Clouds mnaudharaulisha Wimbo wa Taifa

Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,703
3,653
Wadau tokea majuzi Nimesikia Wimbo wa Taifa la Jamhuri la Tanzania Ukipigwa Kwenye Radio Ya Clouds FM Cha kushangaza huu Wimbo Umegeuzwa kama Kibwagizo unapigwa Ovyo Ovyo Na Kibaya Kabisa huo anayeuimba ana sauti mbaya iliyobanwa na Pua tena inawezekana huyo muimbaji aliyeimba pengine aliuimbia alipokuwa Washroom. kwa ujumla kila atakae usikia hatoweza kuupenda.

Huyu Mkurugenzi wa Clouds FM Mr. Kusaga asiachwe hivi hivi kwani hili nadhani ni kosa kwani huu wimbo kila mtanzania akiuimba au kuusikia ukiimbwa huupa Heshima zote na hili tulifundishwa Zamani.

Kama JK ana hisa na Hiyo Radio, Wote waombe Radhi kwa kuruhusu hili
 
Kweli huo wimbo mi pia huwa unanikwaza sana, embu pata picha kesho uimbwe vile uwanjani,dharau kubwa sana.
 
Naungana na wewe Kwa Kweli nadhani ni wanapiga wimbo ulioimbwa na Lady JD amebadilisha melody anauimba kama wimbo wa dansi haiwezekani wimbo wa taifa ukadharauliwa namna hii kama wiki mbili sasa wananiudhi sana kwa kweli hivi wizara ya utamaduni hawaezi kulinda hata wimbo wa taifa ykaheshimiwa hii nchi bwana kweli ni kichwa cha mwendawazimu
 
Mi nikiusikia nabadilisha station!sauti ya yule dada anayeimba zinanitia kinyaa!anajikaza sana!
 
Mkuu nakubaliana na wewe, si tu anaudharaulisha lakini kubadili jinsi unavyoimbwa wameuharibu kabisa, binafsi wananikera!
 
They are triying to be creative, lakini kuchamba kwingi...
Wasouth walipoingia ubi na Air Tanzania, walitengeneza radio jingle wakifananisha wimbo wao na wetu. Ilikuwa ni creativity ya hali ya juu, lakini ulileta usumbufu na kuishtua watu sana, wakacomplain na ukapigwa ban !
 
Kuna kituo huko south Africa walipigwa stop kwa sababu ya kuusharobaro wimbo wa Taifa
 
They are triying to be creative, lakini kuchamba kwingi...

U creative kwenye Wimbo Wa Taifa?? oi

Waache Upuuzi Wao kuharibu Wimbo wa Taifa hadi Bunge lipitishwe Sheria ya Kuubadilisha na Raisi Atie Sahihi Yake Tujue Moja kwa Mtindo Huu hata Mpoki Atakuja Kuimba auite Shangazi Ibariki Tanzania...
 
Wanausharobarosha wimbo wa Taifa? Mwisho hata gwaride wataligeuza kiduku na hautasikia wakichukuliwa hatua
 
hivi hii radio bado mnaisikiliza tu ..
Sometime Lazima Utasikiliza tu ni Chombo cha Habari Huwezi Kikwepa na Katika Kutafuta Tafuta Stesheni Utajikuta tu Umesikiliza hata Kama Hutopenda
 
Nimeusikia.Hawautendei haki wimbo wa Taifa kama alama muhimu ya Taifa.Wapuuzi kweli.Ndio matatizo ya kuchanganya kazi na bange.
 
Duuh!juz nimeusikia,kigoma clouds ndo imeanza,nikajiuliza sana,kama mwaka jana wazir alipiga marufuku watu wasiweke wimbo wa taifa ringtone ktk simu,iweje clouds wanauchezea,mfano mwaka wanafunz fm2 wameulizwa ktk mtihan wa taifa,kuwa wimbo wa taifa unapigwa katk matukio gani,nao ndo wadau wa cluods,waheshimu vitu vya taifa
wakatabahu
 
Sipati picha 2015 rais dr w.slaa waziri wa habari michezo na utamaduni awe sugu!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom