DC Bukoba aamuru walimu wachapwe mboko!

wana JF,
Nafikiri tatizo kubwa la Tanzania ni kukosa MAFIA. Mafia iliyoiba sana na ku-invest Tanzania. Mafia wanaoona kuwa Tanzania ni yao. Mafia wanaotakiwa kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa. Watu hao wangelikuwa wanashughulikia maswala madogomadogo ambayo kwa kweli yanaleta kero. Maswala hayo mara nyingi serikali inakuwa inajifanya haioni ila yanaleta madhara yasiyotakiwa kuwepo nchini.
Kama wangelikuwepo nafikiri ingelibidi wadeal na RA kwanza. Huyu anatakiwa aonyeshwe Tanzania ina wenyewe. Pia wanakuja kwenye watu kama Wauwa Ma-albino. Maadamu serikali inasuasua, hawa jamaa wanaingia kazini na kufanya yale Pinda kasema. Mafisadi wote wanaoibia nchi na kupeleka pesa nje, hawa nao inabidi washughulikiwe. Mwisho wanaweza kuwa wanadeal hadi na watu kama huyu DC. Huyu anatekwa na yeye anatandikwa fimbo barabara na picha zinapelekwa kwa Waalimu na wao wajue kuwa mbaya wao na yeye kakipata. Ila ndiyo upuuzi wa vyeo vya KUZAWADIWA. Kibaya ni kuwa hata kumuondoa unakuta kazi maana MIJITU kama hii ina MGONGO huooo!!!
 
Originally Posted by Eeka Mangi
Hii imetulia sanaaa. Walimu wetu nao wamebweteka sana. Anyway hata Julius Nyerere aliwahi kumchapa waziri wake sembuse mwalimu? Mzee Mkuu Wa Wilaya wakirudia tena kutufanya tuwe wa mwisho tunawapa mboko mbele ya wanafunzi wao. BIG UP DC

I did not expect this disappointing comment from Eeka Mangi!

Hata mimi pia sikutegemea! Inahuzunisha kweli kweli!
 
Last edited:
"Ni kweli kuna tukio la aina hiyo na nimeshamwagiza mkuu wa mkoa kufanya uchunguzi na endapo ukweli utapatikana, serikali itachukuwa hatua kali dhidi ya wahusika," alisema Profesa Magembe na kuongeza:

"Nchi yetu haiwezi kuongozwa na watu wa aina hiyo na kamwe serikali haiwezi kukaa kimya... mara tu baada ya mkuu wa mkoa kumaliza kazi yake, atatuletea taarifa na sisi tutalifikisha kwa waziri mkuu kwa hatua zaidi kwani hao wote wako chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu".

Ni Tanzania tu ndio kuna maajabu kama haya. Prof. Maghembe anasema amemuagiza Mkuu wa Mkoa kuchunguza. Mkuu wa Wilaya alishakiri kwamba ni kweli aliwacharaza viboko hao walimu na akatoa sababu za kufanya hivyo. Sasa hapo kuna uchunguzi upi unaotakiwa kufanyika.

Tukio kama hili linafungua macho ya wananchi na kutuonyesha kwamba viongozi wetu ni wababe, hawafuati sheria wala kanuni na ni mbumbumbu wa sheria. Kosa la mfanyakazi kuchelewa kazini adhabu yake sio viboko, kosa la mfanyakazi kutofika kazini adhabu yake sio viboko. Hawa ndio viongozi wetu wanaosisitiza uongozi unaofuata utawala wa sheria wakati wao wenyewe hawafuati hizo sheria wala kanuni.

Confidence ya hao walimu mbele ya wanafunzi wao imeshuka, hili linafungua ukurasa mpya kwa wanafunzi kuwadharau walimu wao kwa kuwa nao wanajua kwamba kiboko ya walimu ni DC. Kaazi kweli kweli!
 
hakuna kabisa uchunguzi ni lazima ,huwezi kupokea na kuamrisha lazima ufanywe uchunguzi wa kina na ukishatimia ndio hapo hata wale walimu wanaweza wakajikusanya na kumfungulia mashtaka huyo DC Mapepe ili aonje joto la mahakama kama akina Yona na isitoshe wadai fidia ka Bilioni saba tu zinatosha ,nasikia DC hajulikani alipo.
 
Nampongeza sana huyo mkuu wa wilaya waache watandikwe....si majuzi 2 wametoka kugoma hapa oooh hawajalipwa pesa zao,wakalipwa, sasa kwanini wasitekeleze wajibu wao.Hongera sana mkuu wa wilaya endelea hivyohivyo watandike tena ikibidi mbele ya wanafunzi!!!!!!!

