Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Ni kweli,pia kwa level ya chama sasa Multi-track Diplomacy (kuna kitabu kilichoandikwa na Ambassador John W. McDonald) ni muhimu na kuzingatia kanuni zake katika utendaji wa kurugenzi ya mambo ya nje kwa chama kinachosubiri muda mchache kuchukua dola .Ndiyo maana ukiangalia uchaguzi wa kenya 2007,ODM walikuwa wamejiandaa sana kwa hili na Zambia Patriotic Front.
Ukiangalia Congo-Kinshasa hawa jamaa wa upinzani walishindwa katika hili ndiyo maana hata chama tawala kikawa na uwezo wa kufanya ghiliba kama ilivyoelezwa katika ripoti ya waangalizi wa uchaguzi.Tshisekedi na chama chake walijikita kwenye millitary zaidi na kusahau kanuni ya kinyonga kwenye msingi wa diplomasia 'Hatua za kidiplomasia zina militarism kama background'.Chama tawala kilijua zaidi ya upinzani kujipanga ndani lakini walikuwa hawajaandaa kuwashawishi jumuiya ya kimataifa na kuweka mechanism za kuungwa mkono hata kama watawafanyia ufedhuli/uchakachuaji.
Kama unapenda kusoma vitabu jaribu kutafuta hivi vitabu (Stone, Diane. (2004) 'Private Authority, Scholarly Legitimacy and Political Credibility pia kuna virtabu hivi 'Think Tanks and Informal Diplomacy', by Timothy J. Sinclair '
Ben twend mbele turudi nyuma unaonekana ulikuwa umejiandaa vya kutosha kupewa hayo madaraka ama mengine sawa na hayo! Unaonekana unaongelea kwenye corridor za UN pale New York City ambapo watu huwa wanapigana vikumbo kuhakikisha diplomasia zinafanya kazi kwa kuwaghilibu wengine kidiplomasia! Mkuu unaonekana umezama kwenye Diplomasia ya Kimataifa. Tatizo ni kwamba kuna siasa za vyama vyetu ambazo hazitaki diplomasia bali mtulinga. Ukiwa mwanadiplomasia unaonekana mwoga ukiwa wa mtulinga bila hoja unaonekana shujaa!