Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Mkuu katika zote nimeiipenda hii, ndio maana ni muhimu kuwa na shule za kata maana tutapata hata vyuo vya tarafa, watu kama akina Gadner wasiwe wanaenda Roben Island wakidhani ukifika huko umemaliza kila kitu. Kuna watu hawajatia timu huko lakini wanajua kila angle ya ile jela, Gadner jielimishe mwanangu, suala la Biashara za siraha ni suala kubwa mno kwa hawa vijana wazee wawili (Gadner na Kibonde). kwanza sio Vijana any more nadhani waache kutangaza sasa waachie vijana wenyewe. Wakati ule akina Amina wanatangaza they were real young,
mkuu hapo nawe umeniacha hoi, hizi shule zetu za kata zisizo na walimu, hazina maabara, hazina maktaba wala vitabu halafu wewe unapendekeza tuwna vyuo vya tarafa? huoni hiyo ni sawa na kumkuta mtu amezama mtoni ila ameshikilia tawi la mti ulio inamia mtoni wewe ukaamua kuukata ili kumrahisishia safari ya kuzimu!!?? We unategemea tukiwa na vyuo vya kata wahadhiri/wakufunzi tutawatoa wapi? maabara/karakana na vifaa husika vitatoka wapi? muhimu ni kuwashawishi hao ndugu zetu "watangazaji" wa redio clouds wasiogope umande wa taaluma ya utangazaji.