Dr. Slaa,mkombozi wa fikra za Watanzania

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
943
1,988
Nakiri wazi kwamba Mimi ni miongoni mwa Watanzania wanaokupenda Sana na ambao wanavutiwa Sana na wajihi wako.

Nilianza kukupenda wakati ukiwa mbunge na wakati huo nilikuwa mwanafunzi wa level ya secondary. Nilivutiwa Sana hoja zako bungeni Na namna ulivyokuwa ukitetea raslimali za nchi kwa serikali kuingia mikataba mibovu.
Kwa mantiki hiyo niligundua kwamba wewe ni moja ya Watanzania wachache waliojaaliwa akili na mwenyezi Mungu.

Umesimama imara kutetea bandari zetu,umesimama imara kuwaelimisha Watanzania kuhusu katiba, umesimama imara kuwatetea Watanzania.umesimama imara kupinga ufisadi. Mwenyezi mungu akubariki Sana. Wewe ndiye mzalendo wa kweli,wewe ndiye kiongozi wa kweli.

Hawa wanaokukamata leo watapita tu kama walivyopita wajinga wengine. Dr.Slaa nikuhakikishie tu kwamba kabla ya kuwa askari Hawa ni Binadamu kwanza hivyo kama wamejisahau kwamba wao ni Binadamu kabla ya uaskari ,mungu analojibu na anajua mwisho wao.

Naamini mungu amechukizwa na watu wanaokamata Watanzania hovyo hasa wale wanaotetea na kuipigania nchi. Hawa siyo Askari Bali ni watesi. Hawa siyo viongozi ni mafisadi. Kumbe wanaimba wimbo wa taifa "mungu ibariki Tanzania" kinafiki. Kumbe wanaimba "dumisha uhuru na umoja "kinafiki leo wanaligawa taifa.

Dr.Slaa,pamoja na kwamba wamekuondolea hadhi ya ubalozi,wewe Bado ni balozi na kumbukumbu zipo na zitabaki kwamba umewahi kuiwakilisha Tanzania nchini Sweden. Uliteuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wa awamu ya Tano na kuapishwa.

Mimi naamini kwamba Rais Magufuli alikupenda Sana na alikuamini Sana. Na alikupenda kwa uwezo wa akili yako na uzalendo wako. Moja ya sifa ya Rais Magufuli ilikuwa ni akikuona una akili alikuwa anakuamini na kukupenda mno.

Mungu hawezi kushindwa na mafisadi analo jibu kwao,tafadhali usirudi nyuma ipiganie nchi yako na nchi itakuhifadhi katika makazi yako ya milele. Ni udongo huu huu wa Tanzania ndiyo utakuzika. Hawa watesi walikuja na watapita lakini nchi itawahukumu siku za mwisho wa uhai wao.

Sisi Watanzania wenye akili tunawaona na tunayo maamuzi yetu huko mbele.

Dkt. Slaa aluta continua. Wewe ni shujaa misri ya samora machel,wewe ni mzalendo wa kweli kama Julius Nyerere. Wewe ni mwamba kama Magufuli.

Enyi watesi maisha ni mapito,kaburi ni tajiri.
Zidumu fikra za Dr. Slaa🇹🇿
 
Zidumu fikra za Dr. Slaa
Aaaah, wewe umeanzia Ubunge? Wa Karatu? Rudi nyuma kidogo, huyu alikuwa Padri. Ni kozi ngumu sana, ni lazima uwe na akili Division 1 unasomea Seminari ndogo na kubwa. Lakini wana masharti, usioe wala usiolewe, mtumikie Mungu tu, milele. Ni kozi ngumu, ukipita ni kazi ngumu. Wapo wanaopita tunawajua, kwa baraka za Mungu si nguvu yao. Kila mtu angependa asome Seminari baadaye awe Padri lakini masharti ya kuoa na kutoolewa yanawashinda. Ni lazima uwe na afya, ukatae tendo la ndoa, ujinyime, siyo kwamba labda huwezi yaani khanithi, hapana.

Of course hii ni siri yako nani atajua? Seminari wana jinsi ya kujua, wana namna zao. Wengi hujaribu, hushikwa kabla ya kumaluz Form 4 au akimaliza hushokwa Form 6 au akimaliza hushikwa University seminari kuu. Ukifika huko baadaye una nafasi nzuri ya kuwa Askofu.

Padre Slaa alisoma Itaga akasoma Kipalapala akasoma PhD Roma, kote alipita "salama", kawa Naibu Paroko, Paroko kamili, hadi akawa Katibu wa Baraza la Maaskofu TEC wakati Papa alipokuja 1990, Naibu wake akiwa Padri Method Kilaini.

Padre Slaa kidogo spewe Uaskofu ndipo wakajua alikuwa na mke na wajukuu, na mahawara wengi tu wengine wake za watu. Wakamfukuza au tuseme ikabidi ajiuzulu.

Akaingia siasa kajiunga na tawi dogo CCM la Dongobesh akaomba ubunge wa Karatu. Kura ya maoni hazikutosha (shauri ya maadili tajwa), CCM watu safi wakamkataa.

Akahamia CHADEMA, baadaye wakamfukuza nao kwa msemo wa Nyerere "wanasiasa malayamalaya tu".

The rest is history.

Do you trust this man? Would you trust such a one? Would you buy a second-had car from him? Ana miaka 75, eti anatetea bandari "zetu" kutokea Tujuyu milimani dhidi ya "Waalabu". Hii inakuingia akilini? Is he genuine, au anatafuta pension ya lalasalama?
 
Ameipigania sana CHADEMA, muda wake wa kumuondoa Mbowe kwenye uenyekiti umefika, Mbowe amepwaya sana,amuachie kiti Dr. Slaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom