CUF waishambulia CHADEMA

Jazba zote hizi kuhusiana na hii mada hazina tija kwa Chadema.
Matokeao ya viongozi wa chama kuwa hostile kwa vyama vingine vyote (CCM, CUF, NCCR, TLP) si mazuri.
Very soon tutaanza kujiuliza tulidondokea wapi?...
Kwa mwenendo huu.... I'm afraid our dear Chadema is heading into a ditch..... take my word.

JK na Dr Slaa.jpg JK Zito na Simbakalia.jpg
 
ALIYEKUWA kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bunge lililopita, Hamad Rashid Mohamed amewashambulia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.

Hamad amewatuhumu Chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na Chama Cha Wananchi (CUF) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.

Mbunge huyo wa Wawi (CUF) alimewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, wao (CUF) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.

Amewataka viongozi wa Chadema wawe ‘matured’ na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua Rais Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa Hamad, CUF wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo Chadema wajifunze kwao (CUF).

Alisema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na CUF kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika Bunge hilo.

Hamad amesema, alikataa wazo la Mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.

Mwanasiasa huyo amesema, CUF wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, Chadema hawataki.

Hamad amesema, viongozi wa Chadema wamemkwaza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.

Source: Basil Msongo,HabariLeo ,Dodoma; Tarehe: 18th November 2010

Hiyo source ni uchakachuaji mtupu sorry haiziki
 
Jazba zote hizi kuhusiana na hii mada hazina tija kwa Chadema.
Matokeao ya viongozi wa chama kuwa hostile kwa vyama vingine vyote (CCM, CUF, NCCR, TLP) si mazuri.
Very soon tutaanza kujiuliza tulidondokea wapi?...
Kwa mwenendo huu.... I'm afraid our dear Chadema is heading into a ditch..... take my word.

View attachment 17250View attachment 17251

Afadhali Chadema in the ditch with honour kuliko kusaliti dhamira yake ya haki ya wananchi
 
Mimi naona CUF wanasumbuliwa na wivu tu. Wameona Chadema wameenda juu sana kwa umaarufu na wanakubalika nchi nzima. Na wameona kura za Prof Lipumba zimepungua kutoka 1.8m 2005 mpaka laki tano, na Dr Slaa kapanda na kama si uchakachuaji angekuwa Ikulu. Na kauli ya Prof Lipumba kuwa yeye ni mlima Kilimanjaro na Dr Slaa ni kichuguu ikadhihirika kinyume. Sasa kwa hali ya kawaida ya binadamu lazima uone wivu ambao kama hutaangalia vizuri utazaa chuki na mwisho wake si mzuri.

Nawashauri CUF watulie, wenyewe waendelee na muafaka na Zanzibar, huku bara waiachie Chadema ituletee ukombozi wa kweli.
 
Jamani CUF wameishaunda kambi na CCM watawezaje kuunda kambi tena na CHADEMA Kwa hali ilivyo hivi sasa wakati Zanzibar wameunda serikali ya mseto kati ya CCM na CUF ni upuuzi kufikiri ya kua CUF itafanya vinginevyo katika bunge la muungano.Mfano mzuri ni katika zoezi la kumchagua spika.Hapa ukweli unabaki ulele ule CUF haitaweza kua katika upinzani na CHADEMA CUF de fact ni CCM B CUF hamuwezi kukalia farasi wawili kwa wakati mmoja labda iiundwe CUF zanzibar na CUF Tanganyika vinginevyo nimkoroganyiko usio na tija CUF hawana sifa ya kujihita wa pinzani kwa hali ilivyo hivi sasa mazingira yalivyo hivi sasa.MUNGU IBARIKI NTANZANIA
 
Hivi na CHADEMA Walipokuwa wanakampeni kama wakipewa ridhaa kuongoza wataunda serikali ya umoja au sura ya kitaifa walikuwa wanamaanisha nini?Na je hiyo serikali wangeiunda na watu kutoka vyama gani?

Chadema haikuwa na sera ya serikali ya umoja wa kitaifa, hiyo ni sera ya CUF. Chadema uwezo wake ni mkubwa.
 
Ingawa Chadema hawamtambui Kikwete , tangu Bunge la 10 lilipoanza vikao, wabunge wa chama hicho wamekuwa wakihudhuria vikao hivyo, Rais wa Tanzania ni sehemu ya Bunge.

hapo imekaaje!
 
