CUF na CHADEMA waungane kuiondoa CCM madarakani - Mtatiro

Kweli mfa maji haachi kutapatapa. Vipi ule mgogoro wao wa kuchapana makonde kule Arusha umekwisha na sasa wanataka kuungana? Huyu Mtatiro kweli sasa nimeona anataka kuhamia CDM. Nataka kuwa kama mtabiri, miezi miwili haitapita tutamsikia kule kwa vidole viwili kwani kauli hii ni mpya kabisa kutoka kwa huyu mkiristo......


jamani watu wenye mawazo kama jamaa underlined hapo juu mnamsaidiaje
 
Jaman huyu CUF kwani tayari kaachika na mmeo CCM ambaye huwa wanashare TBC?

Kweli CHADEMA ni handsome kiasi hiki hadi CUF wanaanza kujigonga hivi.

VIVA CDM.
 
CDM hakiwezi kuungana na chama chochote kile kwa vile ni walevi wa madaraka! Nani asiyejua? Visingizio vitakuwa viiingi lakini huo ndio ukweli. Mwisho wataanza kubaguana wao kwa wao. Si mliona Zito aliposema anataka kugombea urahisi!

Wote ndani humu walianza mara hili lile! Ah, watu hawa bwana!
 
Msipinge kila kitu anavyozungumzumza ni sawa.kila kitu ni kukaa na kuweka mipango angalia umeya nyamaga ingikuwa kafufu ajaleta noma cdm tungechukua au tarime.lakini kwa sasa imekuwa vita vya panzi furaha ya kunguru (magamba)ni bora tujigawe kwa kanda kusini kafufu na sehemu zenye alkaida wengi.sehemu zingine nikuangali chama gani kina kubalika cha upinzani.
 
CHADEMA na CUF wanatakiwa wafanye kazi kwa kushirikiana.
Waache hizi siasa za maji taka baina yao.

Lilikuwepo pendekezo la kubadilisha sheria ya usajili wa vyama ili iruhusu kuunda "alliance " ya vyama.Hili limepuuzwa na hivyo kuifanya CCM kuendelea kupeta kama mleta mada anavyosema.

Kuindoa kwenye usukani CCM sio kazi ndogo.Kuiondoa CCM madarakani kwa njia za kidemokrasia wakati upinzani wenyewe wanarushiana matope itabakia kuwa ni ndoto.

Kuiondoa madarakani CCM kwa kutegemea kuwa tume ya uchaguzi iliyopo kutenda haki ni sawa na kutegemea tembo kupita kwenye tundu ya sindano. Hata Jaji Bomani alishaonya kuhusu hilo;alisema tatizo sio tume bali sheria inayoounda tume hiyo. Alisema hayo pale alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na alipozungumzia malalamiko ya vyama vya upinzani kuwa tume haitendi haki.

Sio hayo tu, vyama vya upinzani vinaelewa kuwa vyombo vya dola ambavyo vinatakiwa kufanya kazi kama vyombo vya taifa, leo vinafanya kazi pia ya kuibeba CCM lakini bado vinaona ni bora kuendelea kubomoana baina yao na hivyo kuipa CCM nafasi ya kupumua na kupanga mikakati ya kuvimaliza vyama hivyo.

Vyama vya upinzani "vina-bore"!!!

CUF inajisifia kuingiza mguu ndani ya serikali huko Zanzibar, wakati CHADEMA wamefurahi kuongeza viti 3 na kujisifia ongezeko la 60%. Vyama hivi bila kufanya kazi kwa pamoja na kwa ukaribu(sizungumzii kuungana,nazungumzia kushirikiana) ili mtanzania apate "maisha bora" ambayo tokea nchi hii imepata uhuru imekuwa ahadi hewa.

Kuendeleza kwao siasa za majitaka ni kuruhusu nchi hii iendelee kutafunwa na mafisadi na kukubali wananchi ambao wao wanasema wanawatetea, waendelee kugawiwa umaskini na kufanyiwa mazingaombwe.

CHADEMA na CUF kama kweli mna nia njema ya kuwakomboa watanzania kupitia njia za kidemokrasia ni lazima mshirikiane. CCM ambaye ndie ambaye mnajaribu kumfanya awe chama cha upinzani amejijengea kinga(katiba, tume ya uchaguzi,matumizi ya vyombo vya dola) ambayo bila kushirikiana hamwezi kumwondosha kutoka kiti alichokikalia.

Hata pale mtakaposhinda basi atalazimisha GNU kama alivyofanya huko Zanzibar.CHADEMA waulizeni CUF nini walifanmyiwa huko Zanzibar. CUF zungumzeni na CHADEMA.

Nguvu ya umma, ngangari bila mikakati na ushirkiano ni kuwapa CCM na Polisi upenyo/mwanya wa "kutumwangosi na kutulimboka" bila kutufikisha kule mnakotuahidi.

Bado muda na nafasi ipo kwa kutumia njia za kidemokrasia kuisogeza Tanzania mbele.link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/346100-upinzania-sasa-tufanye-nini.html Mtapochangia kuingiza nchi katika vurugu kwa kushindwa kushirikiana hamtoweza kujikosha siku za mbele kwa kusema: "wa kulaumiwa ni CCM tu."

Tayari tunaelewa kuwa CCM ndio ambaye ametujengea Tanzania yenye umaskini, utegemezi wa "wafadhili" hata kwa vyandarua, rushwa imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku,haki haipatikani bila kununuliwa,ufisadi ndio sifa bora ya kuwa kiongozi, uhai wa mlalahoi(mwananchi wa kawaida) imekuwa ni rahisi kuutoa kama polisi wanavyojijengea "heshima mpya" ya kuwa waondosha uhai badala ya kulinda raia na mali zao nk.

CHADEMA,CUF,NCCR,UDP mnatakiwa kuonesha njia mbadala na mpaka mida hii hainekani kama mmejipanga vya kutosha. Bado wananchi wanashindwa kutofautisha utendaji wenu na wa CCM. Tumeshachoka na "Kauli na ahadi" , mko katika bunge pelekeni hoja binafsi/miswada ya kubadilisha sheria, tuanze kubadilisha mfumo. Mfumo haubadilishwi majukwaani,unabadilisha kisheria katika nchi inayofuata demokrasia. Mkienda jukwaani ni kufafanua tu kile mlichokitenda kuleta mabadiliko kwa kuunda/ kubadilisha sheria au kuiboresha sheria husika.

Haya ninayoyashauri sio mepya,yameshasemwa na wengi sasa ondoeni pamba katika masikio yenu na myafanyie kazi.
Kuishtaki CCM kwa wananchi kuwa wanakumbatia mafisadi au rushwa bila kupigania kuundwa kwa tume huru ya kuzuia rushwa na pia kupata watendaji wa tume hiyo wanaoteuliwa au kuthibitishwa na bunge ni kuwatayarishwa wananchi kufanya vurugu. Acheni domo, sasa ni wakati wa kutenda kile mnachokiamini.
 
ni sawa but kwanini tukamilishe mzunguko wa kuwa kwenye duara moja
CUF join CCM
CUF join CDM
Therefore
CDM and CCM are joine together indirect as a result no upinzani tanzania

CUF bana!!!!! sasa wamekuja na wimbo mpya? Alafu wakipanga mikakati na CHADEMA wanakwenda kutoa siri kwa Baba watoto wake (ccm). Hii ni mbinu ya kipumbavu wanayotaka kuja nayo. Sipingi vyama vya upinzani kuunganisha nguvu, lakini sio CUF. Angalia kampeni zao zote lengo ni kupunguza nguvu ya CHADEMA, kama lengo ni kuiondoa ccm ni kwanini nguvu kubwa wanaitumia kupambana na CHADEMA? Pia fedha za kuandaa mikutano sio siri mfadhili wao ni CCM. Wasitake kutupiga changa la macho hawa wanafiki tu.
 
fmpiganaji CUF ni ccm B, wamekuwa wakihujumu vyama vya upinzani, ikiwemo CDM, ndiyo maana kwa msaaada wa ccm wameanzisha V4C ili kuipinga cdm, baada ya kushindwa uchaguzi wanapiga kelele eti cdm waungane nao.

mbona cuf miaka ya nyuma kilipokuwa chama kikuu cha upinzani vyama vingine vya upinzani viliomba viungane na cuf ili kujenga upinzani wenye nguvu mbona cuf walikataa. waliingia kwenye ndoa ya kifisadi na ccm kwa jina la muafaka bila kujua wanajiua kisiasa. waendelee na v4c na cdm nao wataendelea na m4c kisha 2015 wananchi wataamua
 
Last edited by a moderator:
ni sawa but kwanini tukamilishe mzunguko wa kuwa kwenye duara moja
CUF join CCM
CUF join CDM
Therefore
CDM and CCM are joine together indirect as a result no upinzani tanzania

Kwani wewe hujui kuwa CCM na CUF wana serikali ya umoja! Hujui kuwa wana mawasiliano ya nini wafanye pamoja? Hujui kuwa wote wapo kinyume na CDM?
 
CCM Majambazi> Nani asiyejua kwmba chaguzi zote za Zanzibar CUF imekuwa inashinda? Kitu muhimu ni kubadilisha katiba kuwe na tume huru ya uchaguzi na siyo waajiriwa wa serikali (CCM) ndo kuwa marefa
 
Kweli mfa maji haachi kutapatapa. Vipi ule mgogoro wao wa kuchapana makonde kule Arusha umekwisha na sasa wanataka kuungana? Huyu Mtatiro kweli sasa nimeona anataka kuhamia CDM. Nataka kuwa kama mtabiri, miezi miwili haitapita tutamsikia kule kwa vidole viwili kwani kauli hii ni mpya kabisa kutoka kwa huyu mkiristo.

