Walimu kupiga watoto mpaka kuua! ipo siku atauliwa mtoto wa kiongozi ndipo tutaamka

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,264
7,404
Hii tabia imekithiri sana ya kupiga watoto kwa mangumi, mateke, na mbaya zaidi kupiga watoto mgongoni ambako ndiko kuna uti wa mgongo! Tabia ya kuficha na kutoa taarifa za uongo kumkandamiza aliyeuliwa na kukosesha haki ndiko kunafanya walimu waendelee na tabia hii mbaya kabisa!

Halafu kuna hawa walimu wa vitendo ambao sio waalimu kamili wao wanawapigisha watoto mazoezi ya JKT mwishowe wanaua

Soma hii ya tukio la moshi kwa kweli nimesikitika sana

Mimi hii ikinitokea kwa mwanangu lazma ntalala mbele mwalimu husika sina msamaha

----
Jeshi la Polisi linawashikilia na kuwahoji walimu watano tarajali wa mafunzo ya ualimu (BTP) wanaofundisha katika Shule ya Msingi Mrupanga mkoani Kilimanjaro, kwa madai ya kuhusika na kifo cha mwanafunzi wa darasa la kwanza, Jonathan Makanyaga (6).

Mwanafunzi huyo, mkazi wa Kijiji cha Kimanganuni chini, Kata ya Uru Kusini wilayani Moshi, alifariki dunia Machi 10, mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini, KCMC alikolazwa kwa matibabu, kwa kile kinachodaiwa alichapwa viboko na mmoja wa walimu hao baada ya kuchelewa shuleni.

Inadaiwa Februari 28, mwanafunzi huyo akiwa na wenzake wawili walichapwa na mwalimu huyo (jina halijatajwa) baada ya kuchelewa shuleni hapo na Jonathan alichapwa sehemu mbalimbali mwilini, kisha kuangushwa chini.

Inaelezwa wenzake wawili alikuwa nao wakati wanachapwa walijikinga na fimbo hizo kwa kutumia mabegi waliyokuwa wamebeba mgongoni na Jonathan alishindwa kujizuia na kuumizwa sehemu ya uti wa mgongo, mbavuni na sehemu ya mapajani na kisha kuangushwa chini.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema mama na bibi wa Jonathan walikwenda shuleni kuhoji kwa nini mtoto wao amerudi nyumbani akiwa na hali hiyo na ndipo walimu waliwapoza na wakashirikiana nao kumpeleka hospitali bila kutoa taarifa polisi.

“Mtoto aliendelea na matibabu mpaka Machi 10 alipofariki. Tulichofanya, lilifunguliwa jalada la kifo cha mashaka kwa sababu hakuna taarifa iliyotolewa awali, ila tunawashikilia walimu wa mafunzo ya vitendo watano kwa mahojiano na kesho (leo) kutafanyika postmortem (uchunguzi wa kifo) ili kujua chanzo cha kifo chake,” alisema.


Mama afunguka

Janeth Shayo, mama wa mtoto huyo alieleza Februari 28 mwanaye alirudi nyumbani akiwa hana furaha na mdogo wa Jonathan alimweleza kuwa kaka yake anavuja damu mdomoni.

Alisema alipomwangalia alibaini ni kweli, mwanaye anavuja damu mdomoni na puani, na alipomuuliza alimweleza amechapwa viboko na mmoja wa walimu hao kwa sababu ya kuchelewa kushika namba saa moja kamili asubuhi.

“Jioni nilipakua chakula, nikamwambia baada ya kula apumzike kidogo kisha aende kulala, wakati nadeki mdogo wake akaniita akanambia Jonathan anatoka damu puani, nikimwangalia damu zinatoka bado nikamuuliza wapi panauma, akanambia kichwa kinamuuma, nilimpa dawa za maumivu (paracetamol) wakalala na mdogo wake,” alisema.

Alisema asubuhi ya siku iliyofuata aligundua mtoto huyo alikuwa na damu nyingi mdomoni, wakati anamuandaa ampeleke hospitali alibaini ana majeraha mgongoni.