Makubaliano ni kwamba wanawafundishia watoto wenu, na nyie mnawalipa pesa zao. Kama hamridhiki na utekelezaji wa wajibu wao, kuna hatua za kuchukua, na sheria za kazi zinajieleza. Na kwa urahisi unaweza kuwafukuza kazi.

Labda wewe utuambie unafanya kazi wapi, tuje tuangalie kama na wewe hustaili kuchapwa kiboko kama wao ... just kidding ...

Ukitiwa wewe kiboko utakuja kujaza mitundiko ya haki za binadamu hapa JF tehetehe ...:) Ama kweli mkuki kwa mchungu kwa binadamu nguruwe ... kabisa ...
 
hakuna kabisa uchunguzi ni lazima ,huwezi kupokea na kuamrisha lazima ufanywe uchunguzi wa kina na ukishatimia ndio hapo hata wale walimu wanaweza wakajikusanya na kumfungulia mashtaka huyo DC Mapepe ili aonje joto la mahakama kama akina Yona na isitoshe wadai fidia ka Bilioni saba tu zinatosha ,nasikia DC hajulikani alipo.

Ingawa uchunguzi ni lazima, walimu waliochapwa hawana haja ya kungojea. Wao wanatakiwa wakimbie hospitali ambako picha za majeraha yao zitachuliwa kabla hayajapona, halafu moja kwa moja mahakamani! Huo uchunguzi ni wa wizara, wao hauwahusu. Huyu DC amewapa dili bila kujua!
 
hakuna kabisa uchunguzi ni lazima ,huwezi kupokea na kuamrisha lazima ufanywe uchunguzi wa kina na ukishatimia ndio hapo hata wale walimu wanaweza wakajikusanya na kumfungulia mashtaka huyo DC Mapepe ili aonje joto la mahakama kama akina Yona na isitoshe wadai fidia ka Bilioni saba tu zinatosha ,nasikia DC hajulikani alipo.

Mkuu Mwiba,
Mi hata nashindwa kukuelewa. Unataka UCHUNGUZE NINI ZAIDI????
Jamaa kesha kiri ni kweli amewachapa viboko... na akatoa sababu so wewe unataka uchunguzi wa aina ya fimbo iliyotumika, kiwango cha maumivu AU ni nini hasa unachotaka kichunguzwe?? It is wastage of TIME, MONEY na KUFANYA WA TZ WAJINGA.
 
Hii imetulia sanaaa. Walimu wetu nao wamebweteka sana. Anyway hata Julius Nyerere aliwahi kumchapa waziri wake sembuse mwalimu? Mzee Mkuu Wa Wilaya wakirudia tena kutufanya tuwe wa mwisho tunawapa mboko mbele ya wanafunzi wao. BIG UP DC

Ningekuunga mkono kama ingekuwa kwamba mkuu wa wilaya naye akitenda kosa analiwa viboko na RC, na RC naye akikosea naye analiwa viboko na Raisi, na raisi akikosea wabunge wanapiga kura nani awakilishe wananchi kumlamba kiboko ... mbunge akikosea spika anapeleka bakora, spika akikosea ... itabidi tutengeneze mashine ya kulamba hawa wakulu viboko maana anayemlamba mkuu viboko anaweza kumuonea haya ...

... Hivi na wewe bosi wako nani vile? ... Na wewe ukikosea bosi wako anakulamba kiboko ... una mke kaka? maana ingekuwa poa zaidi bosi wako akikulamba kiboko, na mkeo naye anapewa kadhaa ... ahakikishe kwa mfano unawahi kuondoka nyumbani uwahi kazini :) Na mkeo naye kama ameajiriwa, huko kazini kwake akichelewa, mzee unaitwa, unalambwa kiboko ...

Hapo ningekuunga mkono ... na mambo yangeenda safi sana :)
 
Mkuu Mwiba,
Mi hata nashindwa kukuelewa. Unataka UCHUNGUZE NINI ZAIDI????
Jamaa kesha kiri ni kweli amewachapa viboko... na akatoa sababu so wewe unataka uchunguzi wa aina ya fimbo iliyotumika, kiwango cha maumivu AU ni nini hasa unachotaka kichunguzwe?? It is wastage of TIME, MONEY na KUFANYA WA TZ WAJINGA.

