DC Bukoba aamuru walimu wachapwe mboko!

Hivi jamani mnao watetea hao walimu kwa misingi ya haki za binadamu mnaju na hao wanafunzi pia wana haki zao?
Haki za binabamu ni sababu mojawapo .....soma vizuri post zilizopita kwa sababu zaidi!

mkuu wa wilaya kaamuru walimu 32 tu ndio wachapwe viboko kwani mnajua wilaya yake ina walimu wangapi?

Wewe analysis yako is very poor ...hata kungekuwa na walimu 10,000 akamchapa mmoja, bado tungemshambulia....hata angekuwa nae mmoja, kamchapa huyohuyo tungelia naye tu!

na sababu zilizotolewa kwa kuchapwa hao 32 tu hamkuzielewa?

Usidandie gari kwa mbele.....soma habari vizuri...sababu za kuchapwa zimetolewa!

JK huyu ni mfano wa viongozi wenye uchungu na watoto wa taifa hili mpandishe cheo. Tena ikibidi awe waziri mkuu ili viboko viwashukie mawaziri.[/QUOTE]

Na huyo JK kwa kutuangusha wa TZ kwenye issue kama;
  • Inflation 13%
  • Pembejeo bei juu e.g mbolea zaidi ya Ths 100,000 per bag
  • Migomo ya wanafunzi re. suala la mikopo -80%,60%,40% or 0%
  • Mgogoro wa zanzibar - ambao kaushindwa kuupa ufumbuzi
  • Usanii kwenye issue za kifisadi re.EPA,Radar,Richmond,IPTL etc
  • Ongeza mengine unayo yajua
Kutokana na mambo haya maisha ya watanzania yamekuwa ni ya shida mno, so kufuatana wewe na yeye rais tumtandike viboko?

Nakushauri utulie kwanza kabla ya kuchangia bw' mdogo!
 
Last edited:
Hao walimu kama wapo CCM basi warudishe kadi za Chama chao kwani kimewafikisha pabaya na wajiunge na chama kingine chochote ,yaani watu 32 wanarudisha kadi za CCM na kujiunga chama kingine na wengine wanafuatia litakuwa pigo la aina yake.

Mimi naamini kabisa hata wanafunzi hawakubali kwa walimu wao kufanyiwa udikteta kiasi hicho ,kuna haja ya kuandaa maandamano ya wanafunzi kupinga hatua hiyo iliyofanywa na serikali. Kwa maana wacha Kagera uwe ni wa Chadema lakini ukivamiwa na majeshi ya Uganda waTz wote tutakuwa kitu kimoja na kupambana na adui alievamia nchi yetu, ,hivyo walimu na wanafunzi ni kitu kimoja kutokea mhuni wa serikali na kufanya dhambi hakutokubalika katika jamii ya walimu na wanafunzi ni lazima Walimu na wanafunzi wakusanyike ili kupinga ukiukwaji huo ni udhalilishaji mkubwa ambao haujawahi kutokea katika sekta ya elimu.
 
Usitegemea hayo kabisa kutoka kwa ''typical'' walimu wetu wa shule za msingi hasa za huko vijijini......! hawajiamini, hawajui taratibu zao kazi, hawawezi kujitetea kwa sababu wao wenyewe ni vilaza wa kutupwa...most of them ni failures wa f4...sasa what do you expect from them! So hawa inabidi watetewe na wengine wanaojua haki zao kama wewe! We still need them, cause hatuna option for now...hiyo ndo hali halisi ya elimu ya tanzania!

