CUF Ni Mkombozi wa WaTanzania

Yaani mmeshukuru jamaa wameakhirisha mkutano pale Jangwani ,hayajesha watarudi na kama mjuavyo hawana dogo !Kama unamshtuko wa moyo usikaribie ,usiende ,usisikilize redio wala tv, msije mkawauwa tu na kuwalimboka.
 
Masahihisho....CUF bado inapendwa na Wapemba walio wengi. Huwezi kusema chama kinapendwa na Watanzania wakati bara (ambapo ndiyo asilimia KUBWA ya Watanzania walipo) wahaja pata kiti hata kimoja cha ubunge.
 
Toka lini ugaidi ukaongoza tanzania? Chama cha kidini na wapemba! Kwa taarifa yenu hata kuongoza zanzibar hamuwezi labda muongoze uamsho!
 
Wewe usihangaike kutafuta ofisi za CUF kama una roho mbaya huzioni ,ila kama huna basi bakia huko huko uliko timiza wajibu wako siku ya kupiga kura !usipate shida kumaliza ndara

Mkuu umejuaje?{hapo kwenye red}Kwasasa WATANGANYIKA wengi tunavaa ndara tena zilizotengenezwa na mabaki ya tairi za magari sasa CUF kama chama tawala hii ndiyo sera yenu?au ndiyo maisha bora kwa kila mtanganyika?
,
 
CUF ijipange vizuri kwani sasa ina maadui wakubwa wawili;CCM&Chadema tena kwakua cuf ipo vizuri kisera,wanapandikiza udini ili kuidhoofisha,cuf msikate tamaa waTZ watawaelewa tu
 
cuf ijipange vizuri kwani sasa ina maadui wakubwa wawili;ccm&chadema tena kwakua cuf ipo vizuri kisera,wanapandikiza udini ili kuidhoofisha,cuf msikate tamaa watz watawaelewa tu


wameshindwa kuikomboa zanzibar wataweza kuikomboa tanzania??
 
CUF kwa huku Bara wamepoteza dira kabisa, inabidi wajipange sana, la sivyo ndo mwisho wao!
 
CUF ingefanya ukombozi mahali iliko na nguvu ningekuelewa. Tell us what have you done in Pemba with tangible proof?
 
Msahihisho....CUF bado inapendwa na Wapemba walio wengi. Huwezi kusema chama kinapendwa na Watanzania wakati bara (ambapo ndiyo asilimia KUBWA ya Watanzania walipo) wahaja pata kiti hata kimoja cha ubunge.
CUF na Uamsho dugu moja dhidi ya Muungano, Zanzibar ilipatikana wanahamishia nguvu kuitafuta Jamhuri ya Pemba.
 
Nape ndio nani ? Mimi simuelewi wala sina habari nae ,isiwe amewakurupusha huko mkafikiri na huku atathubutu ,huku hakuna kazi za kitoto ,ni mambo ya watu wazima tu.

Unamaanisha wale ambao hawajaenda suna au?
 
Labda ungeweza pia kujenga hoja yako kwa kueleza hizo pembe zote za Tanzania ambako chama kinakubalika, viashiria vyake nk. mfano uwingi wa wanachama, ushindi katika chaguzi ndogo ndogo. Hii itafanya wachangiaji waelewe hasa unataka kusema nini. Pia unaweza kutaja wale waliokihujumu chama kiasi kikashindwakufikia hazma, na labda mikakati iliyopo ili chama kisihujumiwe tena.


Kumbe bado WaTanzania walio wengi wanaipenda CUF , wananchi wanaimani ya kweli na CUF na wanaelewa majungu na njama za kukidhoofisha chama chao ambazo zimefanywa kwa awamu mbalimbali na wapinzani wao na hata wale wasio kitakia mema Chama hiki cha CUF.

CUf tofauti na vyama vingine kimekubalika kila pembe ya Tanzania kutokana na itikadi zake na sera ambazo zinatoa mwanga kwa kila anaezifahamu na hata kwa yule anaehadithiwa ,ni chama ambacho kama kisingehujumiwa basi leo hii waTanzania wangelikuwa mbali sana kimaendeleo.

Nguvu za CUF zimedumaa kutokana na dhoruba ilizopita na sasa imeanza kupata ahueni na kuanza kujipapatua ili kirudie katika hali yake ya zamani ili kufanikisha malengo yake ya kuliongoza Taifa hili la Tanzania.CUf inaamini kabisa nguvu za wanachama wake bado zipo kwani aliewahi kukipenda chama hiki basi hawezi kukiacha na ikionekana amekiacha basi bado ndani ya moyo wake ipo nafasi ya CUF ni kama wale askari wa akiba ,ambao wakati wowote vita ikitokea huwa wapo tayari kupambana.

Akiba hii ya wanachama ambao ndani yamioyo yao bado CUF imo na wapo tayari kwa lolote lile ,hawa ndio wale walio ngangari kinoma na ndio hazina ya CUF iliyo nyamaza na ipo kimya na ni hazina kubwa sana ,isiyomilikiwa na chama kingine.Karibu mbiu ya mgambo itaitishwa ili kuanza mapambano mepya ya kumrudisha na kuwarudisha maadui nyuma.
 
Tanzania itakombolewa na Watanzania.
Ukombozi wa Tanzania hautakuja mpaka
Watanzania wajikomboe kimawazo.
Tunaweza kubadilisha chama, lakini kabla
ya kubadilisha mawazo yetu, ukombozi NG'O.
 
Back
Top Bottom