Kila mmoja apate uhakika wa kimaandishi,sio ushahidi wa kusema ,huo peke yake bado haujakuwa ni ushahidi,maana unaweza baadae akakataa na akasema haukuwachapa viboko isipokuwa wanamsingizia tu na kumpikia majungu kwa sababu anapendeza kwa wananchi, so far inabidi ushahidi uandaliwe kimaandishi ,polisi alietimiza wajibu wake nae ahojiwe mkuu wa kituo cha polisi nae ahojiwe kama alimruhusu kijana wake kwenda uraiani kucharaza mikwaju ndugu hii ni kesi kubwa maana mbali ya kumhusisha DC kuna na wengine nao pia hawatoki ukifuatilia utendaji wa kazi za kipolisi hivyo kinachotakiwa kufundishwa si kwa DC peke yake,bali hata kwa polisi waliotimiza wajibu wakiwa kazini ni nani alimpa polisi amri hiyo nae ahojiwe na akikutwa kwenda kinyume na sheria zao basi hapa Saidi Mwema itabidi amuwajibishe kiranja wake kwa kuliharibia jina Jeshi la polisi ,upo ,haya ni mambo ambayo yanataka yashonwe na yashoneke ili liwe fundisho kwa wengine ndio maana yake ,sio DC peke yake bali na wale waliokuwa nyuma yake ,sidhani kama Dc peke yake na polisi mmoja wangeweza kuwachapa viboko watu 50 lazima kutakuwepo na washiriki wengine na sheria inapochukua mkondo hata dereva nae anaweza kukaa jela wiki moja.
Ndipo sheria na utawala wakisheria utakapoanza kushika kasi.
 
Hao ndo waalimu wetu,Huyo ndiyo DC wao,Huyu ndo Naibu Waziri wetu,Na huyo ndiye Kikwete Rais wetu na Tanzania ndiyo nchi yetu.Kikwete alimteua Mwantumu Mahiza kuwa Naibu Waziri wa Elimu ambaye anasema DC aliyeteuliwa na Kikwete ana kichaa kwa kuwa amewalamba stroke waalimu ambo wamefelisha wanafunzi! Imekaa vizuri kweli wadau hiyo???Juzi Sitta alimrushia madongo Jaji Mkuu,Kule Mbarali DC alimlamba kofi mwananchi,Kule Manyara Mbunge alimkung'uta kijana! JK kule Mbeya alirushiwa mawe! Hapo vipi? Pamekaa vizuri kweli?

Kuna jambo la wazi ambalo wadau hawataki kulisema kwamba kuna mushkeli mkubwa katika uongozi wa JK-Yapo mengi ambayo yanajipambanua huku na kule!!Lakini Chama na Serikali vinaona ni mafanikio tuuu.Jamani tujiuize hadi lini mambo ya jinsi hii yatafika mwisho!?
 
Kila mmoja apate uhakika wa kimaandishi,sio ushahidi wa kusema ,huo peke yake bado haujakuwa ni ushahidi,maana unaweza baadae akakataa na akasema haukuwachapa viboko isipokuwa wanamsingizia tu na kumpikia majungu kwa sababu anapendeza kwa wananchi, so far inabidi ushahidi uandaliwe kimaandishi ,polisi alietimiza wajibu wake nae ahojiwe mkuu wa kituo cha polisi nae ahojiwe kama alimruhusu kijana wake kwenda uraiani kucharaza mikwaju ndugu hii ni kesi kubwa maana mbali ya kumhusisha DC kuna na wengine nao pia hawatoki ukifuatilia utendaji wa kazi za kipolisi hivyo kinachotakiwa kufundishwa si kwa DC peke yake,bali hata kwa polisi waliotimiza wajibu wakiwa kazini ni nani alimpa polisi amri hiyo nae ahojiwe na akikutwa kwenda kinyume na sheria zao basi hapa Saidi Mwema itabidi amuwajibishe kiranja wake kwa kuliharibia jina Jeshi la polisi ,upo ,haya ni mambo ambayo yanataka yashonwe na yashoneke ili liwe fundisho kwa wengine ndio maana yake ,sio DC peke yake bali na wale waliokuwa nyuma yake ,sidhani kama Dc peke yake na polisi mmoja wangeweza kuwachapa viboko watu 50 lazima kutakuwepo na washiriki wengine na sheria inapochukua mkondo hata dereva nae anaweza kukaa jela wiki moja.
Ndipo sheria na utawala wakisheria utakapoanza kushika kasi.