Kweli we ''ngiri'' mtatiro na ukristo inakuaje? P*u*m*b*a*v*u!!!!!!!!!!?
 
Kweli Vita ya Panzi furaha ya kunguru....
Ukisoma comments hapa utagundua watu siasa hawazijui au wanajifanya hawazijui....
Mwisho wa siku CCM Watatawala kwa Miaka 100 ijayo kama wanavyodai....

Hydrobenga,
Ingekuwa hivyo basi kule Zambia MMD(CCM) isingeondolewa madarakani na chama cha PF (CHADEMA) baada ya kusalitiwa na UPND(CUF ya Zambia)
 
cuf wanaweza kuchukua serikali ya zanzibar, sio chadema kuchukua bara hiyo ni ndoto hiki chama wanachama wake ni wakristo ndio tatizo.
 
Copied: CCM ni kweli itakuja ondolewa madarakani, ila sio 2015..
Edited: CCM ni kweli itakuja ondolewa madarakani, ila sio na CDM
 
Muungano wa kutaka kuiondoa CCM madarakani tu unaweza kweli kufanikiwa kuiondoa lakini hautafanikiwa kuliongoza taifa. Utakuwa ni muungano wenye la kuiondoa CCM tu. Ni lazima kuwepo muungano wa maono, sera, malengo, fikra n.k Huwezi kumfunga farasi na ng'ombe halafu ukawataka walime...
 
If the idea is multipartism: Then
CUF + CCM = CCM under control
CUF + CDM = CCM under control + CDM
CCM under control + CDM = CCM Under control

Therefore: CUF + CDM + CCM = CCM Under control
Unaweza kujua nani yuko nyuma ya huu ushauri.

mtatiro hapa kaja na hoja ya msingi,badala ya kutoa hoja mnaishia kuchambana kama mabibi harusi hapa,kweli jf sasa ni jamvi la wambea
 
Nasikitishwa pale wafuasi wa CUF na CHADEMA wanaposemana vibaya na kujenga ukuta badala ya daraja.Kukiondoa madarakani chama kilichodumu zaidi ya miaka 35 ni kazi kubwa inayohitaji umoja na ushirikiano wa vyama vya upinzani.CCM ndiyo waasisi wa mgogoro baina ya vyama vya upinzani (divide and rule) lakini wapinzani wanakuwa kama hawajaliona hilo,wako bize kunyosheana vidole wenyewe kwa wenyewe!
 
Hydrobenga,
Ingekuwa hivyo basi kule Zambia MMD(CCM) isingeondolewa madarakani na chama cha PF (CHADEMA) baada ya kusalitiwa na UPND(CUF ya Zambia)
Siasa za Tanzania si Zambia.....Mimi sijasema CHADEMA Waungane na CUF...Tanzania ni nchi changa sana ...lakini ina utitiri wa Vyama Vya siasa..na kila siku vinaanzishwa vipya....Unajua CCM ina Umri gani ?Unajua CHADEMA NA CUF vina Umri gani ?
Unadhani hamasa za wananchi katika mikutano ya wapinzani zinatosha kuiondoa CCM...Madarakani ?
Unajua kuwa CUF waliamini wanaitoa CCM Madarakani mwaka 2005...unajua nini kilitokea ?
Unajua Kuwa CHADEMA wanaamini wanaitoa CCM Madarakani 2015....unajua nini Kitatokea....?

Stay Tuned
 
Muungano wa kutaka kuiondoa CCM madarakani tu unaweza kweli kufanikiwa kuiondoa lakini hautafanikiwa kuliongoza taifa. Utakuwa ni muungano wenye la kuiondoa CCM tu. Ni lazima kuwepo muungano wa maono, sera, malengo, fikra n.k Huwezi kumfunga farasi na ng'ombe halafu ukawataka walime...

-Mfano rahisi ni Zanzibar sasa hivi kuna serikali ya mseto kati ya CCM na CUF are they doing better?
-Halafu hii tabia ya kugawana madaraka na kulenga kushinda uchaguzi inadumaza fikra za taifa hili.Hatupiganii kubadili sura za watu ikulu ama rangi za chama tawala tu,bali reform kupitia itikadi,sera na muono kupitia dira ya muda mfupi,w kati na muda mrefu.Itakua ni makosa makubwa sana ku-narrow agenda zetu hadi iwe tu kushinda uchaguzi.

Ni jambo la hatari zaidi hoja hii inapotolewa na vijana ambao wamebeba tumaini la kubadili mtazamo wa kisiada kuhusu mabadiliko.Tukua tunaanda kizazi kile kile chenye mtazamo wa kushinda uchaguzi tu

Reform process baada ya kushinda uchaguzi itategemea sera na vision pamoja na commitment.Na huwezi kuwa commited kwenye kitu usichokiamini....
 
Back
Top Bottom