Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

hoja dhaifu sana katika kujenga hoja tupeni sasa hivi hali ipo vipi kuanzia ngazi ya juu,wabunge bila kusahau wa viti maalumu na viongozi wengine.wakati wa kuanzisha hao jamaa wa chini ya mlima kilimanjaro walikuwa wanajaribu baada ya kuona sasa biashara imechanganya wakachukuwa mradi wao,mfano cuf mwanzilishi ni james mapalala,lakini nani anabisha kwamba cuf si ya udini ?
 
Mimi nilichojifunza kutokana na msiba wa Bob Nyanga Makani, mjukuu wa chifu Makwaiya ni kwamba CHADEMA huwa hawkurupuki na hoja nyepesi zinazotolewa na wapinzani ccm,matukio mawili yanatukumbusha mengi;

kwanza
Kumbe CHADEMA waanzilishi wake walipatikana kutoka kila kanda kuu za tanganyika yaani kanda ya ziwa ya kusini ya magharibi, na ya mashariki kama ifuatavyo;
o Edwin Mtei (Arusha),
o Makani (Shinyanga),
o Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
o Edward Barongo (Kagera),
o Mary Kabigi (Mbeya),
o Menrad Mtungi (Kagera),
o Costa Shinganya (Kigoma),
o Evalist Maembe (Morogoro) na
o Steven Wassira (Mara).

PILI
Kumbe CHADEMA si chama cha wachaga kama tulivyoaminishwa na wapinzani, kwani mchaga katika kundi la waanzilishi (WAASIS) ni mzee mtei peke yake.Kumbe influence ya mzee mtei kutokana na CV yake na exposure yake iliwachanganya ccm WAKADHANI NI CHAMA CHA WACHAGA.
Asanteni sana watoa taarifa za waasisi
Washindwe ccm na wakauke.

Brown Ngwilulupi ni Mbeya siyo Iringa!
 
Ila udini upo ndani ya CHADEMA upo ,hilo valangati kuwa Makani na wengine ni waislamu halina mshiko kwani hata bunge linaongozwa kidini asilimia ndogo sana ni waislamu angalia hata safu ya mawaziri ,kwa nini usiwepo iwiano.

CDM kina udini hilo halina upinzani,mtabakia kutetea tu kama kuku aliekosa sehemu ya kutagia.Naona mnafananisha mchana na usiku ,kisa mmeona mwezi.
 
Hakuna ukabila, ukanda, wala udini hapo! Tatizo ni la ccm kuogopa kupokwa madaraka.
 
ndugu yangu ritz huo uchaga munaousimamia unatokana na nini ? hasa ukiangalia safu ya waanzilishi na uongozi uliopo unaweza kujustify kivipi kuwa ni chama cha kichaga au kikanda.?
Mbona uongozi wa serikali kuu ya ccm hatuisema ni ya kidini (kiislamu) hata baada ya wafuatao kushika nafasi zote muhimu za juu? Rais-mwislamu. makamu-mwislamu. jaji mkuu-mwislamu. mkuu wa polisi-mwislamu.rais na makamu wote wa zanzibar ni waislaamu. VS spika -mkristo. Waziri mkuu-mkristo.

Kwa uelewa wangu ninajua wote walioshika nafasi ni kutokana na uwezo wao na sio kigezo cha udini na ukabila.
Mimi ninafikiri mtafute sababu nyingine siyo hizo.

Hoja dhaifu sana wangemchagua vipi wakati yeye ndio muasisi wa Chadema kajipange upya mkuu.
 
:A S 465:
Ni kweli mkuu, hii hoja ya ukabila, udini, na ukanda haina mashiko ndani ya Chadema leo! Ni propaganda za kitoto ambazo hazihitaji mtu kwenda shule kuzitegua na kuzidharau! Hata mimi sikuwahi kujua kuwa Kamanda Bob Mohamed Nyanda Makani alikuwa muislamu, nimekuja jua wakati wa msiba wake! CHADEMA leo, iko kusini mpaka kaskazini, magharibi mpaka mashariki, pembezoni mpaka kitovuni mwa Tanzania! Ni moto wa kifuu, siyo rahisi kuuzima kwa propaganda chapwa za udini, ukanda na ukabila tena!

Bob Nyanga Makani ni mmoja wa waasisi wa CHADEMA, ni Msukuma, Mwislamu kutoka Kutoka Shinyanga na katibu mkuu wa Kwanza wa CHADEMA.

Katibu mkuu ndiye mwenye siri zote Chama, ndiyo anakaa na mafaili yote, ni mwajiri wa wafanya kazi wa makao makuu nk.