So now it will take 3 years to accomplisha all that (eti utawala wa sheria...zipi hizo ambazo haziwi complied to), Ndio maana nilisema It is wastage of TIME, MONEY....JUST WAJIBISHA THAT DC THEN FULL STOP.
 
Habari hii kiasi imekiweka wazi kile ambacho naamini ndio hali ya watanzania walio wengi. Hali hii imewafanya watanzania kuwa wepesi wa kuthbutu na kufanya maamuzi.

Wachukulia hawa waalimu zaidi ya 30 wanacharazwa viboko katika makundi matatu na watu wawili baada ya wao kuridhia (Kulala chini). Hii inasikitisha sana. Hawa ndio tunaowaona kuwa ni wasomi walioenea sehemu kubwa ya Tanzania kuliko wasomi wengine wote. Hawa ndio ambao huchukuliwa kama mfano wa watu waeruvu na wenye uwezo wa kutoa muongozo katika jamii wanazoishi. Wengi wao wana elimu ya kidato cha nne na miaka 2 ya chuo au miaka 4 ya ualimu baada ya darasa la saba.

Hawa ndio wanaowafundisha vijana na watarajiwa wa kesho somo la urai ambamo ndani yake mna haki za binadamu na utawala wa sheria. INASIKITISHA.

Katika hali kama hii unategemea ukombozi wa mtanzania utapatikana lini kama hata hawa ambao wanatakiwa wawe muongozo katika jamii kwa sababu ya kuwa na uelewa wa juu zaidi ya jamii inayowazunguka HAWAELEWI NINI HAKI NA WALA NINI NI UTAWALA WA SHERIA.

Mimi natazama kitendo cha mkuu wa wilaya kama bahati nzuri sana kwa WATANZANIA kujiangalia ndani wenyewe ni KUJIONA walivyo.

DC ametuonyesha jinsi tulivyo, sasa ni wajibu wetu kama taifa kujiangalia na kujua ni wapi tunapopotoka kwa kiasi hiki. Katika hali hii :- 1.hakuna uwajibika katika sehemu za kazi, 2. Haki lazima iendelee kuwa bidhaa 3. Hakuwezi kuwa na demokrasia na hivyo 5. Hakuwezi kuwa na chaguzi huru.

WAALIMU WAMETUSIKITISHA, ILA MKUU WA WILAYA AMETUONYESHA TULIVYO WATANZANIA
 
Kwa Kuwa huyu kawacharaza waalimu Bakora kwa kuwa shule zao zimekuwa za mwisho , na yeye yafaa achapwe na Mkuu wa Mkoa kwa sababu Wilaya yake imekuwa ya Mwisho , na huu ndio utawala wa sheria.
 
Kwa Kuwa huyu kawacharaza waalimu Bakora kwa kuwa shule zao zimekuwa za mwisho , na yeye yafaa achapwe na Mkuu wa Mkoa kwa sababu Wilaya yake imekuwa ya Mwisho , na huu ndio utawala wa sheria.

Sawa sawa MK, ili kila mmoja ahukumiwe kufuatana na cheo, nafasi yake pamoja na matendo yake!
 
Watanzania bana, utawala gani wa sheria wakati watu wanalalalala na kuacha kuwajibika?

Ilitakiwa rais awe mkali kama huyu mkuu wa wilaya. Safi sana. Kila siku hapa tunalalamika kuwa viongozi wetu ni magoigoi ndio maana watu wanashindwa kuwajibika kwa ufanisi unaotegemewa. Sasa huyu DC ameonyesha uzalendo wa kweli na uchungu alionao kwa maendeleo ya wilaya yake.

Elimu ndio ufunguo wa maisha jamani, elimu ikichezewa basi maisha yote yamechezewa, huwezi ukaleta maisha bora kwa kila mtanzania kama huyo mtanzania mwenyewe aliyekusudiwa hana elimu anayodeserve. Na kutokuwa huko na elimu kunasababishwa na mwalimu ambaye ana dhamana ya kutoa elimu hiyo hawajibiki ipasavyo.

Mkuu wa wilaya asisahau kuwachapa viboko wakurugenzi wa wilaya wanaokula pesa za ujenzi wa shule, ununuzi wa madawati vitabu bila kusahau viongozi wa wilaya wanaotumia pesa za miradi ya elimu kujinufaisha.

Kudos bwana mkuu wa wilaya, wakipatikana 100 kama wewe, mambo yangekuwa mswano. Baada ya kuwanyoosha walimu kwa viboko, tungehamia kwa madaktari na wauguzi huko wilayani. Watumishi wengine wakiwamo ma bwana na bibi afya wangelearn a lesson, vinginevyo na wao wapelekwe kwa viboko.
 
