Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Gurti

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
211
59
Bob Nyanga Makani ni mmoja wa waasisi wa CHADEMA, ni Msukuma, Mwislamu kutoka Kutoka Shinyanga na katibu mkuu wa Kwanza wa CHADEMA.

Katibu mkuu ndiye mwenye siri zote Chama, ndiyo anakaa na mafaili yote, ni mwajiri wa wafanya kazi wa makao makuu nk.

Nimejifunza mambo yafuatayo.
Mosi, Kama waanzilishi wa CHADEMA wangekuwa na agenda udini wasingemchagua Bob Makani kwa sababu yeye ni Mwislamu. ( Binafsi nimejua dini yake wakati wa msiba)

Pili kama waasisi wa CHADEMA wangekuwa wanaagenda ya Ukanda wasingemchagua Bob Makani kwa sababu hatoki kanda ya kaskazini.
Tatu, Kama waasisi wangekuwa na agenda ya ukabila wasingemchagua Bob Makani kwa sababu si Mchaga.

Kitendo cha kumchagua Msukuma, Muislamu, kutoka kanda ya Shinyanga katibu mkuu na baadaye kuongezewa cheo na kuwa Mkiti ina maanisha kuwa alifanya kazi vizuri na alikuwa anakubalika na wajumbe wote bila kujali dini, ukanda wala ukabila.

Wale waliokuwa wanacheza CD ya udini, ukanda na ukabila dhidi ya CHADEMA sasa inabidi watafute CD nyingine ya kucheza dhidi CHADEMA vinginevyo hii ya Ukanda, . ukabila na udini sasa zimechuja. Haiuziki tena.

Ni mawazo yangu tu.
 
Mkuu mbona hilo linajulikana toka kitambo tu, hawana CD yoyote wanatapatapa tu
 
Ndugu mwenye macho haambiwi ona ni magamba tu yana haha kamba mbwa aliye pigwa mawe kifupi hawana hoja,wanatumia mbinu walizotumia kuiua cuf wanafikilia watawaweza watanzania walioamua kiwakataa
 
Mimi nilichojifunza kutokana na msiba wa Bob Nyanga Makani, mjukuu wa chifu Makwaiya ni kwamba CHADEMA huwa hawkurupuki na hoja nyepesi zinazotolewa na wapinzani ccm,matukio mawili yanatukumbusha mengi;

kwanza
Kumbe CHADEMA waanzilishi wake walipatikana kutoka kila kanda kuu za tanganyika yaani kanda ya ziwa ya kusini ya magharibi, na ya mashariki kama ifuatavyo;
o Edwin Mtei (Arusha),
o Makani (Shinyanga),
o Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
o Edward Barongo (Kagera),
o Mary Kabigi (Mbeya),
o Menrad Mtungi (Kagera),
o Costa Shinganya (Kigoma),
o Evalist Maembe (Morogoro) na
o Steven Wassira (Mara).

PILI
Kumbe CHADEMA si chama cha wachaga kama tulivyoaminishwa na wapinzani, kwani mchaga katika kundi la waanzilishi (WAASIS) ni mzee mtei peke yake.Kumbe influence ya mzee mtei kutokana na CV yake na exposure yake iliwachanganya ccm WAKADHANI NI CHAMA CHA WACHAGA.
Asanteni sana watoa taarifa za waasisi
Washindwe ccm na wakauke.
 
Kuna kanuni moja ya kumtambua mtu ambaye ni mbaguzi. Inasema hivi: Yeyote anayekuwa wa kwanza kuzungumzia udini ama ukabila ndiye mdini na mkabila namba moja. Anaujuaje?
 
Nilichojifunza kumbe CDM wanapokuwa na majibu wanahifadhi huku wakisubiri muda muafaka, mimi nadhani wameyatoa muda mufaka maana chama tayari kimekubalika na sasa ndiyo wanafanya kwa vitendo kukanusha ukanda udini na ukabila.Hongera kamanda Mbowe kwa kuweka hadharani orodha fupi lakini ya watu makini.Hongera Mukama wa ccm kwa kukurupuka na NITOKE VIPI YAKO ya upotoshaji
 
CHADEMA ni jitahida za WAKRISTO kutaka kuhodhi madaraka yote nchini! Wamenufaika sana na CCM sasa wameanzisha upinzani pia! CCM na CDM ni baba mmoja mama mmmoja! Ona wanavyokubaliana katika kila issue DHIDI ya Waislamu Tanzania! Kama kuna muislamu CHADEMA ni MURTAD!
 
Kuna vyama vya siasa tangu kuanzishwa kwake havijawahi kumbadilisha mwenyekiti au mgombea wao wa uraisi,au akihama chama aendako ni lazima awe mwenyekiti, CDM nadhami ndiyo chama pekee kilichofanya uchaguzi na kibadilisha viongozi tulisha fikia kuwa na wenyeviti watatu,makatibu wakuu sina uhakika vizuri ila na wajua wawili, na viongozi wote hawa ni dini mbali mbali na makabila tofauti.Je CDM ingekuwa kama hivyo vyama ambavyo havibadilishi viongozi leo hii wangekuwa wanaongelea nini? ikiwa tumesha fanya yote hayo na bado yanazungumzwa yale yale kila siku? CDM muasisi wake mkuu ni mchaga/mkistona wengineo kama akina makani, kama usipo kubalika nyumbani kwako ni rahisi kukubalika kwa mwenzako ?
 