Nimejifunza mambo yafuatayo.
Mosi, Kama waanzilishi wa CHADEMA wangekuwa na agenda udini wasingemchagua Bob Makani kwa sababu yeye ni Mwislamu. ( Binafsi nimejua dini yake wakati wa msiba)

Pili kama waasisi wa CHADEMA wangekuwa wanaagenda ya Ukanda wasingemchagua Bob Makani kwa sababu hatoki kanda ya kaskazini.
Tatu, Kama waasisi wangekuwa na agenda ya ukabila wasingemchagua Bob Makani kwa sababu si Mchaga.

Kitendo cha kumchagua Msukuma, Muislamu, kutoka kanda ya Shinyanga katibu mkuu na baadaye kuongezewa cheo na kuwa Mkiti ina maanisha kuwa alifanya kazi vizuri na alikuwa anakubalika na wajumbe wote bila kujali dini, ukanda wala ukabila.

Wale waliokuwa wanacheza CD ya udini, ukanda na ukabila dhidi ya CHADEMA sasa inabidi watafute CD nyingine ya kucheza dhidi CHADEMA vinginevyo hii ya Ukanda, . ukabila na udini sasa zimechuja. Haiuziki tena.

Ni mawazo yangu tu.
 
Mbona uongozi wa serikali kuu ya ccm hatuisema ni ya kidini (kiislamu) hata baada ya wafuatao kushika nafasi zote muhimu za juu? Rais-mwislamu. makamu-mwislamu. jaji mkuu-mwislamu. mkuu wa polisi-mwislamu.rais na makamu wote wa zanzibar ni waislaamu. VS spika -mkristo. Waziri mkuu-mkristo.

Kwa uelewa wangu ninajua wote walioshika nafasi ni kutokana na uwezo wao na sio kigezo cha udini na ukabila.
Mimi ninafikiri mtafute sababu nyingine siyo hizo.

Ila udini upo ndani ya CHADEMA upo ,hilo valangati kuwa Makani na wengine ni waislamu halina mshiko kwani hata bunge linaongozwa kidini asilimia ndogo sana ni waislamu angalia hata safu ya mawaziri ,kwa nini usiwepo iwiano.

CDM kina udini hilo halina upinzani,mtabakia kutetea tu kama kuku aliekosa sehemu ya kutagia.Naona mnafananisha mchana na usiku ,kisa mmeona mwezi.
 
Bob Nyanga Makani ni mmoja wa waasisi wa CHADEMA, ni Msukuma, Mwislamu kutoka Kutoka Shinyanga na katibu mkuu wa Kwanza wa CHADEMA.

Katibu mkuu ndiye mwenye siri zote Chama, ndiyo anakaa na mafaili yote, ni mwajiri wa wafanya kazi wa makao makuu nk.

Nimejifunza mambo yafuatayo.
Mosi, Kama waanzilishi wa CHADEMA wangekuwa na agenda udini wasingemchagua Bob Makani kwa sababu yeye ni Mwislamu. ( Binafsi nimejua dini yake wakati wa msiba)

Pili kama waasisi wa CHADEMA wangekuwa wanaagenda ya Ukanda wasingemchagua Bob Makani kwa sababu hatoki kanda ya kaskazini.
Tatu, Kama waasisi wangekuwa na agenda ya ukabila wasingemchagua Bob Makani kwa sababu si Mchaga.

Kitendo cha kumchagua Msukuma, Muislamu, kutoka kanda ya Shinyanga katibu mkuu na baadaye kuongezewa cheo na kuwa Mkiti ina maanisha kuwa alifanya kazi vizuri na alikuwa anakubalika na wajumbe wote bila kujali dini, ukanda wala ukabila.

Wale waliokuwa wanacheza CD ya udini, ukanda na ukabila dhidi ya CHADEMA sasa inabidi watafute CD nyingine ya kucheza dhidi CHADEMA vinginevyo hii ya Ukanda, . ukabila na udini sasa zimechuja. Haiuziki tena.

Ni mawazo yangu tu.

Gurti upo sawa kabisa my best friend. Unajua, wenzetu wa kijani wana hoja mfu, kwa kuwa chama kimekufa. kwa kweli, naishukia CCM mpaka sasa hata mboga za majani kwa kuwa ni za kijani, kila ninapokula sijisikii vizuri, sema ninachoweza kusema, ni kuwa inabidi hata rangi ya kijani wabadilishe.
 
Hoja dhaifu sana wangemchagua vipi wakati yeye ndio muasisi wa Chadema kajipange upya mkuu.