Wana JF,
Hivi hawa wakuu wa wilaya huchaguliwa na Rais? Kama ni hivyo basi Muungwana ana viongozi MABOMU ya kutupwa. Nampa hongera mkulu huyu kwa kuthibitisha zaidi UIMARA wa Serikali ya awamu ya nne. Huyu angelifaa hata awe Rais wetu naamini tungelifika mbali maana Mafisadi wote wangelichapwa viboko.

Sijui hata yule aliyeko Kigoma na yeye anafanya kazi vipi hasa ukichukuliwa alinyang'anywa mke na kigogo wa CCM na kupewa kifutia machozi akafanywa kuwa Mkuuwa Wilaya. Nategemea hata kuwa Mbovu/imara kama huyo.

Sikonge, nimeshawahi kusema kuwa sioni mantiki ya kuwa na Wakuu wa Mikoa (RCs) na Wakuu wa Wilaya (DCs), hivyo vilikuwa vyeo vya kikoloni na vilitumiwa na wakoloni na si ajabu huyo DC kuamuru Waalimu wachapwe viboko! Vyeo vya RCs na DCs huwa ni vyeo vya kuwasaidia 'wenzetu' ambao hawana pa kwenda na ndo maana utakuta sehemu kubwa ya RCs na DCs ni Wabunge waliopoteza Ubunge, walioondolewa kazini bila sababu za msingi na ili kuficha ukweli au kuepusha kesi anateuliwa kuwa RC au DC (Mfano Col. Simbakalia-RC wa Kigoma alikuwa DG wa NDC, akaondolewa baada ya kukataa matakwa ya Wakubwa kuhusu Mgodi wa Mchuchuma au Liganga).

Kuna DC wa Wilaya ya Hai- Husna Mwilima, huyu alikuwa Katibu wa Tawi moja la CCM Arusha Mjini, baada ya Muungwana na kundi lake kushika hatamu sasa ni Dc wa Hai tena ni bomu kweli! Mkuu wa Wilaya ya Tabora-Moshi Chang'a ulizia elimu yake, utachoka. Lakini alikuwa ni Mkereketwa huko Iringa na Mshereshaji kwenye matukio ya CCM! wako wengi na ni vituko vitupu na wote wamekabidhiwa Mashangingi!

Ingekuwa vema vyeo vya RC na DC vikafutwa wakabaki Maafisa Tawala (RAS na DAS) ambao ndio professionals na si hawa wanasihasa.
 
Sasa kwa kuchapwa hao walimu ndiyo watoto watafaulu?

Labda karudi ofisini kwake akisubiri wilaya iwe ya kwanza...baada ya kuwatandika walimu.
Just thinking loudly... what was the guy expecting anyway... as an outcome of corporal punishment the teachers?
 
Last edited:
Wewe analysis yako is very poor ...hata kungekuwa na walimu 10,000 akamchapa mmoja, bado tungemshambulia....hata angekuwa nae mmoja, kamchapa huyohuyo tungelia naye tu!

Usidandie gari kwa mbele.....soma habari vizuri...sababu za kuchapwa zimetolewa!

[Na huyo JK kwa kutuangusha wa TZ kwenye issue kama;
  • Inflation 13%
  • Pembejeo bei juu e.g mbolea zaidi ya Ths 100,000 per bag
  • Migomo ya wanafunzi re. suala la mikopo -80%,60%,40% or 0%
  • Mgogoro wa zanzibar - ambao kaushindwa kuupa ufumbuzi
  • Usanii kwenye issue za kifisadi re.EPA,Radar,Richmond,IPTL etc
  • Ongeza mengine unayo yajua
Kutokana na mambo haya maisha ya watanzania yamekuwa ni ya shida mno, so kufuatana wewe na yeye rais tumtandike viboko?

Nakushauri utulie kwanza kabla ya kuchangia bw' mdogo![/QUOTE]

Kwa kauli hizi bwa' mkubwa hiyo analysis yako ni very rich naona haushindani na hoja bali unamshambulia mtu binafsi. By analysing your arguments tunahitaji watu kama mkuu wa wilaya huyu wengi tu maana hata wewe unastahili viboko.
 
Unafikiri watz wote tupo kama hao walimu ''kondoo'' mnao waonea? You want some, come get some!
 
Back
Top Bottom