaji wa sheria za nchi, kwa hakika wasingechelewa kuwakamateni tangu last week.But so long as hakuna kilichovunjwa,kinachofanya ni kelele ambazo hazijibu hoja za msingi za CDM.Serikali inapaswa ishughurikie matatizo yanayowakabili wananchi hivi sasa (high prices za vitu, bad leadership maniefested in corruption, embezzlement and other manifestations of incompetent political leadership) na siyo kutuletea cheap politics zao ambao zimeshafeli kwa kiasi kikubwa.
 
Futeni chadema muone,....chama kitakuja kipya lakini hiki ili kisifutwe kita sajiliwa msituni kudadeki
 
Harakati zinazoendelea kwa sasa za CHAMA CHA DEMOCRACIA NA MAENDELEO (CHADEMA) wengi wetu tunajua nini hasa kusudio la chadema...na sivyo wanavyo fikiria CCM na uongozi wao ulioko madarakani.

Kinachoendelea sasa...nikuwaelimisha wananchi hasa wale ambao hawajui ni kitu gani kinachoendelea katika nchi hii...na hasa yale yote yalio pita huko nyuma, na kufikia hali hii ambayo ni ngumu sana kimaisha ukilinganisha na awamu tatu zilizo pita za uongozi wa serikali yetu.

Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kusema kuwa chadema wanaleta vita nchini... bali kama ni vita basi watu wangekuwa wanapigana hv sasa kutokana na Madhambi yanayo tendeka na baadhi ya viongozi ambao wanajiona kuwa wao ndio wameiteka hii nchi, na kulindwa na chama ambacho kipo madarakani. Na hao kupelekea Mtanzania wakawaida kutothaminiwa...

CCM walishazoe baada ya uchaguzi, vyama vya siasa vya upinzani zinakuwa kimya..na wao kuchukulia ndio point kubwa kwa wao kuendelea kushinda...Eti "vyama vya upinzani havina dira" Sasa chadema wanaendeleza moto wao waliounza tokea kipindi kile....wao wanasema ni uchochezi na wanataka kupindua nchi.

Hata kipindi kile Baba wa Taifa alivyo kuwa ana likomboa taifa hili kutoka kwa wakoloni, alifanya kazi ya kuelimisha na kuwaeleza wananchi tushikamane na kujitoa mikononi mwa wakoloni. Kwani hali ya wananchi hakuwa nzuri.

Hivyo hivyo ndicho kinachofanyika kwa chadema hivi sasa...kuwaelimisha na kuwaeleza wananchi...ili wananchi wawaelewe na kufanya mabadiliko mnamo Mwaka 2015.

Ni hayo....

Mawazo yangu...
 
kila mtu anatetea kitumbua chake,lakini maneno ya sumaye ni ujumbe uliojtosheleza.
 
Jamani Sumaye amewapa CCM ushauri mzuri sana,wajibu hoja sio blaa blaa,watanzania sio vihiyo wala vichaa kama sio mabumbuwazi wa kukubali kurubuniwa na viongozi wa CDM kuandamana bila sababu za msingi,wanaitambua serikali ya CCM vyema,ni wapi imewatoa,wapi imewafikisha na wapi inatarajia kuwapeleka,kama CCM ingekuwa inatekeleza sera zake kwa manufaa ya umma na mtanzania mmoja mmoja katu wananchi wasingekubali kuandamana,sasa wajiulize ni kwa nini wanakubali kuandamana,inabidi wakubali udhaifu na wachape kazi kwa maslahi ya nchi watatue matatizo ya wananchi waache porojo,Dr slaa hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke!!!!!!!!!!
 
kila mtu anatetea kitumbua chake,lakini maneno ya sumaye ni ujumbe uliojtosheleza.

NA DPP alidai Kagoda haishtakiki, mbona kampuni ya Quality Finance imepeleka kesi ya kumdai Kagoda mahakamani?

NI MENGI MNO YA MSINGI CDM INASIMAMIA
 
Naunga mkono mkuu, CCM walishazoa vyama dhaifu vinaonekana vinauhai wakati wa uchaguzi tu ,sasa CDM na stratagy ya hakunakulala ni kuchapa kazi katika kuonyesha madudu ya serikali na uwajibikaji sasa ccm wanaogopa kwani huu moto wa chadema ni mkali sana, na kwakuwa ccm wameishiwa hoja ya kuuzima wanasingizia amani na wanajenga mazingira ya kibabe kutaka kukidhibiti na jinsi tunavyokwenda huko mbele dola itangilia kati na kudhofisha CDM.