Chadema should start learning to live their newly found "premium" status.
Kwa sababu they are on their way up, it can't please the likes of CUF - which is natural.

Nitawashangaa sana Chadema kama wata-yield kwa shinikizo zinazokuja sasa eti kujenga alliance ya upinzani. Upinzani upi if I may ask?
Baadhi yetu tuli-advocate sana alliance huko siku za nyuma but.....
It's now too late for Chadema kuangalia nyuma - nawaambia mtageuka jiwe!

You are now on your own folks and all what you have to do now is continue strengthening the position you have decided to take. Your supporters (didn't say members) are probably going to be divided around it but I think you should stick to what you have decided to pursue - mkikubali kuyumbishwa tu, your party's credibility will find itself amongst that sewer stuff!!
 
Nimecheka sana, Yaani sasa malengo ya CUF yanaanza kuwa crystal clear. Yaani CUF ndo wanawaonya Chadema kuwa kuna madhara ya kutomtambua rais aliyetangazwa na tume? CUF ambao wamemkataa karume kule Zanzibar hadi juzi juzi tu baada ya kurushiwa peremende? Sasa CUF wanaanza rasmi kuifanya kazi ya CCM ya kuishauri Chadema imtambue rais!!

Sasa iwe wazi, kwa wale wote waliokuwa wakiamini kuwa CUF inaweza ikawa mpinzani bara wakati Zanzibar wako serikalini, kuwa hilo halipo. Na anayesema CUF na Chadema wanaweza kuunda kambi ya upinzani haitakii mema kambi hiyo na pengine haoni haja ya kuwa na kambi ya upinzani. Na kusema kweli ni CCM pekee anayeweza kuona hilo la CUF kuungana na Chadema kwenye kambi ya upinzani ni jambo jema.

CUF walikuwa wanashirikishwa. Sasa huo usemaji wa vyama vingine CUF wamepewa lini? Yaani CUF wanaambiwa karibuni tuunde kambi ya upinzani, lakini wao wanasema ili sisi tuje inabidi na NCCR, UDP na TLP wawemo!! Si TLP, UDP wala NCCR waliokwishasema kuwa wanataka kuingia kwenye hiyo kambi. Sasa CUF wamepataje hiyo 'authority' ya kuvisemea hivyo vyama vingine??

CUF ni moja na CCM ni moja, kule Zanzibar na huku bara pia! Ni kujilisha upepo kuamini kuwa CUF na CCM sasa hivi watatofautiana kwa lolote, nasema ni kujilisha upepo. Sasa hivi wao, lao moja, nalo ni kuona kuwa ajenda za serikali zao zinapita bila kupigiwa kelele na yeyote.

Asante mkuu. Litakuwa kosa kubwa kwa CHADEMA kushirikiana na CUF ambao wanamakubaliano ya siri na wakubwa zao CCM. CHADEMA wakishirikiana na CUF basi by default CHADEMA itakuwa ni CCM. Dhama za chama kimoja tutarudi huko. Kazi kubwa ya CUF kwenye yale makubaliano yao ni kuuwa upinzani na CHADEMA. Nafurahi viongozi wa juu wameliona hili. CUF imepoteza identity ya upinzani nadhani tamaa ya viongozi wao imewafikisha huko. 2015 CUF itakuwa imefutika kabisa

Mch Masa K
 
aliyekuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni katika bunge lililopita, hamad rashid mohamed amewashambulia viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.

Hamad amewatuhumu chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na chama cha wananchi (cuf) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.

Mbunge huyo wa wawi (cuf) alimewaeleza waandishi wa habari mjini dodoma kuwa, wao (cuf) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.

Amewataka viongozi wa chadema wawe ‘matured’ na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua rais jakaya kikwete.

Kwa mujibu wa hamad, cuf wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo chadema wajifunze kwao (cuf).

Alisema, mwenyekiti wa chadema, freeman mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na cuf kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika bunge hilo.

Hamad amesema, alikataa wazo la mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.

Mwanasiasa huyo amesema, cuf wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, chadema hawataki.

Hamad amesema, viongozi wa chadema wamemkwaza mwenyekiti wa nccr mageuzi, james mbatia na mwenyekiti wa cuf, profesa ibrahim lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.

