Kwa nini hawakumkata mikono kabisa ashindwe kutype ugoro humu?
Mtatiro hajamwambia mwandishi yeyote kuhusu suala la usaliti wa chadema igunga.
Hutu aliyeleta mada hii aseme ni gazeti lipi na mwandishi yupi.
Pia mtatiro siyo mratibu wa kampeni za cuf igunga, mratibu wa kampeni zetu ni shaweji mketo, naibu mkurugenzi wa uchaguzi cuf taifa. Kuna watu humu wasipomshutumu mtatiro kwa maneno ya uongo na vijembe hawaoni raha. Mtatiro anabakia kuwa kiongozi makini na ambaye amesimamia historia ya mapambano na hadi leo hana rekodi ya udhaifu katika uongozi wake.
Mtatiro aliamua kujiunga cuf kwa utashi na akili yake na hakulazimishwa na mtu, kuwa kwake cuf kusiwe hoja kwa wanaoichukia cuf.
Mimi ni mohammed mtutuma - msaidizi maalumu wa mhe. Mtatiro
sasa kama ccm na cuf wakipeleka ben na sharif, nani mpinzani? Let us be logical guys

mbona yeye alijua hashindi lakini alienda UBUNGO badala ya kwenda MUSOMA VIJIJINI

mbona TARIME CUF waliharibia CHADEMA kwa kugawa kura zaidi ya 7000

mbona hazungumzii KIGAMBONI jinsi wapinzani walivyogawana kura

au MTATIRO naye ameanza kutumia akili za kwwnye MASABURI

Ndoa ya kwanza ilikuwa kule Kigoma, sijui ya nani ile? hii ya CUF ya pili na imefana sana, wana makamu wa Rais. Unalo?
Bora tuwe wakweli Vyama vya siasa havitafika mbali kama havitokuwa na tabia ya kuachiana majimbo. Kama kweli CUF ina nguvu zaidi ya CDM basi CDM waiachie CUF Igunga vinginevyo ni kuwapa CCM ubwete wa kushinda.

halafu mbona wanatumia nguvu sana(magamba) si walisema upinzani ni vyama vya msimu?
huu wehu sasa,badala ya kwenda kueleza sera mnaenda kuelezea chadema,si upumbavu mnaenda kufanya,we are tired of u,peoples power 4 evermratibu wa kampeni wa cuf julius mtatiro ameishtumu vikali chadema kwamba kiimeenda igunga kwa lengo la kugawa kura za cuf.mtatiro amesema chadema wanajua wazi hawana nguvu yoyote igunga lakini wameamua kwenda huko ili ccm ishinde.mtatiro amemueleza mwandishi wa habari hizi kwamba chadema wasijidanganye kuambulia hata nafasi ya pili bali watakuwa namba 3 nyuma ya ccm na cuf.mtatiro amesema cuf wamejipanga kuwaeleza wananchi wa igunga ukweli wote kuhusu chadema ili waamue wenyewe.
Kwanini CUF wasiachiane na CCM?

mwenye macho haambiwi tazama,cuf wamechimbia mizizi igunga tokea yaanze mageuzi,chadema hata tawi wa walikua hawana wamekurupuka juzi kwakua kuna uchaguzi mdogo,tatizo chadema wanatamaa mno na wanajidanganya kwandoto zamchana,cdm wangewaachia cuf wenye nguvu kubwa igunga jimbo lingechukuchuliwa na upinzani,ila kwa tamaahizi za cdm naweza sema wazi tayari ccm wameshashinda na wanasubiri kuapisha mbungewao tu.

Mtatiro hajamwambia mwandishi yeyote kuhusu suala la usaliti wa chadema igunga.

Hutu aliyeleta mada hii aseme ni gazeti lipi na mwandishi yupi.

Pia mtatiro siyo mratibu wa kampeni za cuf igunga, mratibu wa kampeni zetu ni shaweji mketo, naibu mkurugenzi wa uchaguzi cuf taifa. Kuna watu humu wasipomshutumu mtatiro kwa maneno ya uongo na vijembe hawaoni raha. Mtatiro anabakia kuwa kiongozi makini na ambaye amesimamia historia ya mapambano na hadi leo hana rekodi ya udhaifu katika uongozi wake.

Mtatiro aliamua kujiunga cuf kwa utashi na akili yake na hakulazimishwa na mtu, kuwa kwake cuf kusiwe hoja kwa wanaoichukia cuf.

Mimi ni mohammed mtutuma - msaidizi maalumu wa mhe. Mtatiro
Sijaongelea suala tajwa hapo juu,
nadhani CHADEMA wamekuja Igunga kama chama cha siasa na CUF tupo Igunga kama chama cha siasa, so ni kiasi cha kusubiri kipenga kipulizwe ndio tutajua nani alikuja kugawa kura za mwingine, nani CCM B au C n.k.
Kwa sasa ni mapema mno kupeana shutuma hizo za uongo, mimi nawaheshimu chadema kama chama cha siasa na sina ugomvi na uwepo wao Igunga.
Jambo lingine muhimu ni kuwa hii forum inaheshimika sana, kuna baadhi ya wadau wanajiunga hapa kuja kupotosha umma au ku_dogoesha watu fulani, yote haya hayatusaidii ikiwa bado watanzania wanashughulikiwa na sera za CCM. Hii ni forum muhimu sana na ninaogopa ikiwa itageuzwa kuwa mahali pa propaganda za vyama na masuala yasiyo na tija kwa jamii na taifa. Hali hii ikiendelea kufurahiwa itaharibu sura halisi ya forum na malengo yake.
Mimi ni kiongozi wa juu wa CUF na niko CUF kwa akili na utashi wangu na wakati najiunga CUF vyama vingine vyote vilikuwepo na sikuamua kujiunga navyo. Nitasimama CUF na kuijenga CUF , sitakimbilia kwenye vyama ambavyo vinaonekana vina mafanikio, nitapambana hapahapa nilipo na kuyatafuta mafanikio ya watanzania hapa hapa CUF.
Nawashukuru wote wanaoniunga mkono, wanaonikosoa kwa makusudi, bahati mbaya , kwa malengo mazuri au mabaya, sote tu watanzania na hatuna cha kuchekana.
Wasalaam,
Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu(CUF),
TANZANIA Bara.
03/09/2011