“Nikamuuliza tena umejigonga wapi? Akasema hajajigonga, mgongo ulikuwa umevimba na eneo la chini ya uti wa mgongo kuna uvimbe umevilia damu na ni kweusi, pajani nako kuna alama ya fimbo na kumevilia damu, kwenye mguu nako kumevimba," alisema.

Alisema hali hiyo ilimfanya aende shule kujua sababu za mtoto wake kuadhibiwa kiasi hicho.

“Nilikutana na mwalimu mkuu msadizi ambaye baada ya kuona hali ya mtoto, akanipa Sh20,000 nikamtibu na itakavyokuwa niwaambie. Nilikwenda zahanati nikapewa dawa, daktari akanambia akizidiwa nimrudishe achomwe sindano, nilienda naye nyumbani lakini bado hali yake ilikuwa si nzuri,” alisema na kuongeza;

“Sikuweza kulala ilibidi nimrudshe zahanati, alipomwona na kumwangalia kwenye macho akanambia nimpeleke hospitali ya St Joseph.
"Nilipofika mapokezi walimwangalia mtoto hali yake ilivyo, nikaambiwa nikafungue faili, walivyomuona mtoto kadri siku zilivyokuwa zikienda, wakanishauri nimpeleke KCMC kwa vipimo vikubwa zaidi na Machi 8 tukawa tumeenda,"

Hata hivyo, alisema baadaye daktari aliyekuwa akimhudumia alimweleza kuwa mtoto ana changamoto ya seli sahani na kuna damu imevujia tumboni, hivyo atawekewa mirija.

“Kabla hilo halijafanyika mwanangu akawa amefariki tarehe 10," alisimulia mama huyo.

Alipotafutwa mwalimu mkuu wa shule, Florah Kahabi alisema hawezi kuzungumzia tukio hilo kwa kuwa lipo kwenye vyombo husika na kwamba yupo msemaji wa tukio hilo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Shedrack Mhagama alisema baadaye ya kupita taarifa ya mwanafunzi kufariki shuleni hapo walifuatilia kujua ukweli wake na kwamba taarifa walizonazo ni kuwa mwanafunzi huyo alikuwa anaumwa saratani ya damu.

“Nilipata hizi taarifa, nilifuatilia kule shuleni, mtoto alikuwa anaumwa saratani kwa muda mrefu na ndio maana amefariki," alisema mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya KCMC, Gabriel Chisseo alisema, “Baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari wetu, waligundua alikuwa na upungufu mkubwa wa damu na baadaye vipimo vilionyesha alikuwa na saratani ya damu, kwa mfano chembe sahani pekee tu zikikutwa 11 kwa hiyo uwezekano wa kupata matatizo ni mkubwa zaidi".

Chanzo: Mwananchi
 
Tatizo la walimu ni failure ndiyo wanaoenda huko hawajui hata miongozo mbalimbali ya ualimu kuhusu adhabu mashuleni.

Sasa mtu aliyefeli akakosa pakwenda akaamua kwenda ualimu anawezaje kuwa na uelewa wa kusoma muongozo wa adhabu mashuleni ambao unamkataza mwalimu kutoa adhabu isipokuwa kwa taratibu maalum tu.
 
Sisi kama wanasheria tumekubaliana ili kukomesha upuuzi huu wa walimu wapumbavu tutajitolea kufungua kesi yoyote hata kama tu mtoto ataadhibiwa pasipo kufuata utaratibu madhubuti uliowekwa.

Hatuwezi kusibiri watoto wauliwe ndiyo tuanze kufungua kesi hapana, tutafungua kesi hata pale tu utaratibu wa adhabu utakapokiukwa.

Sasa fikiria mtoto wa miaka 6 darasa la kwanza anashambuliwa na lijitu lizima halafu sijui linasikia fahari gani.

Stress zao za maisha zinapelekea kuwashambulia watoto wadogo wasio na uelewa wa mambo.
 
Nilishaapa mwalimu yeyote akijichanganya kumuadhibu mwanangu pasipo kufuata utaratibu rasmi uliowekwa kisheria aise atakuwa mfano mzuri kwa walimu wengine wapumbavu.