Source: Basil msongo,habarileo ,dodoma; tarehe: 18th november 2010
huo kama sio umbea maana yake nini? Anongea wanaume wawili mambo ya kitaifa wewe unayatoa hadaharani.
 
Hivi na CHADEMA Walipokuwa wanakampeni kama wakipewa ridhaa kuongoza wataunda serikali ya umoja au sura ya kitaifa walikuwa wanamaanisha nini?Na je hiyo serikali wangeiunda na watu kutoka vyama gani?

We unachanganya sera za Chadema na CUF.Hakuna wakati chadema walisema ataunda serikali ya kitaifa,Fanya utafiti kabla ya kuhukumu.
 
Jazba zote hizi kuhusiana na hii mada hazina tija kwa Chadema.
Matokeao ya viongozi wa chama kuwa hostile kwa vyama vingine vyote (CCM, CUF, NCCR, TLP) si mazuri.
Very soon tutaanza kujiuliza tulidondokea wapi?...
Kwa mwenendo huu.... I'm afraid our dear Chadema is heading into a ditch..... take my word.

View attachment 17250View attachment 17251

Wow!! you missed it, the opposite is true.... forget your word :smile:
 
Wakuu zangu hili sio swala la kupuuza hata kidogo. Chadema acheni uchu wa madaraka kuunda kambi ya Upinzani na haitawasaidia chochote zaidi ya kujenga fitna zaidi.
Kweli kabisa Chadema kulingana na katiba inayo haki ya kufanya kila kitu watakavyo isipokuwa mjue tu kinachozungumziwa zaidi na katiba ni jinsi ya kumpata kiongozi wa kambi hiyo ya Upinzani, kuliko uundwaji wa kambi yenyewe.

Vipengele vyote vinazungumzia nani atakuwa kiongozi wa kambi hiyo lakini haikatazi chama kuunda umoja na vyama vingine kwani maana ya kuunda kambi hiyo ni kutoa fursa kwa vyama vingine vipate nafasi ya kuzungumzia hoja walizokuwa nazo dhidi ya chama tawala. Kinyume cha vyama hivyo havitakuwa na nafasi hiyo isipokuwa kuuliza maswali ya nyongeza tu.

Leo hii wakuu zangu nimeamka vibaya na hakika sipendi kuzungumza mengi isipokuwa nasema Mkuu wangu Mbowe, ile tabia ya kuwatumia watu kisha ukawaacha mataani iache.. sii nzuri hata kidogo na wala sii uungwana kwa sababu siasa sio biashara ni maelewano ambayo yanahitaji uaminifu na makubaliano ambayo hayawezi vunjika mara tu unapofanikiwa na kutaka kuvuta asilimia yote 100 wewe.

Hizi tabia za kusema CUF wana wivu ni tabia za kishenzi tu, ni tabia zisizokuwa na shukranii kutofikiria ulitoka wapi na leo umefika wapi ukasahau kwamba pasipo ushirikiano wa mwenzako pengine usingefika hapo ulipo. Alichozungumza Rashid ndiyo hali halisi na sioni sababu kwa nini watu mlitaka afiche hali ndicho kilichotokea hadi kutokuwepo ushirikiano baina ya vyama kuunda kambi ya Upinzani. Sasa kama Chadema mnafikria mnaweza kwenda solo baada ya mafanikio mloyapata uchaguzi huu, sawa endeleeni kufurahia matunda hayo lakini amini maneno yangu malipo yake yatakuja jitokeza muda sii mrefu... Itakula kwenu.
 
Chadema should start learning to live their newly found "premium" status.
Kwa sababu they are on their way up, it can't please the likes of CUF - which is natural.

Nitawashangaa sana Chadema kama wata-yield kwa shinikizo zinazokuja sasa eti kujenga alliance ya upinzani. Upinzani upi if I may ask?
Baadhi yetu tuli-advocate sana alliance huko siku za nyuma but.....
It's now too late for Chadema kuangalia nyuma - nawaambia mtageuka jiwe!

You are now on your own folks and all what you have to do now is continue strengthening the position you have decided to take. Your supporters (didn't say members) are probably going to be divided around it but I think you should stick to what you have decided to pursue - mkikubali kuyumbishwa tu, your party's credibility will find itself amongst that sewer stuff!!

