CUF na CHADEMA waungane kuiondoa CCM madarakani - Mtatiro

Msimamo gani unao uongelea hapa? Kwenye hii thread anaonesha kuhitaji ushirikiano lakini leo hii hataki na kakataa mwaliko!

Huyu ni kigeu geu tuu hana lolote!

Ni BORA kuonesha msimamo, and Mtatiro is always doing that.
 
Hivi unajua huo ushirikiano alio kuwa ana uongelea mtatiro hautaki tena? Kapewa mwaliko wa mkutano wa pamoja kakataa na kuleta mipasho!

Mtatiro is not strong but flip- flop politician!

Nadhani hii ilikuwa njia ya kuanza ushirikiano alaf yeye analeta mambo ya watoto na huo ni ushahidi mwingine wakuwa cuf na maccm lao moja!

Malemo, again Mtatiro is logical, ingekuwa chadema wana hizo nguvu za tsunami, ilikuwaje CCM wakashinda kata 22 chadema 5 tens mbili zikiwa za leap kabla na CUF wakashinda moja mpya. Na ukisoma vizuri kwenye hiyo analysis Mtatiro anaonesha kuwa, kama kungekuwa na CONSENSUS tangu awali, upinzani ungeshinda kata nyingi sana. Mtatiro hasemi CUF ingeshinda, anasema upinzani ungeshinda, unafiki wake uko wapi? Tatizo letu, tunapenda watu, hatupendi logics wanazotoa. Swali langu hapa ni kuwa, ikiwa CDM ni tsunami, imekuwaje wamepigwa 22 - 5? Na preucaution aliyoitoa Mtatiro ni "very strong", kwamba ni rahisi kuishinda CCM mkipambana katika uchaguzi wa kijiji kimoja, kitongoji kimoja, kata moja au jumbo moja - lakini anatoa onyo kwamba kuishinda CCM kwenye chaguzi za vijiji vingi, kata nyingi, majimbo mengi n.k. ni kazi kubwa na inahitaji upinzani waache ubinafsi. I think the guy is very clever, tatizo lililoko hapa ni kwamba tunamchukia because we wanted him to be CDM and he is not. Mimi husoma sana maandiko yake between the lines and I find him to be one of the very strong politicians.
 
ni rahisi kufikiria kuungana lakini kiukweli ni vigumu kuliko tunavyodhani kwa sababu ukweli ni kwamba hawa watu hawana msingi wa kuunganishwa kwao, nikitazama naona Nccr inaweza kuungana na Chadema lakini Cuf wapo ki zanzbar sana, na kama kama wataungana ili washinde tu uchaguzi hofu yangu ni kwamba tunaweza tukawa na chama dhaifu sana madarakani kwa sababu wanaweza kuanza kupingana kwa baadhi ya mambo muhimu kwa taifa letu, hii ni hatari kwa maslahi ya wananchi kuliko hata ufisadi
 
Back
Top Bottom