Mkuu NL, hapo umeugusa ukweli. Hawa walimu nao wana matatizo makubwa ila kujiamini ndilo tatizo kubwa zaidi. Niliwahi kusikia mwalimu mmoja (tena wa siku nyingi) akisema serikali ni watanzania wote kwa hiyo hakuna sababu ya kuilaumu. Hata baada ya kumuuliza mara kadhaa aliendelea kushikilia msimamo wake kwamba hata yeye ni sehemu ya serikali kwa sababu ameipigia kura! Nimeshasema hapo awali kwamba hizi ni dalili za tatizo kubwa zaidi katika mfumo mzima wa elimu. Labda tunaweza kupata mahali pa kuanzia. Mwalimu haelewi kwa nini anafanya hiyo kazi, Mkuu wa wilaya (haelewi wajibu wake) anatwanga walimu mboko, Waziri anaanzia kwenye matusi kwamba DC ni kichaa (badala ya kuongelea suluhu).....Total chaos...!!!:confused:
 
Last edited:
Hivi jamani mnao watetea hao walimu kwa misingi ya haki za binadamu mnaju na hao wanafunzi pia wana haki zao? mkuu wa wilaya kaamuru walimu 32 tu ndio wachapwe viboko kwani mnajua wilaya yake ina walimu wangapi? na sababu zilizotolewa kwa kuchapwa hao 32 tu hamkuzielewa? JK huyu ni mfano wa viongozi wenye uchungu na watoto wa taifa hili mpandishe cheo. Tena ikibidi awe waziri mkuu ili viboko viwashukie mawaziri.

Burn; wanafunzi pia wana haki. kumbuka pia serikali imekataza viboko kwa wanafunzi, leo hii unafurahia walimu kuchapwa eti wamefelisha.
Hatupingi walimu kupata adhabu kwa kuchangia kufeli kwa wanafunzi. Lakini ufahamu kuwa mwalimu si sababu pekee ya wanafunzi kufeli. Ninaamini kama hawa walimu wangepewa kalipio, wakajieleza ingelikuwa vyema na mkuu wa wilaya angejuwa wapi pana tatizo. Je mwaka jana walifelisha, mwaka juzi, na miaka ya nyuma ilikuwaje performance?. Hujawai ona darasa la mwaka huu ni baya kuliko la mwaka jana? Hii inawezekana. Kunakitu kinaitwa nature of the learners and individual differences. Si vizuri kwa mkuu wa wilaya kuwachapa walimu. Nadhani hata wewe unajuwa si vizuri.
Sababu za walimu kuchapwa tumezisoma. ndio maana tunasema kunasababu nyingi za wanafunzi kufeli.
Unamsifia mkuu wa wilaya, mpaka unafikia hatua ya kumshauri JK ampe uwaziri. hapa ndipo ninapowambia rafiki zangu " Individual differences". Well, nimawazo yako baada ya kumchambua mwalimu, kuangalia anavyofundisha, anavyofundishwa, anavyoishi, anavyojali kazi yake. Binafsi namshauri Jk amfukuze kazi huyu mkuu wa wilaya na si amwambie ajiuzuru. Nasema hivyo baada ya kuelewa na kufahamu taaluma ya uwalimu, uwalimu na uwalimu katika nchi ya Tanzania ukilinganisha na uwalimu wa nchi zingine.
Hatupingi adhabu kwa mtu aliekosea au aliechangia makosa, tunapinga aina ya adhabu. Ndio maana hata serikali inapinga adhabu ya viboko mashuleni.
 
Hivi jamani mnao watetea hao walimu kwa misingi ya haki za binadamu mnaju na hao wanafunzi pia wana haki zao?
Haki za binabamu ni sababu mojawapo .....soma vizuri post zilizopita kwa sababu zaidi!

mkuu wa wilaya kaamuru walimu 32 tu ndio wachapwe viboko kwani mnajua wilaya yake ina walimu wangapi?

Wewe analysis yako is very poor ...hata kungekuwa na walimu 10,000 akamchapa mmoja, bado tungemshambulia....hata angekuwa nae mmoja, kamchapa huyohuyo tungelia naye tu!

na sababu zilizotolewa kwa kuchapwa hao 32 tu hamkuzielewa?

Usidandie gari kwa mbele.....soma habari vizuri...sababu za kuchapwa zimetolewa!