........ got you loud and clear.
 
Wakuu zangu hili sio swala la kupuuza hata kidogo. Chadema acheni uchu wa madaraka kuunda kambi ya Upinzani na haitawasaidia chochote zaidi ya kujenga fitna zaidi.
Kweli kabisa Chadema kulingana na katiba inayo haki ya kufanya kila kitu watakavyo isipokuwa mjue tu kinachozungumziwa zaidi na katiba ni jinsi ya kumpata kiongozi wa kambi hiyo ya Upinzani, kuliko uundwaji wa kambi yenyewe.

Vipengele vyote vinazungumzia nani atakuwa kiongozi wa kambi hiyo lakini haikatazi chama kuunda umoja na vyama vingine kwani maana ya kuunda kambi hiyo ni kutoa fursa kwa vyama vingine vipate nafasi ya kuzungumzia hoja walizokuwa nazo dhidi ya chama tawala. Kinyume cha vyama hivyo havitakuwa na nafasi hiyo isipokuwa kuuliza maswali ya nyongeza tu.

Leo hii wakuu zangu nimeamka vibaya na hakika sipendi kuzungumza mengi isipokuwa nasema Mkuu wangu Mbowe, ile tabia ya kuwatumia watu kisha ukawaacha mataani iache.. sii nzuri hata kidogo na wala sii uungwana kwa sababu siasa sio biashara ni maelewano ambayo yanahitaji uaminifu na makubaliano ambayo hayawezi vunjika mara tu unapofanikiwa na kutaka kuvuta asilimia yote 100 wewe.

Hizi tabia za kusema CUF wana wivu ni tabia za kishenzi tu, ni tabia zisizokuwa na shukranii kutofikiria ulitoka wapi na leo umefika wapi ukasahau kwamba pasipo ushirikiano wa mwenzako pengine usingefika hapo ulipo. Alichozungumza Rashid ndiyo hali halisi na sioni sababu kwa nini watu mlitaka afiche halki ndicho kilichotokea hadi kutokuwepo ushirikiano baina ya vyama kuunda kambi ya Upinzani. sasa kama Chadema mnafikria mnaweza kwenda solo baada ya mafanikio mloyapata uchaguzi huu, sawa endeleeni kufurahia matunda hayo lakini amini maneno yangu malipo yake yatakuja jitokeza muda sii mrefu... Itakula kwenu.

Kiongozi acha utani!

CUF + CCM unataka na CHADEMA waingie kwenye huo muungano? unajua makubaliano ya CUF na CCM kuunda serikali ya kitaifa huko Zanzibar, baraza la mawaziri lina CUF na CCM na Seifu ni makamu wa raisi (kivuli). Upinzani utafutika iwapo CHADEMA wakiamua kushirikiana na CUF. Ukiangalia kwa mbali utaona CUF ni wasemaji wa CCM
 
Mbona CCM na CUF kwenye serikali ya umoja wa kitaifa hawakuvishirikisha vyama vingine? Sasa iweje leo walete hoja ya kuvikusanya vyama vyote? Yaani CCM na CUF ni haki kufanya waliyoyafanya Zanzibar ila Chadema ni haramu kufanya hivyo bara?
 
Wakuu zangu hili sio swala la kupuuza hata kidogo. Chadema acheni uchu wa madaraka kuunda kambi ya Upinzani na haitawasaidia chochote zaidi ya kujenga fitna zaidi.
Kweli kabisa Chadema kulingana na katiba inayo haki ya kufanya kila kitu watakavyo isipokuwa mjue tu kinachozungumziwa zaidi na katiba ni jinsi ya kumpata kiongozi wa kambi hiyo ya Upinzani, kuliko uundwaji wa kambi yenyewe.

Vipengele vyote vinazungumzia nani atakuwa kiongozi wa kambi hiyo lakini haikatazi chama kuunda umoja na vyama vingine kwani maana ya kuunda kambi hiyo ni kutoa fursa kwa vyama vingine vipate nafasi ya kuzungumzia hoja walizokuwa nazo dhidi ya chama tawala. Kinyume cha vyama hivyo havitakuwa na nafasi hiyo isipokuwa kuuliza maswali ya nyongeza tu.

