Walimu mbaroni wakidaiwa kufanyisha wanafunzi wa Sekondari Mitihani ya Darasa la 7

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1695390804128.png
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia walimu wanne kwa tuhuma za kuwafanyisha mitihani ya darasa la saba wanafunzi watatu wa sekondari katika Shule ya Msingi Igulumuki Wilaya ya Sengerema mkoani humo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa Septemba 22, 2023; Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amewataja walimu wanaoshikiliwa ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari Sima wilayani humo na Msimamizi Mkuu wa Mitihani katika shule ya Msingi Igulumuki, Maiko Sheusi (35).

Wengine ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Kilabela ambaye ni msimamizi wa mtihani mkondo namba 2, Musa Mwashihava (38), Mwalimu wa Shule ya Sekondari Buzilasoga, Bonasi Balozi (33) na Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Msingi Igulumuki, Azizi Mohamed (36).

"Walimu hawa wanatuhumiwa kwa kosa la udanganyifu wa mitihani ya darasa la saba kwa kuwachukua wanafunzi wa Sekondari na kuwafanyisha mitihani hiyo kwa niaba ya wanafunzi wa darasa la saba,” amesema Mutafungwa

Mutafungwa amesema wanafunzi wanaoshikiliwa wote wana miaka 14 wanaosoma shule ya Sekondari Sima Kata ya Igukumuki wilayani humo wakidaiwa kuingizwa kwenye chumba cha mtihani kwa ajili ya kufanya mitihani hiyo kwa niaba ya wanafunzi wengine.

Amesema tukio hilo lililotokea Septemba 13, Mwaka huu, baada ya Kamati ya Mitihani ya Wilaya ya Sengerema kutembelea na kukagua namna mitihani hiyo inavyofanyika na kubaini udanganyifu huo ambapo mkondo namba mbili na namba tatu wa shule hiyo ilibainika kuwa na wanafunzi wa Sekondari wakifanya mitihani hiyo.

"Watuhumiwa wote wamehojiwa kwa kina na watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya upelelezi kukamilika. Tunaendelea kuimarisha ulinzi maeneo yote na hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wahalifu na wadanganyifu wa aina yoyote," amesema Kamanda huyo

Katika hatua nyingine, Jeshi hilo limeanza uchunguzi wa Kampuni ya Alliance Global in Motion ambayo inadaiwa kufungua Ofisi katika jengo la Rock City Mall wilayani Ilemela mkoani Mwanza huku ikituhumiwa kufanya utapeli dhidi ya vijana 150 kwa kuwatoza fedha kwa ahadi ya kuwawezesha kufanya biashara ya tiba lishe kwa njia ya mtandao.

"Tulianza uhunguzi wa kampuni hiyo Septemba 19 mwaka huu baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa wananchi kwa kuwahoji watu mbalimbali wakiwemo wanachama 46 kati yao mabinti wawili wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali,"amesema

Amesema jeshi hilo linaendelea kufuatilia uhalali wa kampuni hiyo pamoja na shughuli inazozifanya kwa mujibu wa sheria na katika uchunguzi huo litashirikiana kwa ukaribu na tasisi nyingine za Serikali.

MWANANCHI
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia walimu wanne kwa tuhuma za kuwafanyisha mitihani ya darasa la saba wanafunzi watatu wa sekondari katika Shule ya Msingi Igulumuki Wilaya ya Sengerema mkoani humo...
Tukisema hii nchi ina watu wa hovyo wanachukia!! Imagine!! Mtihani wa std 7 unafanya udanganyifu ili upate nini?
 
Siwalaumu Ila huruma imewaponza, watoto wapo wanaofeli na wanakosa nafasi za kujiunga sekondary, Bora walewale wenye mtihani wao wangewaacha wasingewachukia hao wakubwa wa seco, Ila wasingewabania kivile kusaidiana kimakini.
 
Katika hatua nyingine, Jeshi hilo limeanza uchunguzi wa Kampuni ya Alliance Global in Motion ambayo inadaiwa kufungua Ofisi katika jengo la Rock City Mall wilayani Ilemela mkoani Mwanza huku ikituhumiwa kufanya utapeli dhidi ya vijana 150 kwa kuwatoza fedha kwa ahadi ya kuwawezesha kufanya biashara ya tiba lishe kwa njia ya mtandao.

MWANANCHI
Vijana 150. Haya yote HAYANA AKILI na ni MAFALA.
 
Pumbavu sana, hii tabia ya kutaka sifa za kijinga eti shule fulani inafaulisha sana ni upuuzi. Ofisa elimu wa ngazi yeyote hawezi kunishuritisha nifanye manuever ya kufaulisha kwa wingi kwa kutumia mbinu zozote hata mbinu za kimafia. Potelea mbali watafaulu haohao wachache walioelewa walichofundishwa kwa miaka yote wakiwa shuleni. Sifa za kijinga haziwezi kusababisha niharibu ajira yangu kwa kuwafurahisha mabosi nionekane nimefaulisha wanafunzi wengi. Kila mwanafunzi atavuna alichopanda, no spoon feeding
 
Kweli kabisa "Better few but better" haohao wachache watakao faulu ndio walioelewa Kila mwanafunzi atavuna alichokipanda ,Bora wachache walioelewa kuliko kutumia mbinu za zakufaulusha mbumbumbu
 
Amesema tukio hilo lililotokea Septemba 13, Mwaka huu, baada ya Kamati ya Mitihani ya Wilaya ya Sengerema kutembelea na kukagua namna mitihani hiyo inavyofanyika na kubaini udanganyifu huo ambapo mkondo namba mbili na namba tatu wa shule hiyo ilibainika kuwa na wanafunzi wa Sekondari wakifanya mitihani hiyo.
Siku zote hizi walikuwa wanasubiri nini kutoa taarifa au ni baada ya wazazi na hao walimu kushindwa kutoa mlungura
 
Siwalaumu Ila huruma imewaponza, watoto wapo wanaofeli na wanakosa nafasi za kujiunga sekondary, Bora walewale wenye mtihani wao wangewaacha wasingewachukia hao wakubwa wa seco, Ila wasingewabania kivile kusaidiana kimakini.
Sio huruma ni njaa, hapo pesa walopata haizidi 50k kila mmoja
 
Back
Top Bottom