Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

umeona eeh? Ccm hoja zao dhaifu sana. Ni kama mtu aliyevaa kaptula kichwani na kuacha utupu nje halafu anamcheka alovaa kaptula kiunoni. Hahaaa, pole Ritz.

Hoja ya chadema ni ipi zaidi ya kurukia hoja za CCM?
 
Mnajidanganya,hapo hakuna ukweli wowote mnaanzisha mada kupotosha umma,mnapewa semina kuingia kwenye mitandao ya jamii kuficha maovu ya chama chenu CDM,mtoa maada tunaomba mtupe safu ya uongozi wote wa Chadema pale makao makuu ,taja majina yao,makabila yao na dini zao alafu pia tunaomba mtuambia hiyo safu ya uongozi wa CDM imepatikanaje je zilipigwa kura na wakina nani wakati gani au walijiteua? Na kwa nini chadema haitaki kufanya uchaguzi wa uongozi wake wa juu kuanzia mwenyekiti wao mnateuana tu? Mtupe majibu hayo vinginevyo ata mjitete vipi kwa semina zenu za uchochoroni hatuwaelewi ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu!
 
CHADEMA ni jitahida za WAKRISTO kutaka kuhodhi madaraka yote nchini! Wamenufaika sana na CCM sasa wameanzisha upinzani pia! CCM na CDM ni baba mmoja mama mmmoja! Ona wanavyokubaliana katika kila issue DHIDI ya Waislamu Tanzania! Kama kuna muislamu CHADEMA ni MURTAD!

Wewe hutufai kabisa humu jamvini,
story zako za kwenye gahawa unatuletea JF,
hebu potea na udini wako hapa.
 
CHADEMA ni jitahida za WAKRISTO kutaka kuhodhi madaraka yote nchini! Wamenufaika sana na CCM sasa wameanzisha upinzani pia! CCM na CDM ni baba mmoja mama mmmoja! Ona wanavyokubaliana katika kila issue DHIDI ya Waislamu Tanzania! Kama kuna muislamu CHADEMA ni MURTAD!

Makamu wawili wa m/kiti wa cdm, naibu katibu mkuu wa cdm yaani akina Said Arfi, Zitto, na makamu m/kiti Z'bar wote ni viongozi wa ngazi ya juu kabisa ya cdm na ni waislam! Prof. Abdalah Safari ni mwislam safi. Au mwislam hadi awe sheikh au imam? Peleka ujinga wako huko!
 
Mkuu mbona hilo linajulikana toka kitambo tu, hawana CD yoyote wanatapatapa tu
Walikuja na yule mama wa Igunga aliyevuliwa kilemba, baadae wakakuta kumbe ni Mkatekista, Wakaumbuka. Mtaji mkubwa wa Magamba ni Ujinga na Umasikini wa Watanzania, kwa hiyo hawatakaa wayamalize matatizo haya.
 
Marehemu Brown Ngwilupipi anatoka Mbeya sio Iringa, umenukuu wapi hii taarifa yako yote inaweza kuonekana ya uongo kama huzingatii kuondoa makosa madogodogo kama haya

Habari za utokako mama,ulipotea sana tangu tulivyoasisi M4c sijakuona kabisa jamvini.
 
Bob Nyanga Makani ni mmoja wa waasisi wa CHADEMA, ni Msukuma, Mwislamu kutoka Kutoka Shinyanga na katibu mkuu wa Kwanza wa CHADEMA.

Katibu mkuu ndiye mwenye siri zote Chama, ndiyo anakaa na mafaili yote, ni mwajiri wa wafanya kazi wa makao makuu nk.

Nimejifunza mambo yafuatayo.
Mosi, Kama waanzilishi wa CHADEMA wangekuwa na agenda udini wasingemchagua Bob Makani kwa sababu yeye ni Mwislamu. ( Binafsi nimejua dini yake wakati wa msiba)

Pili kama waasisi wa CHADEMA wangekuwa wanaagenda ya Ukanda wasingemchagua Bob Makani kwa sababu hatoki kanda ya kaskazini.
Tatu, Kama waasisi wangekuwa na agenda ya ukabila wasingemchagua Bob Makani kwa sababu si Mchaga.

Kitendo cha kumchagua Msukuma, Muislamu, kutoka kanda ya Shinyanga katibu mkuu na baadaye kuongezewa cheo na kuwa Mkiti ina maanisha kuwa alifanya kazi vizuri na alikuwa anakubalika na wajumbe wote bila kujali dini, ukanda wala ukabila.