JK huyu ni mfano wa viongozi wenye uchungu na watoto wa taifa hili mpandishe cheo. Tena ikibidi awe waziri mkuu ili viboko viwashukie mawaziri.[/QUOTE]

Na huyo JK kwa kutuangusha wa TZ kwenye issue kama;
  • Inflation 13%
  • Pembejeo bei juu e.g mbolea zaidi ya Ths 100,000 per bag
  • Migomo ya wanafunzi re. suala la mikopo -80%,60%,40% or 0%
  • Mgogoro wa zanzibar - ambao kaushindwa kuupa ufumbuzi
  • Usanii kwenye issue za kifisadi re.EPA,Radar,Richmond,IPTL etc
  • Ongeza mengine unayo yajua
Kutokana na mambo haya maisha ya watanzania yamekuwa ni ya shida mno, so kufuatana wewe na yeye rais tumtandike viboko?

Nakushauri utulie kwanza kabla ya kuchangia bw' mdogo!

Huyo anapigika kirahisi kwa kuwa maboss wake ni thithi! Bado kama miezi 20 tu tutamtundika kwenye ukuta tumsulubu! Ila hawa wateule wake ni ngumu kuwafikia. Lakini tukiamua tunawatimulia mbali, kwani tumesahau hadithi ya "Kibanga amkung'uta mkoloni"??
 
Last edited:
BIG-UP DC! wamzidi mbona wao huwa wanawacharaza wantu pale wanapofeli so mkuki kwa nguruwe..... kumbukeni enzi za mwalinhu tulipokuwa shule za msingi jinsi tulivyokuwa tunachapa ukichelwa kushika namba fimbo, ukifeli mtihani ama testi fimbo tena bila hata ya huruma... Jamani waliosomba Muhimbili enzi hizo mwamkumbuka Mwl. Ndosi yule baba siku akikuvalia jinsi na tshirt ujue siku hiyo kiama akiwa zamu balaa, mkifeli hisabati mmnae sasa hawa kuchapwa ni haki yao maana wameshindwa kuwafundisha wanetu. Wanachojua ni kuwapa wanafunzi miradi yao wawauzie mwanafunzi akikataa ana chapwa walimu wa vijijini wao ni kuwachukua wanafunzi wakawafanyie kazi zao za nyumbani kipindi cha kilimo wanafunzi wananda pia kufanya kazi ktk mashamba ya walimu . DC kanifurahisha sana wnye kuchukia wachukie but narudia tena na tena DC BIG UP kazi nzuri wengine waige mfano wako.

Mimi ni mmoja wa wale wachukiao. Umempa big up DC kwa kuwachalaza viboko walimu, hiyo big up umempa kutokana na historia yako pale Muhimbili kupia mwl Ndosi. Kumbe bila hiyo hisitoria kunauwezekano wa kutompa big-up DC. Well, sawa haujakosea kumpa big-up DC, mimi nampa big-down DC. Cha ajabu hata mimi nimechalazwa fimbo kama wewe, lakini ninapinga adhabu ya fimbo kwa walimu hawa walioCHANGIA kufeli kwa darasa la saba, wanaosemekana wanachelewa shule.
 
Hao walimu kama wapo CCM basi warudishe kadi za Chama chao kwani kimewafikisha pabaya na wajiunge na chama kingine chochote ,yaani watu 32 wanarudisha kadi za CCM na kujiunga chama kingine na wengine wanafuatia litakuwa pigo la aina yake.

Mimi naamini kabisa hata wanafunzi hawakubali kwa walimu wao kufanyiwa udikteta kiasi hicho ,kuna haja ya kuandaa maandamano ya wanafunzi kupinga hatua hiyo iliyofanywa na serikali. Kwa maana wacha Kagera uwe ni wa Chadema lakini ukivamiwa na majeshi ya Uganda waTz wote tutakuwa kitu kimoja na kupambana na adui alievamia nchi yetu, ,hivyo walimu na wanafunzi ni kitu kimoja kutokea mhuni wa serikali na kufanya dhambi hakutokubalika katika jamii ya walimu na wanafunzi ni lazima Walimu na wanafunzi wakusanyike ili kupinga ukiukwaji huo ni udhalilishaji mkubwa ambao haujawahi kutokea katika sekta ya elimu.