Kuna haja ya walimu kupimwa akili kabla na baada ya ajira maana wengi ni wagonjwa wa akili.
 
Tatizo la wazazi mnaficha magonjwa ya watoto wenu,akiguswa na mwalimu kidogo inakuwa tiketi ya kifo na malalamiko kuanzia hapo,hakuna mwalimu wa kuchapa mtoto wa miaka 6 kwa jinsi hiyo inavyoelezwa never
 
Hawa walimu wakuu nao kuna haja ya kuunganishwa kwenye kesi maana wao ndiyo wenye dhamana ya kusimamia ustawi wa watoto mashuleni.

Wawape onyo walimu wao juu ya kutoa adhabu kiholela vinginevyo mwalimu akikaidi basi apendekeze kuhamishwa kwa mwalimu huyo ili iwe fundisho.

Kwenye kesi kama hizi lazima kuwaunganisha walimu wakuu kwenye hati ya mashitaka ili wakajibu uzembe wao wa kutowasimamia vuzuri walimu walio chini yao.
 
Tatizo la wazazi mnaficha magonjwa ya watoto wenu,akiguswa na mwalimu kidogo inakuwa tiketi ya kifo na malalamiko kuanzia hapo,hakuna mwalimu wa kuchapa mtoto wa miaka 6 kwa jinsi hiyo inavyoelezwa never
Wewe ni miongoni mwa walimu vilaza mliofeli form four mkaamua kujiingiza kwenye ualimu.

Mimi ni shuhuda walimu wanne wamejipanga mstari wanaadhibu watoto wadogo kwa viboko visivyo na idadi.

Nilikuwa napita maeneo hayo ya shule nikaenda kwa mwalimu mkuu nikamwambia njoo uone walimu wako wanachowafanyia watoto wadogo. Alivyotoka alishuhudia ninachokisema.

Aliwaita ofisini akawaandikisha barua za maelezo zikae kwenye kumbukumbu ili kosa kama lile likijirudia basi wapate adhabu inayostahili.

Walimu wengi wana upungufu wa akili wanachapa watoto popote mwilini sasa hapo utasema wana akili timamu?
 
Wazazi watoto muwasomeshe wenyewe nyumbani.
Wewe kama mwalimu huwezi kufuata muongozo wa utoaji adhabu kwa wanafunzi?

Au kusoma hamjui vizuri ndiyo maana licha ya kupewa muongozo wa utoaji adhabu mashuleni lakini bado hukuelewa?

Fuateni sheria vinginevyo mtaishia jela na kupelekea kunyongwa hadi kufa kisa kuendekeza upuuzi.

Mimi kitaaluma ni lawyer huwa napita mashuleni kukutana na walimu kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya elimu na adhabu.
 
Kuna siku nilikuwa kwenye shule fulani nilikuwa kwenye darasa fulani nikifanya shughuli fulani iliyonipeleka hapo na wakati huohuo masomo yalikuwa yanaendelea kwenye hilo darasa alilokuwa anafundisha mwalimu fulani binti binti.Kuna mda yule teacher alimkata kibao mtoto fulani wa kike bongebonge inaonekana yule mtoto alikuwa mzito kimasomo lakini pamoja na hilo kofi alilomkata yule mtoto hata ukipigwa mtu mzima lazima uweweseke nilimuonea sana huruma yule mtoto upigaji kama ule ni wa hatari
 
hii tabia imekithiri sana ya kupiga watoto kwa mangumi, mateke, na mbaya zaidi kupiga watoto mgongoni ambako ndiko kuna uti wa mgongo! tabia ya kuficha na kutoa taarifa za uongo kumkandamiza aliyeuliwa na kukosesha haki ndiko kunafanya walimu waendelee na tabia hii mbaya kabisa!


halafu kuna hawa walimu wa vitendo ambao sio waalimu kamili wao wanawapigisha watoto mazoezi ya JKT mwishowe wanaua

soma hii ya tukio la moshi kwa kweli nimesikitika sana


mimi hii ikinitokea kwa mwanangu lazma ntalala mbele mwalimu husika sina msamaha
Mtoto wa waziri hasomi shule za mafagio na vidumu vya maji
 
Back
Top Bottom