Unaongelea waanzilishi wakati yeye ni mwanzilishi mmoja wapo? sijui mnajuwa mnachokiongea au mnakurupuka tu.

Hata harakati za kudai uongozi wa wenyewe kwa nchi hii ulianzishwa na Waislaam, hata TANU ilianzishwa na Waislaam. Tatizo nini?
 
Unaweza kuanzisha na ukashindwa kukiendeleza.hilo ni tatizo kubwa
 
Mimi nilichojifunza kutokana na msiba wa Bob Nyanga Makani, mjukuu wa chifu Makwaiya ni kwamba CHADEMA huwa hawkurupuki na hoja nyepesi zinazotolewa na wapinzani ccm,matukio mawili yanatukumbusha mengi;

kwanza
Kumbe CHADEMA waanzilishi wake walipatikana kutoka kila kanda kuu za tanganyika yaani kanda ya ziwa ya kusini ya magharibi, na ya mashariki kama ifuatavyo;
o Edwin Mtei (Arusha),
o Makani (Shinyanga),
o Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
o Edward Barongo (Kagera),
o Mary Kabigi (Mbeya),
o Menrad Mtungi (Kagera),
o Costa Shinganya (Kigoma),
o Evalist Maembe (Morogoro) na
o Steven Wassira (Mara).

PILI
Kumbe CHADEMA si chama cha wachaga kama tulivyoaminishwa na wapinzani, kwani mchaga katika kundi la waanzilishi (WAASIS) ni mzee mtei peke yake.Kumbe influence ya mzee mtei kutokana na CV yake na exposure yake iliwachanganya ccm WAKADHANI NI CHAMA CHA WACHAGA.
Asanteni sana watoa taarifa za waasisi
Washindwe ccm na wakauke.

Umesema kweli. Lakini si unajua CCM inakwea mnazi ilhali imevaa msuli!
 
wataleta sababu ingine,kama wao ndani kwa ndani wanabaguaa,utasikia flani sio mtanzani,kwa sababu tu amekizidi hoja,ili kumharibia unamtangazia kuwa sio raia.nakumbuka 2005 kuna mzee mmja alikuwa akiwania kuwa raisi na alitokea visiwani zanziba,kashfa aliyoundiwa na wenzake,hana hamu ya siasa kabisa,mzee wa watu,nilimuonea huruma,inawezekana kama angepewa hiyo nafasi ya kuchaguliwa kuwa raisi,may be mabo yasingekuwa yalivyo.lakini ufisadi na tamaa za madaraka zilimfanya ashindwe kuwatumikia wa tz.dhambi ya ubaguzi itawamaliza nyinyiemu.
 
Hoja dhaifu sana wangemchagua vipi wakati yeye ndio muasisi wa Chadema kajipange upya mkuu.

umeona eeh? Ccm hoja zao dhaifu sana. Ni kama mtu aliyevaa kaptula kichwani na kuacha utupu nje halafu anamcheka alovaa kaptula kiunoni. Hahaaa, pole Ritz.
 
Unaweza kuanzisha na ukashindwa kukiendeleza.hilo ni tatizo kubwa

Na ndio tatizo hilohilo alikuwa nalo Nyerere alikuwa ndio wa mwanzo kuwa Rais wa nchi hii tena kwa muda wa miaka 24 akashindwa kila nyanja akatuwacha masikini wa mwisho duniani.
 
Mimi nilichojifunza kutokana na msiba wa Bob Nyanga Makani, mjukuu wa chifu Makwaiya ni kwamba CHADEMA huwa hawkurupuki na hoja nyepesi zinazotolewa na wapinzani ccm,matukio mawili yanatukumbusha mengi;

kwanza
Kumbe CHADEMA waanzilishi wake walipatikana kutoka kila kanda kuu za tanganyika yaani kanda ya ziwa ya kusini ya magharibi, na ya mashariki kama ifuatavyo;
o Edwin Mtei (Arusha),
o Makani (Shinyanga),
o Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
o Edward Barongo (Kagera),
o Mary Kabigi (Mbeya),
o Menrad Mtungi (Kagera),
o Costa Shinganya (Kigoma),
o Evalist Maembe (Morogoro) na
o Steven Wassira (Mara).

PILI
Kumbe CHADEMA si chama cha wachaga kama tulivyoaminishwa na wapinzani, kwani mchaga katika kundi la waanzilishi (WAASIS) ni mzee mtei peke yake.Kumbe influence ya mzee mtei kutokana na CV yake na exposure yake iliwachanganya ccm WAKADHANI NI CHAMA CHA WACHAGA.
Asanteni sana watoa taarifa za waasisi
Washindwe ccm na wakauke.

Marehemu Brown Ngwilupipi anatoka Mbeya sio Iringa, umenukuu wapi hii taarifa yako yote inaweza kuonekana ya uongo kama huzingatii kuondoa makosa madogodogo kama haya
 
Back
Top Bottom