Mawazo yako mazuri sana ila ushauri wako umeupeleka mahali ambapo sipo. Hao wanaostahili huo ushauri siyo walimu wa Tz. Walimu wetu wana adabu sana, hata ukiwambia wapige magoti na kumsalimia hata mwenyekiti wa kijiji watafanya hivyo tu. Wana heshima bwana, na ni waaminifu sana. Kwa hiyo hapa wataombwa radhi na mwaka huu huu watasimamia uchaguzi wa serikali za mitaa. Ngoja usikie matoke, chama chetu kitashinda kwa asilimia 99. Na mwakani lazima wahakikishe raisi wetu anashinda kwa asilimia zaidi ya 80. Unacheza na walimu wetu nini? Wanaipenda serikali yao kwa sababu nao ni sehemu ya serikali na pia ni sehemu ya tume ya uchaguzi (NEC). Tuwaache tu, DC atamalizana nao sasa hivi na mambo yatakuwa poa. Kwanza ni masuala ya serikali na chama chetu. Hebu acheni kuingilia mambo yetu!!:rolleyes:
 
This habari has made my day kwakweli. I can just imagine mwalimu anaambiwa "Aroooo, inama na ushike masikio" "Ukigusa **** tu, naanza kuhesabu upya". This is so funny! Lakini swali ninalojiuliza kichwani kwangu ni, hawa walimu walikamatwa kwa nguvu ili kuchapwa? Kwanini wasingekataa kama waliona si sahihi wao kuchapwa? We are speaking of 32 teachers here. Yaani wote wakalambishwa mboko bila kukubali? Something is wrong with the teachers as well. Sijui scenario ilikuwaje, lakini I can just imagine they were too dumb kuitwa mmoja mmoja na kupigwa mboko.
 
Inawezekana DC amekosea kuwacharaza viboko walimu wetu hawa. Lakini naamini ujumbe umefika kwa wadau wote wa elimu ya nchi yetu ambayo iko katika hali mbaya sana kwenye shule za serikali. Walimu kwenye shule za serikali HAWAFUNDISHI kuanzia msingi hadi sekondari. Mtoto ambaye hachangii kwenye TUITION zao anasoma kwa taabu kwelikweli. Serikali iangalie pia ujumbe aliotaka kuuwasilisha DC huyu.
 
Waziri Mkuu "mkimshika muuwaji wa Albino muuweni", Mkuu wa Wilaya "Waalimu wachapwe viboko". Kila mtu anaamua analofikiri. Sheria ziko wapi?
 
Mawazo yako mazuri sana ila ushauri wako umeupeleka mahali ambapo sipo. Hao wanaostahili huo ushauri siyo walimu wa Tz. Walimu wetu wana adabu sana, hata ukiwambia wapige magoti na kumsalimia hata mwenyekiti wa kijiji watafanya hivyo tu. Wana heshima bwana, na ni waaminifu sana. Kwa hiyo hapa wataombwa radhi na mwaka huu huu watasimamia uchaguzi wa serikali za mitaa. Ngoja usikie matoke, chama chetu kitashinda kwa asilimia 99. Na mwakani lazima wahakikishe raisi wetu anashinda kwa asilimia zaidi ya 80. Unacheza na walimu wetu nini? Wanaipenda serikali yao kwa sababu nao ni sehemu ya serikali na pia ni sehemu ya tume ya uchaguzi (NEC). Tuwaache tu, DC atamalizana nao sasa hivi na mambo yatakuwa poa. Kwanza ni masuala ya serikali na chama chetu. Hebu acheni kuingilia mambo yetu!!:rolleyes:

Kazi kwelikweli. Ukiambiwa washauri utawaambiaje?
 
Hali za walimu na wanafunzi ni sawasawa wote hohehahe masikini za Mungu, Mwalimu mshahara wake anaupata kwa mbinde akielekea kazini lazima apitie shamba aone kama kutavunika na mtoto nae akitoka nyumbani amekula kipande cha embe na hajui mchana akirudi atakula nini.

Hivyo maendeleo ya walimu na wanafunzi kwa ujumla yanasababishwa na serikali na wasituambie kuwa walimu ndio wahusika wakuu wa kufeli kwa wananfunzi huo ni uongo wa kupandikiza ili kujikosha kwa Chama Tawala,mitihani ambayo huko wanakopasi huwa imeibiwa ,ni mara ngapi tumesikia kuwa mitihani imevuja ? Kwa maana waliopasi walikwisha kuiona mitihani.

Aidha kuwachapa walimu kutasaidia zaidi katika wizi wa mitihani maana hata huyo DC itabidi aibe mitihani ili wanafunzi na walimu wake waonekane ni mahodari.

Serikali ya CCM inashindwa kuwaeleza wananchi kwa nini wanafunzi wanafeli ,mwalimu na Wanafunzi wote ni njaa tupu ,hivi kuna kupasi hapo ? Shida nchini zimeenea kila sehemu hivi kutakuwa na kupasi hapo ? Hali ya maisha ya Mtanzania imeshuka hivi kutakuwa na kupasi hapo ? Serikali iliyopo haina habari haiwashughulikii walimu kutakuwa na kupasi hapo ? Na ikiwa wanashughulikiwaa ni wachache wale wa miji mikuu hivi vijijini huko kutakuwa na kupasi ? Mijini kumejaa mashule ya kulipia ,maisha ya mijini yanajulikana njia za kujipatia fedha zipo lakini kijijini huna njia zaidi ya kijishamba chako na kwenda kuuza maembe sokoni ,Walimu kama hawakupatiwa mishahara kwa wakati unafikiri kutakuwa na usomeshaji zaidi mwalimu atatumia muda kujilimia ili asije akaaibika hivyo kupasi kwa wanafunzi ni jambo linalochangiwa na serikali na Chama chake tawala ambacho kumejaa wizi wa mabilioni ya shilingi ,fedha ambazo zingeweza kabisa kuwalipa walimu na kuwasaidia wanafunzi katika hali zao za kila siku.

Mabilioni hayo yangeweza kabisa kuwekesha mashule na nyumba za kisasa kwa wanafunzi na walimu hata generators huko vijijini na watu wakawa wanasoma na kufundishana usiku na mchana.

CCM ndio iliyotufikisha hapa tulipo sasa tunaanza kupigana bakora wenyewe kwa wenyewe kisa wanafunzi hawakufaulu .Na wananchi waifahamu CCM maana CCM haina hasara sana ,ikiwa viongozi wenyewe ni akina Makamba unategemea nini ikiwa si kutufungafunga kwa kutumia kamba hizo. Wakati wao wanajali maslahi yao binafsi na watoto wao ,ndio kama tuonavyo CCM likibambwa na ufisadi unalikuta lina mimali kibao na dhamana hata iwe bilioni mia utakuta asubuhi yake anazitoa.

Sasa huku wanakofanya ni kutudhslilisha tu na kutufanya tuwe bize wakati wao wanapanga mingine ya kukwiba 2010.
 
Taaluma yangu ni ualimu, lakini hata nilipokuwa chuoni hdai nahitimu mafunzo ya ualimu sikuwahi chapwa viboko hata mara moja, hii imenikera sana hasa ukizingatia walimu hawa ndio wanaoandamana kila siku kudai haki, Dc kawachapa walimu kwa sheria ipi?katiba ipi? kanuni zipi? No anapaswa kuwajibika japo nilishapumzika ualimu miaka kumi iliopita HAPANA
 
What is required is Mild Dictatorship. DC amepata uchungu nadhani kwa sababu mbili. Moja wilaya yake kuwa wa mwisho mkoani. Hii ina maana katika KPI zake zinamuharibia. Pili wanafunzi wanaharibiwa future yao kwa sababu waalimu hawakutimza wajibu wao. Waalimu wamekuwa wakidai malipo yao na wamepewa basi ni zamu yao kutekeleza wajibu wao.