Leo hii wakuu zangu nimeamka vibaya na hakika sipendi kuzungumza mengi isipokuwa nasema Mkuu wangu Mbowe, ile tabia ya kuwatumia watu kisha ukawaacha mataani iache.. sii nzuri hata kidogo na wala sii uungwana kwa sababu siasa sio biashara ni maelewano ambayo yanahitaji uaminifu na makubaliano ambayo hayawezi vunjika mara tu unapofanikiwa na kutaka kuvuta asilimia yote 100 wewe.

Hizi tabia za kusema CUF wana wivu ni tabia za kishenzi tu, ni tabia zisizokuwa na shukranii kutofikiria ulitoka wapi na leo umefika wapi ukasahau kwamba pasipo ushirikiano wa mwenzako pengine usingefika hapo ulipo. Alichozungumza Rashid ndiyo hali halisi na sioni sababu kwa nini watu mlitaka afiche hali ndicho kilichotokea hadi kutokuwepo ushirikiano baina ya vyama kuunda kambi ya Upinzani. Sasa kama Chadema mnafikria mnaweza kwenda solo baada ya mafanikio mloyapata uchaguzi huu, sawa endeleeni kufurahia matunda hayo lakini amini maneno yangu malipo yake yatakuja jitokeza muda sii mrefu... Itakula kwenu.

........ umesikika kwa chini sana mkuu.
 
tusiwe blinds kwenye hili... Lazima tuelewe ukweli kabla ya kudhani CUF hawana point

Much as we seek for changes, it has to be very systematic and sophisticated... nadhani kuna haja ya CHADEMA ku-take things slow and cut off drama ili wajipange upya, including kujenga kambi ya upinzani

Nakumbuka niliuliza kuhusu kambi ya upinzani, nikaambiwa kwamba CHADEMA ndio walikua na haki ya kufanya, lakini naamini kama wangeamau kukaribisha wapinzani wote, hilo lingeleta maana zaidi na ile courtesy ingezaa imani ndani ya upinzani

Najifunza hayo masiasa because i am for changes lakini nadhani kuna tatizo kidogo... haiwezekani wewe tu ndio uchukiwe na kila mtu

Having said that, nashauri wakuu chadema wakae chini na wa-shut down media for three months kupunguza impurities and reach out to wapinzani ili kujenga upya upinzani

Sio lazima kuungana wapinzani wote na sio kila anaejiita mpinzani anamaanisha ni mpinzani, mtu kama Mrema na chama chake unawaita wapinzani? Je, ulifuatilia kauli zake wakati wa campaign? alivyokuwa akiisifia CCM na wakati huohuo kasimamisha mgombea Urais kwa chama chake huku akidai jk ni kiongozi bora, sasa km jk ni kiongozi bora alisimamisha mgombea urais ili iweje?
Hivi bado unahisi CUF ni wapinzani? Pole sana CUF sio wapinzani hata chembe wamekwisha pata madaraka Unguja hivyo wanachukulia kila jambo po tu. Na ninakuambia jk atakapo mpa madaraka Lipumba ndo utaona habari yake, na kwataarifa yako atapewa madaraka na CUF wanatambua hilo ndo maana wameanza kujikomba kwa CCM.:nono:
 
Mbona CCM na CUF kwenye serikali ya umoja wa kitaifa hawakuvishirikisha vyama vingine? Sasa iweje leo walete hoja ya kuvikusanya vyama vyote? Yaani CCM na CUF ni haki kufanya waliyoyafanya Zanzibar ila Chadema ni haramu kufanya hivyo bara?

Sawa mkuu sijui inakuwaje watu wengine wanashindwa kuliona hili. Ubinafsi wa CUF umeanzia visiwani, na ukijaribu kuleta hoja ya kutaka kushirikisha vyama vingine kwenye hiyo serikali ya umoja wa kitaifa huko Zenj CUF waweza kukupasua kichwa. Kwa sababu wanaona ni haki yao hao wawili tu.
 
Mbona CCM na CUF kwenye serikali ya umoja wa kitaifa hawakuvishirikisha vyama vingine? Sasa iweje leo walete hoja ya kuvikusanya vyama vyote? Yaani CCM na CUF ni haki kufanya waliyoyafanya Zanzibar ila Chadema ni haramu kufanya hivyo bara?

Hilo nalo neno:nono:
 
Back
Top Bottom