Hongera Clouds FM kwa kupiga wimbo wa taifa kila siku lakini msiutumie kama kitambulisho cha kipindi

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,969
Clouds FM wamekuwa wakiutumia wimbo wa taifa kila siku asubuhi saa moja kutambulisha taarifa yao ya habari. Kituo chao dada pia cha Choice FM nako nimewahi kuusikia wakiupiga. Ni jambo jema wanafanya kwani ni sehemu ya kuonesha uzalendo lakini kwa hadhi ya wimbo wa taifa, kwa maoni yangu nadhani siyo sahihi kuutumia kama kitambulisho cha kipindi au habari inayofuata kutokana na hadhi yake.

Wimbo wa taifa hutumika kwa matukio maalumu na kila mtu anapousikia huwa anahisi kuna jambo na kuwa tayari kupokea taarifa au tukio lolote kubwa la kitaifa. Hivyo kuutumia kila siku kutambulisha taarifa ya habari ni kuushushia hadhi yake kwani utaonekana ni wa kawaida sana na kupoteza maana hasa ukichukulia kuwa ni moja ya nembo za taifa ambazo maana na matumizi yake ni ya kitaifa na zimewekewa maelekezo na masharti ya matumizi yake ndiyo maana mtu huwezi kupeperusha bendera ya taifa kwenye gari lako au nyumbani kwako bila kuwa na hadhi na idhini hiyo ingawa nayo sasa tunaanza kuona hata baadhi ya viongozi wakianza kuidunisha kwa kuishonea kwenye suti zao.

Baadhi ya matumizi ya wimbo wa taifa yaliyoelezwa ni pamoja na wakati rais anakagua gwaride rasmi, tangazo kubwa la kitaifa ambalo hutolewa na rais au kuhusu tukio kubwa kama mfano kifo cha kiongozi mkubwa, kwenye michezo ya kimataifa ambako wimbo wa taifa wa kila timu hupigwa, kabla rais haja hutubia taifa, wakati wa kupandisha bendera ya taifa na wakati vituo vya redio na televisheni vya taifa vinapomaliza matangazo yao kila siku (in case vinafunga matangazo)

Wanachofanya Clouds FM ni kizuri lakini hawajaangalia upande wa pili kuwa kwa hadhi yake wanaufanya wimbo huu uonekane ni wa kawaida sana kiasi kwamba kila mtu anaweza kuutumia atakavyo na kupoteza uzito wake. Mimi nawashauri Clouds FM wautumie wimbo wa kuonesha uzalendo (Patriotic song) wa Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote zile beti mbili za kwanza inatosha kabisa. A National Anthem is a sacred song. Ni maoni yangu.
 
Niliusikia leo asubuhi nikawaza kama wewe. National anthem sio wa kuimba ovyo ovyo.
 
Acha upigwe kuna watu wasiposikiliza watasahau kuimba wimbo wa taifa lao
 
mbaya zaidi ni endapo wimbo wa taifa upigwe halafu kinachofata ni shilawadu
 
Back
Top Bottom