Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,140
- 14,678
Kwanini CUF wasiungane kwanza na ADC kabla ya kuifikiria Chadema?...
Mtatiro alivyo mnafiki amechukua zile kata ambazo CUF imepata kura nyingi ili ahalalishe hoja yake.Kwanini asiweke matokeo ya kata zote 29?
Kwani lengo ni nini kuiondoa CCM madarakani, Kwenda Ikulu au kuwaletea wananchi maendeleo? Saidieni maendeleo bila hata kuiondoa CCM madarakani na hapo wananchi wenyewe wataona umuhimu wenu. CCM haiwezi kuondoka madarakani kwa kupnga kuungana bila kujua mnataka kuwafanyia nini wananchi.
Kutokana na hiyo red, nadiriki kukuita wewe poyoyo! Kichwa chako hakina kitu kabisa. Hivi hii mitizamo ya ukristo na uislamu mmeitoa wapi watanzania wenzangu? Mbona hili tatizo linakua kwa kasi ya kutisha?Kweli mfa maji haachi kutapatapa. Vipi ule mgogoro wao wa kuchapana makonde kule Arusha umekwisha na sasa wanataka kuungana? Huyu Mtatiro kweli sasa nimeona anataka kuhamia CDM. Nataka kuwa kama mtabiri, miezi miwili haitapita tutamsikia kule kwa vidole viwili kwani kauli hii ni mpya kabisa kutoka kwa huyu mkiristo.
Cuf zanzibar haijaungana na ccm bali wamegawana madaraka tu,bado cuf ipo pale pale,kilichofanyika ni kuwaletea maendeleo wananchi.Muda huu CCM inaogelea kwenye starehe la utawala kutokana na mifumo duni ya kiuongozi ndani ya vyama vya upinzani, Kuungana kwa CCM na CUF katika GNU huko Zanzibar kumetoa nafasi kubwa kwa CCM kupumua sana bila tatizo, aidha kwa CHADEMA kutokuwa na mipango madhubuti ya kufikia wananchi kwa sera zinazoeleweka kwa urahisi huku Tanzania bara, kunaisidia CCM kuwatumia Wananchi wa Vijijini kupata Ushindi.
Iwapo CUF itarudisha ungangari wake wa siku za nyuma huo ZANZIBAR na CHADEMA ikaimarisha safu yake mikoani na kuacha kuzunguka ziarani tu bila kusimika misingi imara ya chama huku bara niwazi kabisa CCM itaelemewa na na itakuwa ni muda mwafaka kwa wao kuachia.