Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 353
Mkuu wa wilaya aamuru polisi kucharaza bakora walimu 32
"Hilo ni tukio la aina yake na lakusikitisha sana kwa sababu binadamu hawezi kuongozwa njia kwa kuswagwa kama ng'ombe... ni lazima serkali ichukue hatua kali dhidi ya wahusika".[/SIZE][/FONT]
Binadamu hawezi kuongozwa kwa kuswagwa kama ng'ombe....excellent! Wanafunzi wanalambwa viboko kila siku na hakuna anayesema kitu, ina maana wao si wanadamu na ni sawa na ng'ombe? Hii adhabu ya viboko nimekuwa nikiipinga toka zamani lakini naona waalimu hawako tayari kutumia njia nyingine mbadala za kuwadiscipline, sasa sijui ndo tuseme..mkuki kwa nguruwe.......? Sifagilii alichofanya Mkuu wa wilaya lakini labda huu ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa adhabu za viboko mashuleni, and am sure kwa kuwa waalimu sasa wanaujua 'utamu wa bakora' watakuwa wakifiria mara mbilimbili kabla ya kutumia adhabu hii ya kikatili katika karne hii!