Ushauri.
Chadema lazima wajipange kubadilisha mbinu za upambanaji kadri mazingira yatakavyoruhusu mfano kumobulize watu wafungue matawi kakatika kila wilaya na na kuwalika vionguzi wa juu kuja kuyafungua, pia kuwatumiwa vingoozi wa wilaya katika kuanzisha matawi na kuwa karibu na wanachama wa eneo lao.
Pia kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua mara ikibainika kuwapo kwa mamluki na wasaliti ndani ya chama , jua hali hii imejitokeza sana kipindi cha uchaguzi na ikiachiwa itastawi na kuwa tatizo
 
Kwa kila CCM itakacho kifanya dhidi ya Chadema au uongozi wake ndivyo watakavyowazidishia umaarufu.
Haki inayodaiwa ni ndogo sana. JK ni rais tena analindwa vibaya sana na katiba iliyopo, hivyo swala hapa ni kuwachukulia hatua tu viongozi wenzake waliotufikisha hapa. Maandamano ya Chadema yanatokana na kundi dogo na wahuni wachache sana ndani ya chama chao.
Swala la Dowans, wananchi wasikilizwe kama alivyowaahidi wananchi mwaka jana akisema ni swala la muda tu watalisahau.
Mafisadi kama RA na EL awaambie jamani eeeh mmeisha chuma vya kutosha nendeni Pemba au Ukerewe mkajipumzishe maanake hapa sii tu mnanivurugia jina langu ila mnakisambaratisha chama pia..
Kwa uchache huu tu, CCM itaweza kurudisha tumaini la wananchi kwao lakini wakiendelea kukumbatia udikteta kama kina Mubarak hauwezi kuwasaidia kwa lolote maanake itafikia hata wanachama wa CCM wenyewe watachoka na ufisadi unaondelea ukilindwa na dola.. Sasa sielewi, hivi kweli makosa yatakuwa ya Chadema au CCM wenyewe..
Mimi nasema hivi ikiwa hofu ya JK ni huko nyuma ktk ushirika wake na RA, na hata kama RA atamhusisha JK na lolote lile ndio kinga ya RA na EL kumfunga kamba ya mbuzi shingoni...mbinu hii haina mvuto kwa wadanganyika kwani sisi wepesi sana wa kusamehe.
JK analindwa na katiba iliyopo na kwa kumtosa RA na EL, bunge haliwezi kumwadhibu kama vile wananchi watakavyo waadhibu wote siku ya siku.. chief in command
Mkuu,
Mbinu za ccm zimeaanza kufanikiwa...Umeshaanza kuwaita Dkt Slaa na Mbowe wahuni.
 
Kwa kweli, CDM ndiyo chama pinzani pekee ambacho kinaonekana kuwa ni mpinzani wa kweli. Aidha, ni chama ambacho, dola imeshindwa kukiwekea mamluki wa kukimaliza. Hivyo, ni vema viongozi wake wawe makini. Hasa, kuwaangalia kwa karibu viongozi wa chama ambao hawaeleweki eleweki ama msimamo wao ni kujipendekeza kwa sisiem. ni vizuri wawe makini nao.
 
Sielewi ni kwanini Dr. Slaa ana hofu ya Chadema kuadhibiwa, sielewi hii hofu yake inatoka wapi?
Tafuta kwenye threads nyingine viongozi walichosema dhidi ya maandamano hasusani Pinda na Tendwa au ni unazi unakusumbua.
 
Watumie akili sio kukurupuka kufuta chadema madhara yake ni makubwa mno kuliko wanavo fikiria
 
Rais wa Moyoni wa Watanzania waliochakachuliwa Maisha.KAMA KUNA MTANZANIA ANABISHA AJARIBU.DR SLAA SIYO MNAFIKI NA HUWA AMUMUNYI MANENO.
 
CDM wametuamsha ktk mengi: EPA, Meremeta, etc
CCM na vibaraka wake m*@k0 yanalia mbwata!
 
Dola imeshindwa kutumia mamluki wa ndani. Lakini hawajakata tamaa. Hivi sasa wameuagiza tendwa atishie nyau. Hili nalo litashindwa.
 
hakili ni nywele kila mtu anazake! kwa kuwa wapambe wapo Dr slaa atavimba kichwa na kujiona shujaa,haya mshangilieni.
<br />
<br />

Mbona wananchi wapo tayari kwa lolote! Uwezi kujiuliza leo mkuu wa nchi anatoa tamko, kesho yake wananchi wanafurika barabarani kuandanama. Ugumu wa maisha walonayo wananchi huwezi kuwanyamazisha kwa porojo, ukilazimisha wanyamaze mawe yataandamana badala yake.
 
CCM inasababisha umwagaji wa damu kila siku Watanzania kufa mahospitalini kwa maelfu bila tiba shauri chama hiki kimefungua mdomo mpana sana kwa ajili ya UFISADI.

Muda wa kuondolewa madarakani kwa nguvu ya umma baada ya uchakachuaji wote ndio huu umewadia!!
 
Uko sawa kabisa Kanyasu.
Watu badala ya kuwashangilia mashujaa kama Chiligati, Makamba, Wasira au Pinda wanamshangilia Slaa.

Tanzania zaidi ya uijuavyo!!!

Dah! Hii kali sana eti Chiligati, Makamba na Pinda nao wanastahili kuitwa mashujaa! Kwa lipi hasa waliloifanyia nchi yetu hata wastahili kuitwa mashujaa!?...kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya firauni.
 
Back
Top Bottom