Wale waliokuwa wanacheza CD ya udini, ukanda na ukabila dhidi ya CHADEMA sasa inabidi watafute CD nyingine ya kucheza dhidi CHADEMA vinginevyo hii ya Ukanda, . ukabila na udini sasa zimechuja. Haiuziki tena.

Ni mawazo yangu tu.
Sasa hivi Nape ameanza na CD ya uchangishaji wa pesa tunapokuwa mikutanoni. Eti kwa nini wananchi wa hali ya chini wanachangishwa na CHADEMA mikutanoni. Hili nalo bado la kifala.
 
Makamu wawili wa m/kiti wa cdm, naibu katibu mkuu wa cdm yaani akina Said Arfi, Zitto, na makamu m/kiti Z'bar wote ni viongozi wa ngazi ya juu kabisa ya cdm na ni waislam! Prof. Abdalah Safari ni mwislam safi. Au mwislam hadi awe sheikh au imam? Peleka ujinga wako huko!

Mjinga wewe unaelishwa sumu kwenye semina zenu uchochoroji kwa ajili ya kuingia kwenye mitandao ya jamii kwa ajili ya kuwadanganya watanzania na kuficha maovu na upuuzi uliomo Chadema!
 
Hoja dhaifu sana wangemchagua vipi wakati yeye ndio muasisi wa Chadema kajipange upya mkuu.

Viongozi wa kwanza baada ya chama kuasisiwa. Hapo utagundua CHADEMA hakuna udini, ukabila wala ukanda. wacha wenge weweeeeee!!!!!!

1.Ndg. Edwin Isaac Mbiliewi MteiMwenyekiti - Arusha
2.Ndg. Ali Suleiman AhmedMakamu mwenyekiti (visiwani) - zanziba
3.Ndg. Brown NgwilulupiMakamu Mwenyekiti (bara)
4.Ndg. Bob Nyanga MakaniKatibu Mkuu - Shinyanga
5.Ndg. Mustafa. S. SimbaNaibu Katibu Mkuu (visiwani) - Pwani
6.Ndg. Eric Rashid MchattaNaibu Katibu Mkuu (bara) - Mara
7.Ndg. Eric Rashid MchattaKatibu Mwenezi

CHADEMA ni jitahida za WAKRISTO kutaka kuhodhi madaraka yote nchini! Wamenufaika sana na CCM sasa wameanzisha upinzani pia! CCM na CDM ni baba mmoja mama mmmoja! Ona wanavyokubaliana katika kila issue DHIDI ya Waislamu Tanzania! Kama kuna muislamu CHADEMA ni MURTAD!

hebu angalia vizuri hapo
Viongozi wa Kitaifa

free_sk.jpg
Mwenyekiti
Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe (51)
Kutoka Hai, Kilimanjaro
freeman@chadema.or.tz

Makamu Mwenyekiti Bara
Mhe. Said Amour Arfi (57)
Kutoka Mpanda, Rukwa
arfi.gif

blank.gif
Makamu Mwenyekiti Zanzibar
Mhe. Said Issa Mohammed (37)
Kutoka Pemba

Katibu Mkuu
Mhe. Willibrod Peter Slaa (63)
Kutoka Karatu, Arusha
slaa_sk.jpg

zito_sk.jpg
Naibu Katibu Mkuu - Bara
Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (36)
Kutoka Mwandiga, Kigoma Kaskazini
zitto@chadema.or.tz

Naibu Katibu Mkuu - Zanzibar
Mhe. Hamad Mussa Yussuf (34)
Kutoka Kaskazini Pemba
hamad_sk.jpg

Hawana cd nyingine tena ya kurusha, waangalie plan b kama kawaida yao.
 
Nadhani ccm inadhani bado ipo na watu wa kale wa kudanganywa pengine kwa sababu wengi walikuwa hawana elimu walidanganyika kwa urahisi ila kwa sasa wanaitaji wafanye kazi kweli kweli sio kuja na hoja nyepesi nyepesi kama ukabila, udini n.k wakadhani watu awaoni au awafuatilii mambo kwa ukaribi. Na kwanini kabla ya cdm ijawatishio kwao walikuwa awaongei hayo? Wajuwe kwanza cdm ndio chama chenye wasomi wengi zaidi. Wabishe................
 
