Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro ameripoti kwenye kituo chake kipya cha kazi Shinyanga

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
MTATIRO AKABIDHIWA MIKOBA SHINYANGA
IMG-20240312-WA0022.jpg

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Wakili Julius Mtatiro ameripoti kwenye kituo chake kipya cha kazi ili kuanza majukumu ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga.

Katika kikao kifupi cha makabidhiano ya ofisi, kilichohudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya hiyo na Wakurugenzi 2; Manispaa na Shinyanga Vijijini, DC Mtatiro amekabidhiwa nyaraka mbalimbali, zikiwemo Taarifa ya Wilaya, Katiba ya Tanzania, Ilani ya CCM 2020 - 2025.
IMG-20240312-WA0019.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza Bi. Johari Samizi ambaye amehudumu kama DC Shinyanga kwa kipindi cha mwaka mmoja, ndiye amemkabidhi ofisi na mamlaka kwa DC Mtatiro.

DC Mtatiro amesema ameridhishwa na kasi ya maendeleo inayoendelea wilayani Shinyanga na kwamba anajipanga kushirikiana kwa dhati na viongozi, wadau na wananchi wote ili kazi ya Mkuu wa Mkoa na Rais Samia iwe nyepesi.
IMG-20240312-WA0023.jpg

Mtatiro ameahidi kuja na mpango kazi kabambe ambao utaendelea kuipaisha Wilaya ya Shinyanga na wananchi wake kiuchumi huku akisisitiza kuwa kipaumbele chake ni "haki" za wananchi.
IMG-20240312-WA0020.jpg

Mara baada ya makabidhiano hayo, DC Mtatiro ameanza safari kuelekea Tunduru mkoani Ruvuma ili kukabidhi Ofisi ya DC Tunduru kwa Mkuu wa Wilaya hiyo wa sasa, Simon Chacha, ambaye kabla alikuwa DC Sikonge, mkoani Tabora.

Faraja Stanley,
Shinyanga,
12.03.2024.
 
hivi kwa wanaomjua, pale usoni aliumia au ni signo?
Ni muislamu anaitwa Julius kuna mwingine nilikutana naye anaitwa Abdallah ni mkristo tena mchungaji kanisa la pentecostal mlokole nikashangaa ila sasa hivi sishangai nikimkuta mtu anaitwa Julius halafu muislamu na ana Sigda
 
CCM killed the young man charisma and talent. Lipumba na Maalim ndio waliiona tunu na kipaji cha huyu bwana mdogo, mimi nilishuhudia maana akikuwa mbele yangu hapo Mlimani.
Kile kipaji cha kujenga hoja na kuzitetea, uwezo mkubwa wa kuhoji na kutetea hoja siouni tena kwa huyu jamaa. Kweli hakuna mkate mgumu mbele ya chai.
 
Huyu mwamba hakuna anachojua ni mweupe sana kichwani. Nimesoma naye udsm 2007 namjua sana.
Nina Uhakika ulikuwa na Kipimo chako cha ubora Kichwani. Niambie wewe saizi na hicho Kichwa chako unasomeka pande zipi.
Ni Muhimu kuwaheshimu Watu hasa ullosoma nao maana inakuletea Faraja kuwa Mungu Darasa lenu ameliona. Sasa Wewe Badala ya Kumshukuru Mungu kwa hillo wewe unaleta porojo.
 
Majukumu ya DC yangeongezewa kuwa majukumu ya DED ILI tupunguze mzigo Kwa serikali!
nchi hii ni maskini, matumizi ni makubwa mno.
 
Majukumu ya DC yangeongezewa kuwa majukumu ya DED ILI tupunguze mzigo Kwa serikali!
nchi hii ni maskini, matumizi ni makubwa mno.
Mtatilo ana uwezo wa kufanya kama dc na ded at the sametime. This man will be able to be the country president
 
Back
Top Bottom