Clouds mnaudharaulisha Wimbo wa Taifa

Upuuzi mtupu wimbo wa taifa kuchezewa vile na pia nimaona matangazo(banners) za mchezo wa kuigiza wenyewe wanaita sinema eti mr president Ina nembo ya Bibi na bwana ambayo Mara nyingi naiona katika nyaraka za serikali huu ni upuuzi mwingine
SERIKALI LEGELEGE
 
Pengine Washagundua Wimbo Hauna Hati Miliki So Mzee wa Loose Ispekta Haroon Hatochelewa aibuke Tena kwa Remix
 
Niliwahi kusikiliza taarifa yao ya habari wakati ndo wameanza kusoma taarifa ya habari. Sikupenda kabisa, yaani ilikuwa ni uhuni kabisa. Hiyo ya wimbo wa taifa sijausikia lakini mkumbuke wengi wao hawa jamaa wameanzia u-DJ. What do you expect from those kind of people? Na kama wahusika wa maadili wakikaa kimya ndo basi tena. Ndo bongo lakini...
 
Kama ilikua ni kusherehekea miaka 50 ya uhuru si imeshapita jamani? Hivi ni kweli wahusika hawajalisikia hili au ni sawa tu vile yule dada anavyoimba wimbo wa taifa kihuni vile?? Wahusika hebu fuatilieni tafadhali kwa nini wimbo wa taifa unapigwa kama kibwagizo au tangazo hivi tena kila wakati.....hii ni aibu kwa taifa zima kwa kweli.
 
wana mpango wa kuufanya tuwe tunaucheza kiduku... :lol:

kwa kweli mana nimeusikia nikiwa ktk duka flani nikinunua vocha na pembeni kulikua na mtoto wa miaka kama 9-10 anafatisha ule wimbo huku kanachezacheza.....kwa kweli si sawa
 
ndio tatizo la kuwa swahiba na rais...si naskia wako bega kwa bega na mkulu? hata wakiimba huo wimbo kwa jinsi wanavyotaka na kwa mazingirayoote yale hawatafanywa kitu....hiyo ndiyo editing ya ile studio yetu ya Tanzania fleva unit...
 
mimi ninakereka natamani niwatume al-shabab waiteketeze mitambo ya clouds ili nisiusikie tena maana clouds imeshaanza kunikera
 
Jamani mie nimetokea kusikiliza wimbo wa Taifa uliofanywa tangazo na hawa clouds,naomba nipate mwongozo,nani kawaruhusu kuuchezea?wanaimba vibaya,hovyohovyo,zamano ilikuwa ukisikia wimbo wa taifa unajua kuna jambo.

Naomba kueleweshwa
 
Kwa heshima na taadhima naomba kuwafikishia ujumbe huu Wamiliki wa Clouds FM juu ya wimbo wa Taifa ambao umekuwa ukipigwa sana kwa sasa kwenye radio hii.

Wimbo huu unaopigwa siyo wimbo halisi wa Taifa letu, umeongezwa vionjo vya aina ya akapela hivi na midundo lakini mapungufu makubwa zaidi ya huu wimbo ni kwamba umeimbwa ubeti mmoja tu wa mwisho. Hii kwa imani yangu kwa taifa hili naiona kuwa siyo sawasawa na ni vizuri kuikemea ili usiendelee kupigwa.

Naomba uongozi, Kaka yangu Joseph uliangalie hili kwa makini zaidi, nakubaliana na ubunifu ambao umekuwa ukifanyika na timu yenu kwenye mambo mengi lakini hapa kwenye wimbo wa Taifa nashauri tuuache ubaki vile vile. Tayari mtaani kwetu watoto wanaimba wimbo huo mpaya kama vile ndiyo wimbo wa taifa.

Kwa uelewa wangu na kwa kutembea kwangu, wimbo wa taifa unaweza kuimbwa tofauti lakini kwenye majukwaa ya live consert na hairuhusiwi kurecord. kwa sababu kuna madhara mengi sana ya kuupiga wimbo wa taifa kwa utofauti. Mojawapo ya madhara ni kwamba watoto wanaokua hawataelewa waushike wimbo upo tayari umebadilisha nembo mojawapo ya utaifa wetu.

Kwa kuwa hata watu wazima hawawezi kuuimba wimbo wetu wa Taifa ni vizuri mtusaidie basi kuwa mnaupiga wimbo halisi ili wengine waweze kuendelea kujifunza kutokea kwenu.

Naomba kuwasilisha
 
Wewe kama bado una muda wa kuisikiliza radio hiyo usituletee ulichosikia humu forum kwani wengine hatusikilizi radio hiyo na wala hatuhitaji kusikia wanafanya nini sawa mkuu!
 
hawa wengine ni wafanyakazi wa clauds wanataka kuikuza redio tuuu!
 
Me mwanzo nlifikiri wameremix TZ TZ nakupenda kwa mooyyooo wote, kumbe Mungu ibariki Tz ilbidi nigande mdomo wazi
 
Mimi nashangaa kuona unendelea kupigwa tuu yaani unatia kichefuchefu kusikiliza, nilidhani nimeliona mi peke yangu, akhhhhhhhhhhhh
 
Mnategemea nini kwa redio inayofadhiliwa na serikali ya uingereza!!!!!!
 
Clouds fm wameuwekea swagger wimbo wetu wa taifa, hivi wamepewa mamlaka na nani au mtu yeyote ana ruhusa ya kuufanya atakavyo. Maana walivyo ufanya sasa ukipigwa huwezi kusimama wima lazima utachezesha kichwaa, au mikono au mguu!!!
 
Clouds fm wameuwekea swagger wimbo wetu wa taifa, hivi wamepewa mamlaka na nani au mtu yeyote ana ruhusa ya kuufanya atakavyo. Maana walivyo ufanya sasa ukipigwa huwezi kusimama wima lazima utachezesha kichwaa, au mikono au mguu!!!
Ni "REMIX"
 
Back
Top Bottom