Mficha ficha maradhi kifo kitamuumbua. Agenda ya udini, ukabila ukanda utakuumiza mkuu. HAIUZIKI
 
hoja dhaifu sana katika kujenga hoja tupeni sasa hivi hali ipo vipi kuanzia ngazi ya juu,wabunge bila kusahau wa viti maalumu na viongozi wengine.wakati wa kuanzisha hao jamaa wa chini ya mlima kilimanjaro walikuwa wanajaribu baada ya kuona sasa biashara imechanganya wakachukuwa mradi wao,mfano cuf mwanzilishi ni james mapalala,lakini nani anabisha kwamba cuf si ya udini ?

Na JK kumteua Mbatia ni uchaga na ukaskazini? Haya washikaji wakiislam na vijumba vidogo vya JK ni poa kwa taifa? Ona shemeji yake Hawa Ghasia anavyolikoroga? Vipi Sophia Simba? Mlolomgo wa kishkaji ni mrefu hamuwezi kuwa na jibu la matatizo ya nchi ilimradi maamuzi nyanafanyika kiunoni.
 
Marehemu Brown Ngwilupipi anatoka Mbeya sio Iringa, umenukuu wapi hii taarifa yako yote inaweza kuonekana ya uongo kama huzingatii kuondoa makosa madogodogo kama haya

HIZO NI TYPING ERRA MKUU, lakini hazibadishiu ya maana ya kuwa CDM sio chama cha ukabila, udini na ukanda!
 
Ccm wanafkiri wakituletea agenda eti chadema ina ukabila pamoja na udini eti watafanikiwa kuwashawishi wananchi kukichukia chama chao kizuri na kiadilifu. Nawashauri magamba kuwa watafute plan B manake ni mabongolala na hao wanaokubali kudanganyika ni mabongolala tu.
 
Ila udini upo ndani ya CHADEMA upo ,hilo valangati kuwa Makani na wengine ni waislamu halina mshiko kwani hata bunge linaongozwa kidini asilimia ndogo sana ni waislamu angalia hata safu ya mawaziri ,kwa nini usiwepo iwiano.

CDM kina udini hilo halina upinzani,mtabakia kutetea tu kama kuku aliekosa sehemu ya kutagia.Naona mnafananisha mchana na usiku ,kisa mmeona mwezi.

Hata "bunge" linaongozwa kiudini asilimia ndogo sana ni waislam. Pia "safu ya mawaziri". CDM kina udini hilo halina upinzan.
Mweh. Arguments zingine bana.
 
Acha unafiki wewe gwanda,fuatilia histolia ya prof safari alianza CCM akaenda,cuf nako katimuliwa kwa matendo yake maovu kaja chadema huo ni mfano wa prof wenu mchumia tumbo ukitaka wengine nitakutajia,kwa hilo huna hujanja ata namna ya kuendesha siasa mfumo wa uongozi wa chadema wameiga CCM,sijuhi mwenyekiti,makamu mwenekiti bara na visiwani mmeiga ata mfumo kwa katiba ya CDM ya vijana,wakina mama na chama kwa ujumla mmeiga CCM,mnakopi kila kitu mnajifanya wajanja mnabadili kidogo wenyewe,hamna jipya mlikuka na sera za majimbo mkachemsha leo mmekuja na sera za kutukana na kushambulia watu,mnafanya mikutano badala mmwage sera mnanashambulia watu! Tunawaomba mtoe kitabu kitachoeleza ahadi za wabunge wenu walizotekeleza majimboni kwao toka walipochaguliwa 2010,mtuambie wamefanya lipi toka waingie madarakani siyo mnazunguka tu mikoani kutukana na kushambulia watu kwa hoja zisizo na mashiko!
kumbe panadol ni dawa ya usingizi!!amka wewe gamba!! Hizi bange za UDINI na ukabila mnazolisha watanzania ni bomu litakalowamaliza wenyewe! siye hatupo I swear. Unazungumza KUMWAGA sera. Kweli bangi ya UDINI na Ukabila inawalevya!! Hivi bado huwezi kuchambua ujambazi unaofanywa na MAGAMBA huoni huruma kwa watanzania. Akikosolewa Rais UDINI. Wakiguswa wazanzibar UDINI. Narudia tena MNA UTAPIAMLO WA AKILI. Jitibu kwa kusikiliza na kuchambua sera za CDM - PEOPLES jibu we Gamba sema POWER!!
 
attachment.php
 
1: Lucy owenya ni mbunge viti maalum lakini ni shemeji wa mbunge wa jimbo la moshi mjini (ndesamburo) ambaye pia ni mfadhili mkubwa wa chama hicho.hapa utagundua kuwa cdm imeamua kulipa fadhila kwa mfadhili bila kuangalia usawa wanaoulili,je siyo unafiki?

2: grace kiwelu ndesamburo ni mb viti maalumu na ni mtoto wa ndesamburo.je cdm si ya wachaga?
 
Back
Top Bottom