Hoja dhaifu sana wangemchagua vipi wakati yeye ndio muasisi wa Chadema kajipange upya mkuu.

Ni lini alikiuza chama kwa wachaga, Hivi kabla hamjaanza propaganda zenu za UDINI mlifanya baseline survey kujua CDM ina wanachama wangapi na sasa mmefnya reserach kujua ina wangapi ili kuases impact mkuu?
 
Sasa hivi Nape ameanza na CD ya uchangishaji wa pesa tunapokuwa mikutanoni. Eti kwa nini wananchi wa hali ya chini wanachangishwa na CHADEMA mikutanoni. Hili nalo bado la kifala.

Hatushangahi wanachama wa chadema na viongozi wenu kuwa na lugha chafu,matusi,jazba ,kutokuwa na busara na hekima ndiyo jadi yenu tunamshukuru mungu watanzania wanawaelewa ndiyo maana hawawapi madaraka ya kushika nchi!
 
Nilichojifunza kumbe CDM wanapokuwa na majibu wanahifadhi huku wakisubiri muda muafaka, mimi nadhani wameyatoa muda mufaka maana chama tayari kimekubalika na sasa ndiyo wanafanya kwa vitendo kukanusha ukanda udini na ukabila.Hongera kamanda Mbowe kwa kuweka hadharani orodha fupi lakini ya watu makini.Hongera Mukama wa ccm kwa kukurupuka na NITOKE VIPI YAKO ya upotoshaji
Ni kweli mkuu Chadema hawakupenda kupoteza muda mrefu kwaajili ya kubishana na kitu kilicho wazi wamesubiri CCM yote ipo pale wakasema badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari hata huku jamvini imeisha nguvu kabisa anayeishabikia ni kichaa zombi tuu
 
Ni timing ya aina yake.Japo ni katika tukio lisilotarajiwa la kufiwa na mpendwa wetu
 
Nadhani ccm inadhani bado ipo na watu wa kale wa kudanganywa pengine kwa sababu wengi walikuwa hawana elimu walidanganyika kwa urahisi ila kwa sasa wanaitaji wafanye kazi kweli kweli sio kuja na hoja nyepesi nyepesi kama ukabila, udini n.k wakadhani watu awaoni au awafuatilii mambo kwa ukaribi. Na kwanini kabla ya cdm ijawatishio kwao walikuwa awaongei hayo? Wajuwe kwanza cdm ndio chama chenye wasomi wengi zaidi. Wabishe................

Acha uongo gwanda wewe,tupe data tujiridhishe kwa sababu maprofesa na madokta lukuki wamejaa CCM,mfano angalia safu za mawaziri hapo hujaangalia wanachama wake! Kwa huo ndiyo uongo mnaofundishwa kwenye semina zenu kwa ajili ya kupotosha umma wa watanzania uzuri wake watanzania wanawajua vizuri mnatwanga maji kwenye kinu!
 
CHADEMA ni jitahida za WAKRISTO kutaka kuhodhi madaraka yote nchini! Wamenufaika sana na CCM sasa wameanzisha upinzani pia! CCM na CDM ni baba mmoja mama mmmoja! Ona wanavyokubaliana katika kila issue DHIDI ya Waislamu Tanzania! Kama kuna muislamu CHADEMA ni MURTAD!
Utapiamlo wa akili mbaya sana yaani ukiwa na hasira kila mtu ni adui yako!. Ndugu yangu huridhiki na lolote!! Hata JMK kuwa Rais wako! na mwenyekiti wa CCM unahisi anaendesha mfumo Kristo! Hata Shein anayeongoza Zanzibar anaongozwa na mfumo Kristo! Hata Makamu wa Rais anaongozwa na mfumo Kristo.
Sawa mfumo ni tofauti na watu lakini watu ndio hutengeneza mifumo. Unataka nini sasa wewe ndugu sema! Tuwaue wakristo wote ili waislamu wapate huduma zote muhimu hasa baada kujua idadi yao?
Tufanye jitahada za makusudi kuhakikisha waislamu wengi wanasoma na wakristo hawasomi ili kubalance!!
Tubadilishe Hadidu za rejea za Ajira ili kuhakikisha sifa moja wapo "DINI GANI?"!!
Inaudhi sana kwa kweli.
 
Back
Top Bottom