Guys, let us not just comment when we dont have facts, inauma sana I sometimes feel like crying when I read some posts. Nani kasema walimu wamelipwa mafao yao? just because they are quite. Naomba nikupe evidence of the situation. Mkoani mbeya kati ya walimu wote wanaoidai serikali ni walimu 70 tu ndio wamepata mafao yao kwa madai kuwa serikali bado inahakiki, my mom is a teacher as well. sasa unaposema wamelipwa unahizo takwimu? lakini hata kama wangekuwa wamelipwa ndo tuwachape? pleasee

Wilaya ya bukoba inaweza kuwa ya mwisho kwa mkoa wa kagera lakini yaweza kuwa ya 30 katika ya wilaya zaidi ya 180 za tanzania, kwa hiyo hizo wilaya nyinge tuwafanyeje? the way people comment on this naamini kunahata mtu atasema wanyongwe,

I believe huyo DC will get what he deserves na kwa kweli akiendelea kuwa DC walimu watastahili kugoma and I will support the move.

Kila mpenda maendeleo nchi hii anaumia sana perfomance za shule zetu zinapokuwa mbaya lakini cha msingi sote tunahitaji kuwajibika kwa pamoja, mwalimu na chaki, serikali na sera nzuri ma mazingira mazuri ya kufundishia, na sisi wengine wote kufanya bidii wherever we are it tusonge mbele. they are many causes of poor perfomace in schools mwalimu is just one of those, kumchapa ni kumwonea tu.
 
Enzi za ukoloni nasikia kulikuwepo na adhabu ya viboko hadharani, raia akifanya kosa kama kutupa taka ovyo au kujisaidia ovyo adhabu yake ilikuwa viboko au corporal punishment ikiitwa kwa wakati huo. Lakini sijafikiria kama karne hizi mtu mwenye wadhifa kama Mkuu wa Wilaya anaamuru adhabu hiyo ambayo labda uwaulize walioishi wakati wa ukoloni wanaweza kutambua lakini akina sisi hatujawahi kusikia adhabu hiyo. Nafikiri huyu mkuu wa wilaya yeye mwenyewe akapimwe akili na kama akili yake ni nzuri basi wale walimu wapewe bakora wamtandike na yeye.
 
Walimu waliochapwa wachukue hatua mikononi mwao maana wakienda mahakamni jamaa atavuka na wajue wanapotumwa kusimamia upigaji kura basi wasiwe wenye kuisaidia CCM kwani malipo yake ndo wameyaona.
 
Taaluma yangu ni ualimu, lakini hata nilipokuwa chuoni hdai nahitimu mafunzo ya ualimu sikuwahi chapwa viboko hata mara moja, hii imenikera sana hasa ukizingatia walimu hawa ndio wanaoandamana kila siku kudai haki, Dc kawachapa walimu kwa sheria ipi?katiba ipi? kanuni zipi? No anapaswa kuwajibika japo nilishapumzika ualimu miaka kumi iliopita HAPANA

Bora tumekupata mwal hapa jamvini!
 
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Magembe alikiri kuwa na taarifa hyo na kusema kwamba kamwe hawawezi kulivumilia.

"Ni kweli kuna tukio la aina hiyo na nimeshamwagiza mkuu wa mkoa kufanya uchunguzi na endapo ukweli utapatikana, serikali itachukuwa hatua kali dhidi ya wahusika," alisema Profesa Magembe na kuongeza:

"Nchi yetu haiwezi kuongozwa na watu wa aina hiyo na kamwe serikali haiwezi kukaa kimya... mara tu baada ya mkuu wa mkoa kumaliza kazi yake, atatuletea taarifa na sisi tutalifikisha kwa waziri mkuu kwa hatua zaidi kwani hao wote wako chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu".

"Hilo ni tukio la aina yake na lakusikitisha sana kwa sababu binadamu hawezi kuongozwa njia kwa kuswagwa kama ng'ombe... ni lazima serkali ichukue hatua kali dhidi ya wahusika". Ila Pemba waliwaswaga na kuwadhalilisha ama kweli damu nzito.
 
Back
Top Bottom