Uanzishwe mpango maalumu wa usafiri Kwa wanafunzi wa shule za Umma

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Kwako Waziri wa uchukuzi Prof. Makame Mbarawa na wahusika wengine. Kwanza, napenda kuwapa pole Kwa kazi ngumu na pongezi Kwa kazi nzuri ambayo wizara ya uchukuzi inafanya hususani ujenzi wa miundombinu mbalimbali na kubwa zaidi ujenzi wa Reli.

Waziri, binafsi ninakukubali Kwa uchapakazi na uwajibikaji na matokeo ya uchapakazi wako yanaonekana popote unapokuwepo.

Waziri ,pamoja na mambo mengine ninapenda kutumia jukwaa hili kukufikishia maoni yangu yanayohusu wizara unayoongoza. Naamini ujumbe utaupata.

Adha ya usafiri Kwa wanafunzi wa shule za Umma Kwa Dar es salaam ni kubwa na wanakumbana na changamoto nyingi si tu wakati wa kwenda shule bali hata wakati wa kurudi.

Tunashuhudia mara nyingi wanafunzi wakikataliwa kuingia kwenye daladala Kwa madai mbalimbali ambayo hayana tija. Kwa mfano , mwanafunzi ambaye hana nauli kamili anakataliwa kupanda daladala au wengine wanapakia idadi ndoto wakisema wanatosha. Sasa huwa tunajiuliza, je Kuna muongozo wowote wa kupakia idadi ya wanafunzi au ya kupokea pesa kamili kutoka Kwa wanafunzi?

Waziri, kutokana na changamoto hizo na nyingine nyingi wanafunzi hawa hususani wa kike wanajikuta wakiingia majaribuni kwenye makucha ya 'watoa lift' Kwa sababu ya kunyanyasika kwenye usafiri wa Umma na akiangalia muda anaona umeenda anaona bora akubali kupewa " lift" na hapo ndipo matatizo mengine hutokea.

Ninaamini changamoto hii Kwa hawa wanafunzi inaweza kutatuliwa na Serikali na kupitia wizara unayoongoza ninaamini Serikali itasaidia hili kufanyika.

Kama mmoja wa watu ambaye ninaguswa na changamoto hii wanayokumbana nayo wanafunzi ,ninawiwa kutoa mchango mdogo wa maoni na haya ndio maoni yangu:

Kwanza, kama inawezekana Serikali ianzishe mpango maalumu wa usafiri Kwa wanafunzi katika shule za Umma Kwa kununua magari (daladala) ambazo zitakuwa na jukumu la kusafirisha wanafunzi tu ,kuwapeleka shule na kuwajesha makwao.

Pili, wizara ikemee vikali vitendo vya makondakta kuzuia wanafunzi kupanda kwenye daladala Kwa sababu yoyote ambayo haina mashiko. Serikali itoe muongozo juu ya hili.

Tatu, kuwepo na usimamizi mkubwa kutoka Kwa askari wa usalama barabarani kusaidia wanafunzi kupanda kwenye daladala nyakati za jioni ili kuwasaidia kuwaepusha na lift Giza linapoingia.

Nne, iwe ni lazima Kwa mwanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la Tano kusoma karibu na nyumbani maana wanafunzi hawa wadogo mara nyingi ndio wanakuwa ni wahanga wakubwa.

Ni hayo tu Waziri niliyotaka kukufikishia.

Ahsante
 
Kwako Waziri wa uchukuzi Prof. Makame Mbarawa na wahusika wengine. Kwanza, napenda kuwapa pole Kwa kazi ngumu na pongezi Kwa kazi nzuri ambayo wizara ya uchukuzi inafanya hususani ujenzi wa miundombinu mbalimbali na kubwa zaidi ujenzi wa Reli.

Mhe. Waziri, binafsi ninakukubali Kwa uchapakazi na uwajibikaji na matokeo ya uchapakazi wako yanaonekana popote unapokuwepo.

Mhe. Waziri ,pamoja na mambo mengine ninapenda kutumia jukwaa hili kukufikishia maoni yangu yanayohusu wizara unayoongoza. Naamini ujumbe utaupata.

Adha ya usafiri Kwa wanafunzi wa shule za Umma Kwa Dar es salaam ni kubwa na wanakumbana na changamoto nyingi si tu wakati wa kwenda shule bali hata wakati wa kurudi.

Tunashuhudia mara nyingi wanafunzi wakikataliwa kuingia kwenye daladala Kwa madai mbalimbali ambayo hayana tija. Kwa mfano , mwanafunzi ambaye hana nauli kamili anakataliwa kupanda daladala au wengine wanapakia idadi ndoto wakisema wanatosha. Sasa huwa tunajiuliza, je Kuna muongozo wowote wa kupakia idadi ya wanafunzi au ya kupokea pesa kamili kutoka Kwa wanafunzi?

Mhe. Waziri, kutokana na changamoto hizo na nyingine nyingi wanafunzi hawa hususani wa kike wanajikuta wakiingia majaribuni kwenye makucha ya 'watoa lift' Kwa sababu ya kunyanyasika kwenye usafiri wa Umma na akiangalia muda anaona umeenda anaona bora akubali kupewa " lift" na hapo ndipo matatizo mengine hutokea.

Ninaamini changamoto hii Kwa hawa wanafunzi inaweza kutatuliwa na Serikali na kupitia wizara unayoongoza ninaamini Serikali itasaidia hili kufanyika.

Kama mmoja wa watu ambaye ninaguswa na changamoto hii wanayokumbana nayo wanafunzi ,ninawiwa kutoa mchango mdogo wa maoni na haya ndio maoni yangu:

Kwanza, kama inawezekana Serikali ianzishe mpango maalumu wa usafiri Kwa wanafunzi katika shule za Umma Kwa kununua magari (daladala) ambazo zitakuwa na jukumu la kusafirisha wanafunzi tu ,kuwapeleka shule na kuwajesha makwao.

Pili, wizara ikemee vikali vitendo vya makondakta kuzuia wanafunzi kupanda kwenye daladala Kwa sababu yoyote ambayo haina mashiko. Serikali itoe muongozo juu ya hili.

Tatu, kuwepo na usimamizi mkubwa kutoka Kwa askari wa usalama barabarani kusaidia wanafunzi kupanda kwenye daladala nyakati za jioni ili kuwasaidia kuwaepusha na lift Giza linapoingia.

Nne, iwe ni lazima Kwa mwanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la Tano kusoma karibu na nyumbani maana wanafunzi hawa wadogo mara nyingi ndio wanakuwa ni wahanga wakubwa.

Ni hayo tu mhe. Waziri niliyotaka kukufikishia. Ahsante
ok,
vipi na mikoani hali okoje...

nako kuna haja ama ni dar pekee?
 
Sema baadhi ya vitu kutafuta lawama,
Wazazi tuepuke kupeleka watoto wetu shule za mbali na nyumbani,
Wazazi tuwape pesa ya kutosha watoto ya nauli
 
Unayo hoja ya msingi sana, serikali inapaswa kukusikiliza. Changamoto inakuja pale ambapo huku Vijijini kuna vijana wanatembea km 10 kwa siku kwa ajili ya kuifuata shule, hawa tunapaswa kuangalia namna ya kuwasaidia pia.
 
HOJA ZOTE NI NZURI
1. DAR ( kati na pembezoni)
2. MIKOANI

Nakumbuka zamani UVCCM ilianzisha MRADI WA MABASI YA WANAFUNZI......

NI WAZO CHANYA LENYE LENGO BORA KABISA
 
Back
Top Bottom