Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

Hahahaha mkuu, hivi dar huwa kuna baiskeli eee. Ngoja nianze kuzingatia.
zipo ndugu yangu...ukienda mwanzo wa kariakoo pale ILALA zipo baiskeli za mtumba Chopa nzuri kweli ukiwa na 150,000/= au 200,000/= unapata baiskeli nzuri mountain bike ambayo utapita popote bila kukuchosha sana.

siku za mwanzo utachoka sana ila ukizoea mkuu utakuwa umejitoa kwenye hicho kitanzi cha usafiri wa kugombania...

je unaishi wapi...? na kazini kwako ni wapi...?​
 
018100094042.JPG
 
Dah nmetoka kupiga jana tu hesabu ya mwezi maana nlidownload app ya budget playstore ambayo nilikua naandika kila income na expenses nlizokuwa natumia mbona macho yaligeuka mekundu na nguvu kuniisha

Maana daily 20k mafuta gari
Daily 20k home na hapo baadh ya vitu vipo
Bills umeme,maji nk 50k
Chakula job 10k hpo ndo kujibana
Vocha
Na mengineyo.
NB;
Sinywi pombe wala si mtu wa starehe
Umefka mwsho wa mwezi Expenses zimegonga 3m+ nikawa kama nimemwagiwa maji

kuna vitu sio sawa kuvipigia hesabu unaweza jikuta siku nzima umevimba uso hucheki na mtu.
 
Huyu ni mwajiriwa wa serikali atawezaje kuamua sehemu ya kwenda kufanya kazi?
Kama ni mwajiriwa wa serikali angalia makazi ya karibu na kazini, unafanya kazi tmk kwanini ukakae Kimara? au tegeta? Panga hapo Mbagala, buza n.k.

Usiishi sehemu kwa kufata mkumbo, hasa marafiki na ndugu, angalia unafuu wako wa kufika kazini tu.

Mfano mm wakati naanza maisha nilitaka kukaa karibu na kazi yangu lakini kwa sababu ni Mbagala ndugu walinisema sana, unakaeje Mbagala kama..... Mm sikuskiliza leo wenyewe wamekubali na kuacha kunishangaa kama mwanzo na ili waone mm ni mtu wa msimamo nimenunua kiwanja sehemu wasioikubali kabisa yan mbali nao, ila mm naangalia kipato changu sio chao.

MATOKEO YA MAISHA YAKO YA BAADAYE NI WW MWENYEWE SIO NDUGU WALA MARAFIKI ZAKO.
 
Pengine atakuwa amejenga mbali ndiyo maana analalamika kuhusu nauli kwasababu sio yeye Tu wapo wengi ambao wamejenga nje ya mji na wanafanya kazi city centre
 
Pengine atakuwa amejenga mbali ndiyo maana analalamika kuhusu nauli kwasababu sio yeye Tu wapo wengi ambao wamejenga nje ya mji na wanafanya kazi city centre
Asee ni kweli mkuu lakini kama anashindwa kuresize iyo 10k ya nauli ili aweze kuilipa basi hali yake itakuwa ngumu, kwa mfumo wa Kiafrika pambana kuendana na mabadiliko, punguza matumizi yasiyo ya lazima ili ujazie iyo ya naul. Mambo mengine huwezi kubadili hata ufanye nini.
 
Ningeshauri kama ingependeza kungekua na usafiri wa kushare ambao watu wanaotoka Kimara mpaka Posta, Gongo la mboto mpaka Posta na Bunju mpaka Posta na kama gari ya watu watano then mnachangia hata elfu 5 na inakua ni nzuri zaidi
 
Katafute chumba karibu na ofisi pangisha ili uwe unaenda home wikiend tu
Ukishindwa huko unapokaa Kama umejenga pangisha ilo jengo lako ww kapange mjini karibu na ofisini kwako
 
Back
Top Bottom